Showing posts with label MICHEZO. Show all posts
Showing posts with label MICHEZO. Show all posts

BARCELONA NA PSG ZATINGA ROBO FAINALI LIGI YA MABINGWA ULAYA

Lionel Messi akishangilia na wachezaji wenzake wa Barcelona baada ya kufunga bao la kwanza dakika ya 67.
Pablo Zabaleta wa Man City akitolewa kwa kadi nyekundu baada ya kupewa kadi ya pili ya njano.
Wachezaji wa PSG wakifurahia kutinga Robo Fainali.
Patashika wakati wa mtanange huo.
TIMU ya Barcelona imeibuka na ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Manchester City kwenye mpambano wa Hatua ya 16 Bora ya Michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya uliopigwa Uwanja wa Nou Camp nchini Hispania na kufanikiwa kutinga Robo Fainali ya michuano hiyo.
Kwa matokeo hayo, Man City wameondolewa kwenye michuano hiyo kwa kufungwa jumla ya mabao 4-1. Nayo timu ya PSG ya Ufaransa ilifanikiwa kutinga robo fainali ya michuano hiyo baada ya ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Bayer Leverkusen. Leverkusen wameondolewa baada ya kufungwa jumla ya mabao 6-1.

Soma Habari Kamili

ARSENAL NJE LIGI YA MABINGWA, ATLETICO YAPETA!



Arsenal imeshindwa kufuzu hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Bayern Munich, kwenye Uwanja wa Allianz Arena jijini Munich, jana hivyo kutolewa kwa jumla ya mabao 3-1 kwa kuwa katika mechi ya kwanza Arsenal ilifungwa mabao 2-0.

Mfungaji wa Bayern alikuwa ni Bastian Schweinsteiger katika dakika ya 54, Arsenal ikasawazisha kupitia kwa Lukas Podolski katika dakika ya 57 kwa shuti kali baada ya nahodha wa Bayern, Philipp Lahm kujichanganya.
Mechi nyingine ya ligi hiyo ilishuhudia Atletico Madrid ikitoa kipigo cha mabao 4-1 kwa AC Milan, hivyo kusonga mbele kwa jumla ya mabao 5-1, wafungaji wa Atletico wakiwa ni Diego Costa dakika ya tatu na 85, Arda Turan (40) na Raúl García (70), huku ikikumbukwa kuwa Milan ilichapwa bao 1-0 katika mechi ya kwanza.
Bayern Munich: 1-Manuel Neuer; 21-Philipp Lahm, 4-Dante, 8-Javi Martinez, 27-David Alaba; 6-Thiago Alcantara, 31-Bastian Schweinsteiger; 10-Arjen Robben, 19-Mario Goetze, 7-Franck Ribery; 9-Mario Mandzukic
Substitutes: 22-Tom Starke, 5-Daniel van Buyten, 13-Rafinha, 17-Jerome Boateng, 25-Thomas Mueller, 39-Toni Kroos, 14-Claudio Pizarro
Arsenal: 21-Lukasz Fabianski; 3-Bacary Sagna, 4-Per Mertesacker, 6-Laurent Koscielny, 5-Thomas Vermaelen; 8-Mikel Arteta, 11-Mesut Ozil, 15-Alex Oxlaide-Chamberlain; 19-Santi Cazorla, 12-Olivier Giroud, 9-Lukas Podolski
Substitutes: 13-Emiliano Viviano; 25-Carl Jenkinson, 7-Tomas Rosicky, 20-Mathieu Flamini, 44-Serge Gnabry, 45-Isaac Hayden

Soma Habari Kamili

TFF YAIOMBA RADHI SERIKALI KWA UHARIBIFU WA VITU KATIKA UWANJA WA TAIFA ULIOSABABISHWA NA VURUGU ZA WATAZAMAJI


Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) tunalaani vikali fujo na uhabirifu wa mali unaofanywa na washabiki viwanjani wakati mechi mbalimbali zikiwemo zile za kimataifa na ligi za hapa nchini.
  
Tunaiomba radhi Serikali kwa uharibifu wa viti uliotokea kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Yanga ya Tanzania na Al Ahly ya Misri iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 
 
Uharibifu huo wa viti umesababisha hasara ya sh. milioni 15 kwa wamiliki wa uwanja huo ambao ni Serikali. TFF tutalipa fedha hizo kwa Serikali kutokana na uharibifu huo. 
 
Tunaendelea kuchunguza tukio hilo, huku tukijiandaa kutoa adhabu kwa klabu na washabiki husika kulingana na kanuni zetu. Adhabu itakuwa kali ili iwe fundisho kwa wengine.
 
Kwa mujibu wa Serikali, viti kumi viling’olewa na kutupwa ovyo ovyo uwanjani wakati vingine 40 viliathirika kutokana na vurugu za watazamaji hao. 
 
Tumebeba dhamana ya kulipa uharibifu huo kwa vile TFF ndiyo wenye dhamana ya kusimamia mechi za kimataifa, na ndiyo tulioomba idhidi ya kutumia uwanja huo. 
 
Kwa vile sasa baadhi ya washabiki, wapenzi na wanachama wa klabu mbalimbali nchini wanataka kufanya suala la uharibifu kuwa la kawaida na mazoea, Serikali inakusudia kuchukua mapato yote ya mchezo husika endapo kutatokea uharibifu.
 
Pia kuruhusu uwanja kutumiwa bila watazamaji kwa baadhi ya mechi, na kutoruhusu uwanja huo kutotumika kabisa kwa baadhi ya mechi.
 
Boniface Wambura Mgoyo
Media and Communications Officer
Tanzania Football Federation (TFF)

Soma Habari Kamili

TAARIFA KUHUSU KOCHA WA TAIFA STARS KUACHISHWA KAZI


Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Kocha wa Taifa Stars, Kim Poulsen wamekubaliana kuvunja mkataba katika makubaliano ambayo ni siri kwa pande zote mbili.

Uamuzi huo ulitangazwa jana (Februari 27 mwaka huu) jijini Dar es Salaam kwa pamoja na Rais wa TFF, Jamal Malinzi na Kocha Poulsen mbele ya waandishi wa habari.
 
Rais Malinzi kwa niaba ya TFF ametoa shukrani za dhati kwa Kocha Poulsen kwa ushirikiano na mchango ambao ameutoa kwa Tanzania kuanzia kwenye mpira wa miguu wa vijana.
 
Naye Kim amewashukuru Watanzania kwa ushirikiano waliompatia kwa kipindi cha miaka mitatu alichokaa nchini kuanzia Mei 2011 alipoteuliwa kuwa kocha wa timu za Taifa za vijana, na baadaye Taifa Stars.
 
Akizungumzia benchi jipya la ufundi la Taifa Stars, Rais Malinzi amesema linatarajiwa kutangazwa hivi karibuni likiongozwa na kocha kutoka nje ya Tanzania.
 
Amesema kwa upande wa mechi dhidi ya Namibia itakayochezwa Machi 5 mwaka huu jijini Windhoek, Stars itaongozwa na Kaimu Mkurugenzi wa Ufundi, Salum Madadi akisaidiwa na kocha Hafidh Badru kutoka Zanzibar.
 
Katika hatua nyingine, Kocha Madadi amewaondoa wachezaji watano wa Yanga katika kikosi kilichotajwa awali ili wapate fursa ya kuitumikia timu yao kwenye mechi mbili za Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al-Ahly ya Misri.
 
Wachezaji hao ni Athuman Idd, David Luhende, Deogratius Munishi, Frank Domayo, Kelvin Yondani na Mrisho Ngasa. Pia kipa Ivo Mapunda ameondolewa katika kikosi hicho baada ya kupata msiba.
 
Nafasi zao zimezibwa na wachezaji Abdi Banda (Coastal Union), Himid Mao (Azam), Juma Luizio (Mtibwa Sugar), Said Moradi (Azam) na Shabani Kado (Coastal Union).
 
Taifa Stars itaingia kambini kesho (Machi 1 mwaka huu) jioni kwenye hoteli ya Accomondia jijini Dar es Salaam, na itaondoka Machi 3 mwaka huu alfajiri kwa ndege ya South African Airways na kurejea nchini Machi 7 mwaka huu saa 8.15 mchana.

Soma Habari Kamili

WAYNE ROONEY ASAINI MKATABA WA KUICHEZEA MANCHESTER UNITED MPAKA 2019

Wapenzi wa Manchester united hii itakuwa habari ya nzuri kwao kwasababu mtu muhimu kwenye kikosi chao amesaini mkataba wa kuendelea kuichezea timu hiyo kwa muda mrefu zaidi.
Rooney amesaini mkataba wa kuendelea kuwa na club ya Manchester united kwa miaka 4 zaidi ambapo atakuwa hapo hadi 2019.
Picha kwenye instagram ya Man united ambayo inamuonyesha Rooney akisaini mkataba huo pembeni ya kocha wake imepewa caption hii “Great news for #mufc as Wayne Rooney signs a four-year contract extension keeping him at #mufc until June 2019. #rooneymufc”

Soma Habari Kamili

MATOKEO RAUNDI YA 3 KOMBE LA FA: LIVERPOOL, CHELSEA ZAPETA, MAN UTD HOI

Wilfried Bony wa Swansea baada ya kufunga bao la pili na la ushindi dhidi ya Manchester United.
Mchezaji wa Manchester United, Danny Welbeck, akiwa kichwa chini miguu juu wakati wa mtanange huo uliomalizika kwa Swansea kushinda 2-1.
Manchester United 1-2 Swansea City
Liverpool 2 - 0 Oldham Athletic
Derby County 0 - 2 Chelsea
Sunderland 3 - 1 Carlisle United
Nottingham Forest 5 - 0 West Ham United

Soma Habari Kamili

LEWANDOWSKI ASAINI MKATABA MPYA NA BUYERN MUNICH BUREE

Klabu ya Bayern Munich hatimaye imethibitisha kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Poland Robert Lewandowski . Lewandowski amesaini mkataba wa miaka mitano ambapo ataanza kuichezea Bayern Munich mwezi julai mwaka huu baada ya kuisha kwa msimu wa sasa wa ligi ya Ujerumani ambako atakuwa anamalizia mkataba wake na Borrusia Dortmund. Robert Lewandowski anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya na klabu ya Bayern Munich baada ya kusaini ikiwa ni taratibu za mwisho kabla ya kujiunga nayo rasmi.
Lewandowski yuko kwenye miezi sita ya mwisho ya mkataba wake na Dortmund hali inayomruhusu kuingia makubaliano ya awali na klabu nyingine na atajiunga na Bayern kuanzia msimu ujao ambapo anaondoka Dortmund bure.

Soma Habari Kamili

KOCHA ATUA YANGA AMFUTA KASEJA

Kipa ya Yanga, Juma Kaseja.

MABADILIKO yanaendelea kutokea ndani ya kikosi cha mabingwa wa soka Tanzania, Yanga kwani tayari imepata kocha mpya wa makipa ambaye hata kabla ya kuanza kazi, ametangaza kumfuta kipa Juma Kaseja kama kipa namba moja.
Kaseja alipewa nafasi hiyo katika mechi yake ya kwanza akiwa amerudi Yanga na kufungwa mabao matatu wakati Yanga ilipolala kwa mabao 3-1 dhidi ya Simba katika mechi ya Nani Mtani Jembe, Desemba 21, mwaka jana.
Juma Pondamali ambaye si mgeni kwa Kaseja ndiye kocha mpya wa makipa Yanga akichukua nafasi ya Mkenya Razack Siwa na amesisitiza: “Kwa sasa Yanga hakuna kipa namba moja.”
Kauli hii ya Pondamali maarufu kama Mensah inamaanisha Kaseja ambaye alilaumiwa kufungisha bao la tatu walipoivaa Simba, atalazimika kuwania namba dhidi ya Deougratius Munishi ‘Dida’ na Ally Mustapha ‘Barthez’.
Kipa huyo wa zamani wa Yanga na Taifa Stars, ameliambia gazeti hili kuwa kinachofuata kwake ni kazi tu na hatakuwa na utani hata chembe.
Kaseja alikuwa chaguo la kwanza katika kikosi cha Ernie Brandts na Siwa, halafu Deogratius Munishi ‘Dida’ akawa chaguo la pili huku Ally Mustapha ‘Barthez’ akiporomoka hadi chaguo la tatu ikiwa ni siku chache baada ya Kaseja kusajili Yanga.
“Kuanzia sasa hakuna kipa namba moja tena, nitawapa mazoezi ya uhakika mpaka wawe na viwango vya juu ninavyotaka. Makipa wote si wageni kwangu, nimewahi kuwafundisha katika timu ya taifa,” alisema Pondamali.
Akizungumzia juu ya ajira yake mpya klabuni hapo, Pondamali alisema: “Nimeshasaini mkataba wa miaka miwili Yanga na nimelipiwa kodi ya nyumba kwa mwaka mzima palepale nilipokuwa naishi Kigamboni (Dar es Salaam).
“Kuhusu usafiri, sijapewa gari binafsi ila nimekabidhiwa dereva ambaye atakuwa anatumia gari la klabu kwa ajili ya kuniendesha katika safari zangu za hapa na pale.
“Nashukuru Mungu mkataba wangu niliopewa hapa Yanga ni mzuri na kama ukizungumzia maslahi nadhani ni bora mara tano ya nilivyokuwa nalipwa Coastal Union na klabu nyingine zote nilizopita.”
Pondamali pamoja na Charles Boniface Mkwasa ambaye ni kocha msaidizi  mpya walitambulishwa jana katika kikao cha viongozi na wachezaji, ikiwa ni cha kwanza kukutana tangu kutangazwa kutimuliwa kwa Brandts na benchi la ufundi.
Mkwasa anakuwa kocha msaidizi huku Yanga ikiendeleza mchakato wa kumpata kocha mkuu na tayari zaidi ya makocha 40 wametuma maombi.
Aidha, Yanga imemrudisha daktari Juma Sufiani ambaye ilimuacha na nafasi yake kuchukuliwa na Nassor Matuzya ambaye pia ameachwa.

Soma Habari Kamili

KAWAMBWA CUP YAFIKA TAMATI

Meneja wa Masoko wa Kampuni ya Konyagi Joseph Chibehe (kulia) akimkabidhi nahodha wa timu ya Mwambao, Selemani Lugono baada ya timu yake kuibuka washindi wa pili katika Ligi ya Kawambwa Cup iliyomalizika mjini Bagamoyo mwishoni mwa wiki. Wanaoshuhudia kutoka kulia ni Mbunge wa Jimbo hilo, Dk. Shukuru Kawambwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa BMT, Iddi Kipingu.

Soma Habari Kamili

CHELSEA YAIPIGA LIVERPOOL 2-1

Wachezaji wa Chelsea wakishangilia bao lililofungwa na Samuel Eto'o dhidi ya Liverpool leo.
Chelsea imeibuka na ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Liverpool katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyopigwa Uwanja wa Stamford Bridge!

Soma Habari Kamili

ARSENAL YAFUNGA MWAKA 2013 KILELENI

Olivier Giroud akishangilia bao pekee aliloifungia Arsenal na kukwea kileleni.
Cheick Tiote wa Newcastle (kulia) akiwania mpira na Wilshere wa Arsenal.

Soma Habari Kamili

TASWIRA ZA MECHI YA NANI MTANI JEMBE

Mashabiki wa Yanga wakishangilia.

Soma Habari Kamili

MANJI AKUBALI KIPIGO CHA 3-1

Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji, akiongea na wanahabari (hawapo pichani).
MWENYEKITI wa Yanga, Yusuf Manji, amekubali kipigo cha 3-1 kutoka kwa Simba na kusema asitupiwe lawama mchezaji wala kiongozi yeyote kwa matokeo ya jana.

Soma Habari Kamili

MATOKEO: LIVERPOOL WASHIKA USUKANI

Wachezaji wa Liverpool wakimpongeza Luis Suarez (wa pili kulia) baada ya kuwafungia moja ya bao dhidi ya Cardiff leo

Soma Habari Kamili

NANI MTANI JEMBE?......MNYAMA SIMBA!

Haruna Shamte akiwa amenyanyua juu Kombe la Mtani Jembe alilokabidhiwa na Mgeni Rasmi, Waziri wa Sheria na Katiba, Mathias Chikawe (mwenye suti nyeusi kulia) baada ya kuwashushia kichapo cha mabao 3-1 Watani Wao, Yanga SC katika mechi ya Nani Mtani Jembe iliyopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar leo jioni.

Soma Habari Kamili

OKWI AAPA KUFANYA MAKUBWA YANGA.

Mshambuliaji mpya wa Yanga, Emmanuel Okwi kutoka Uganda ametua nchini kuja kuitumikia klabu hiyo na kusema ataichezea kwa mapenzi makubwa. Mchezaji huyo wa zamani wa Simba alitua jana saa 9:30 na kulakiwa na viongozi wa Yanga na mashabiki wachache wa klabu hiyo waliojitokeza kumpokea Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, Dar es Salaam.

Soma Habari Kamili

EMMANUEL OKWI ALIVYOTUA DAR KUJIUNGA NA YANGA LEO

Emmanuel Okwi akilakiwa na shabiki maarufu wa Yanga, Steven (kulia) katika uwanja wa ndege alipowasili.

Soma Habari Kamili

DROO YA PILI SHINDA MAHELA NA CHAMPIONI NI DESEMBA 23


Na Mwandishi Wetu DROO ya pili ya Shinda Mahela na Championi inatarajiwa kufanyika Desemba 23, mwaka huu kwa ajili ya kuwapa zawadi za Krisimasi washindi wake.

Soma Habari Kamili

KOMBE LA DUNIA: RAJA CASABLANCA YAIZAMISHA 3-1 ATLETICO MINEIRO NA KUTINGA FAINALI….WACHEZAJI WAGOMBEA VIATU VYA RONALDINHO!!

Souvenir: Raja Casablanca players crowd round Ronaldinho to get his boots
Balaa tupu!: Wachezaji wa Raja Casablanca wakiwa wamemzunguka Ronaldinho kutaka viatu vyake Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail BAADA ya kutolewa katika mchezo wa nusu fainali wa klabu Bingwa ya Dunia  ya FIFA, inawezekana  Ronaldinho alikuwa anataka kurejea kwenye chumba cha kubadilishia nguo cha klabu yake ya  Atletico Mineiro ili kujiliwaza kufuatia kula kipigo.

Soma Habari Kamili

ICHEKI RATIBA YA UEFA HAPA, MANCHESTER CITY NA ARSENAL WAINGIA CHA KIKE!

Soma Habari Kamili

Ungana Nasi, Like Page Yetu Hapa Chini