WEMA, MAMA YAKE KUSOMA ALBADILI

Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu.
SIKU chache zimekatika tangu kusambazwa kwa picha feki inayodaiwa ni ya mama wa Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu, Mariam Sepetu, wawili hao wako kwenye mkakati mzito wa kuwasomea kisomo cha Albadili wale wote waliohusika kwa namna yoyote ile kuitengeneza picha hiyo na kuitupia mitandaoni, Risasi Jumamosi linakumegea.
Picha hiyo iliyosambazwa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwa na kichwa cha mama Wema, lakini sehemu ya kuanzia shingoni kwenda chini si yeye na mhusika alikuwa hana nguo, ilizua gumzo kwa wiki mbili sasa huku watu wanaojiita Timu Dengue wakitajwa kuhusika.

KINYWANI MWA CHANZO CHA HABARI
Kwa mujibu wa chanzo chetu, mama Wema na mwanaye wameamua kusoma Albadili ili kuwaadabisha wale wote waliohusika na sakata hilo lenye kufedhehesha.
“Mama Wema na mwanaye walikasirishwa sana na watu waliotengeneza ile picha na kuitupia kwenye mitandao ya kijamii kama Instagram.
“Wiki iliyopita baadhi ya wasamaria wema walikwenda nyumbani kwa mama Wema na kumtajia majina ya wahusika, lakini hawakuwa na ushahidi hivyo yeye na Wema wameamua kujiunga kiimani zaidi kwa kusoma Albadili.
Wema Sepetu akiwa na mama yake, Mariam Sepetu.
“Wamesema kwanza kabla ya tukio hilo la Abdadili wametoa siku saba kwa yeyote anayejijua amehusika na picha zile za kutengeneza aende mwenyewe kwa mama Wema, nyumbani kwake, Sinza-Mori (Dar) ili kuomba msamaha.
“Kama zitapita siku saba na hakuna atakayejitokeza, Albadili itasomwa na mmoja baada ya mwingine watakufa. Tayari wameshawasiliana na mashehe ambao watasoma Albadili hiyo,” kilisema chanzo hicho.

WEMA AYEYUKA HEWANI
Baada ya kusikia kutoka kwa chanzo chetu cha uhakika, juzi Risasi Jumamosi lilimsaka Wema ili kumsikia anasemaje kuhusu kuwepo kwa madai hayo lakini muda mwingi wa maandalizi ya habari hii, simu yake haikuwa hewani!

MAMA WEMA SASA
Baada ya kumkosa Wema, Risasi Jumamosi lilimtafuta mama yake, naye kwa njia ya simu na alipopatikana aliombwa kutoa ufafanuzi juu ya madai hayo.
KUHUSU ALBADILIAkizungumza kwa hasira huku sauti yake ikionesha dalili kwamba bado hayuko sawa, mama Wema alisema:
“Ni kweli, nimeshapanga kufanya hivyo, nitasoma Albadili. Haiwezekani watu wakae na kuamua kunichafua mimi, nimewakosea nini cha mno mpaka kufikia kufanya vile! Siwezi kukubali hata kidogo.”

KUHUSU MASHEHE
“Ni kweli pia, nimeshawasiliana na mashehe. Wao wako tayari wanachosubiri ni kupita kwa siku ambazo nimetoa. Kama hakuna atakayejitokeza kuomba radhi, kisomo cha Albadili kitasomwa, wataanza kupukutika mmoja baada ya mwingine kweli nasema.”

SIKU SABA ZINAANZA LINI?
“Jumamosi ijayo (leo) itakuwa siku ya kwanza. Kwa hiyo mpaka Ijumaa ya Julai 11 (mwaka huu), itakuwa siku ya mwisho.”

NENO LAKE KWA WAHUSIKA
“Nawaambia wale wote wanaojijua walihusika na ile picha ya uongo, ya kutumbukiza kichwa changu kwenye picha nyingine na wale waliohusika kuitupia kwenye mitandao, waje waniombe radhi kabla siku saba hazijaisha, sitanii jamani.”

UKWELI WAKE
“Mimi ni Muislamu safi, nasema sijawahi kupiga picha za namna hiyo katika maisha yangu tangu nizaliwe mpaka utu uzima wangu huu na wala sijawahi kufikiria.”

KUMBUKUMBU YA WEMA
Katika Gazeti la Risasi Mchanganyiko, Toleo la Juni 25, mwaka huu, ukurasa wa mbele kulikuwa na habari yenye kichwa; Wema azimia!
Habari ile ilimhusu Wema kupoteza fahamu kufuatia kuiona picha hiyo kwenye mitandao akidai ililenga kumchafulia mama yake jina.

KILIO KWA TCRA
Kumekuwa na wimbi la watu  kuchafuana kwenye mitandao ya kijamii ambapo ukiacha watu maarufu kutengenezewa picha chafu, pia wanafunzi wa vyuo wamekuwa waathirika wakubwa.
Hata hivyo, baadhi ya wananchi waliowahi kuzungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti walitoa kilio chao kwa Wizara ya Sayansi na Teknolojia kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kudhibiti usambazwaji wa picha chafu mitandaoni.

Soma Habari Kamili
Blogger Tricks

LUCY KOMBA ATENGWA BONGO MOVIE


STAAwa sinema za Kibongo, Lucy Komba, amedaiwa kutengwa na wasanii wenzake wa Klabu ya Bongo Movie kwa kosa la kuwatolea lugha za kejeli.Staa wa sinema za Kibongo, Lucy Komba,
Chanzo makini kimepenyeza habari kuwa, Bongo Movie wamemsusia msanii huyo katika vikao vya harusi yake kwa madai kuwa aliwahi kuwaponda kwenye vyombo vya habari kuwa klabu hiyo si chochote kwake.
Alipotafutwa na paparazi wetu, Lucy ambaye anatarajia kufunga pingu za maisha Septemba, mwaka huu, alisema hakumbuki kama aliwahi kuwakejeli wasanii hao isipokuwa wengi wamekuwa wakimjadili kwa suala hilo na sasa hawahudhurii kwenye vikao vya harusi yake.
“Mimi hata sikumbuki kama niliwahi kuongea hayo kwenye vyombo vya habari na kama niliongea labda walinielewa tofauti na kauli niliyoitoa, sioni sababu ya kuwekeana bifu ila kwa anayetaka acha aendelee,” alisema Lucy.

Soma Habari Kamili

ODAMA AELEZA ALIVYO KUTANA NA MAREHEMU RECHO

MTOTO mzuri mwenye asili ya Kihaya, Jenifer Kyaka ‘Odama’ aliyesoma shule ya msingi mkoani Kigoma kisha kuhamia jijini Dar na kupitia kozi tofautitofauti kabla kutupa karata yake katika anga la filamu ndiyo tupo naye leo katika Exclusive Interview.
Mtoto mzuri mwenye asili ya Kihaya, Jenifer Kyaka ‘Odama’ akiwa na marehemu Recho Haule enzi za uhai wake.
Awali, hakuwahi kuwaza kama siku moja anaweza kuwa mwigizaji, lakini baadaye upepo ulibadilika na kujitengenezea jina la kazi, Odama. Kwenye makala haya amefunguka mambo mengi kuhusiana na safari yake ya uigizaji, twende pamoja:
Mwandishi: Wasomaji wetu wangependa kujua historia yako kifupi?
Odama: Nilianzia masomo yangu kule Kigoma baadaye nikahamia Shule ya Msingi Mburahati, sekondari nikamalizia Moshi mwaka 2000.

Mwandishi: Nini kilifuata baada ya kumaliza masomo yako ya sekondari?
Odama: Nilisoma kozi mbalimbali za kompyuta kisha ndipo nikajikuta nimekita nanga katika masuala ya filamu.

Mwandishi: Ulianzaje na nani ambaye alikuunganisha na fani hiyo?
Odama: Nilivutiwa na uigizaji ghafla, nikajiunga na Kikundi cha Kidedea, nikafanya mazoezi lakini bahati mbaya mmiliki wa kikundi hicho, Peace alifariki kikasambaratika hivyo nikawa nimepoteza uelekeo wa kisanaa.

Mwandishi: Ulifanya nini baada ya kundi hilo kufa?
Odama: Nilikaa kwa muda kisha baadaye nilikutana na ‘camera man’ mmoja anaitwa Musa Banzi ambaye alinikuta Holliday Inn, Posta nikiwa na rafiki yangu ndipo wakaniomba kushuti katika kipande cha wimbo wao baada ya mtu waliyekuwa wamempanga aje kuchelewa, baada ya kumudu uhusika vizuri katika video hiyo, kila mtu aliyekuwepo hotelini hapo aliguswa na mimi. Wakanishauri nijikite katika uigizaji.

Jenifer Kyaka ‘Odama’
Mwandishi: Wazazi wako walikupokeaje ulipoanza kujishughulisha na sanaa?
Odama: Nashukuru Mungu walinipokea vizuri, walinitia moyo na kuamini kwamba naweza kujiingizia kipato kupitia sanaa.

Mwandishi: Ugumu gani ulipitia kwenye sanaa?
Odama: Kujifua kwenye mazoezi pasipo kujulikana na watu kwa muda mrefu ndiyo changamoto kubwa niliyopitia. Kidogo nilianza kuona mwanga wa mafanikio nilipokutana na wasanii wenzangu kina Riyama, Shumileta na wengineo katika Kundi la White Elephant ambalo lilikuwa chini ya Banzi.

Mwandishi: Katika upande wa filamu, muvi gani ilikuwa ya kwanza wewe kuigiza?Odama: Sikuwa muhusika mkuu katika muvi ya kwanza kuigiza lakini ilikuwa ni Shumileta ambayo ilimpa jina mwenzangu Jenifer Mwaipaja, kila mtu akamtambua kwa jina la Shumileta.
Mwandishi: Kwa nini majina ya umaarufu zamani yalikuwa yanazalishwa na jina la filamu?
Odama: Basi tu ilikuwa inatokea hivyo, mashabiki walikuwa wakipenda kutumia jina la filamu hususan ile ambayo umecheza vizuri na kukubalika ndiyo maana hata mimi jina langu lilizaliwa mwaka 2005 nilipocheza filamu ya Odama.

Mwandishi: Ulianza lini  kujitegemea mwenyewe rasmi na kusimama katika soko la filamu?
Odama: Ilikuwa ni mwaka 2009 baada ya kufanikiwa kuanzisha kampuni yangu ya filamu, J Film 4 Life.
Mwandishi: Ulipata wapi mtaji wa kuanzisha kampuni?

Odama: Nilikuwa nafanya biashara zangu tu ambazo zilinipa mtaji wa kwenda kununua vifaa vyangu na kufungua ofisi.
Mwandishi :Inasemekana mapedeshee ndiyo ambao walikupa mtaji wa kufungua kampuni ya filamu, ni kweli?
Odama: Sijawahi kupewa mtaji na pedeshee, sina pedeshee aliyeniwezesha na wala sitakuja kuwa naye.
Mwandishi: Mlikutana wapi na marehemu Recho (Sheila Haule).
Odama: Recho nilikutana naye kipindi f’lani nilipokuwa nikifanya kazi na Bajomba (prodyuza) ambapo nilikutana na Lamata (muongozaji), tukakutana na Recho na kuanza kufanya naye kazi.

Mwandishi: Unakumbuka muvi ya kwanza kucheza na marehemu Recho?
Odama: Nakumbuka, ilikuwa ni muvi iliyofahamika kwa jina la Candy.
Mwandishi: Hebu tuambie mlikutana wapi na boifrendi wako wa kwanza?
Odama: Heeee! Swali gumu…anyway ni hivi….

Usikose wiki ijayo ili kujua Odama alikutana wapi na ‘boyfriend’ wake wa kwanza.

Soma Habari Kamili

MADAI YA KUCHEPUKA KAJALA ACHARUKA

Mwigizaji wa Bongo movie Kajala Masanja
BAADA ya kuzagaa kwa taarifa mbalimbali kwamba mwigizaji wa Bongo, Kajala Masanja anachepuka nje, ameibuka na kukanusha madai hayo akisema hayana ukweli wowote.
Mitandao mbalimbali ya kijamii imekuwa ikiposti taarifa mbalimbali zinazomhusisha Kajala kutembea na wanaume tofauti kitu ambacho mwenyewe amesema hakina ukweli na wanaosambaza uvumi huo, wakome.
Akizungumza na mwanahabari wetu Julai 3, mwaka huu alisema wanaoeneza habari za yeye anachepuka wanamtafuta ubaya kwani hana mpango wowote wa kuolewa wala kuishi na mwanaume kwa sasa.
“Waniache, mtu akisema nina mwanaume alishawahi kuniona? Sina mwanaume mwingine zaidi ya mume wangu,” alisema Kajala.

Kwenye mahojiano hayo, Kajala alisisitiza kuwa, haoni sababu ya yeye kuchepuka wakati mumewe Faraja Augustino yupo hai na anaamini ipo siku atatoka gerezani na ataendelea na maisha ya ndoa yake kama ilivyokuwa zamani.
Kajala Masanja akiwa kwenye pozi
“Kiukweli sioni haja ya kuolewa na mwanaume mwingine tena wakati ni wazi ipo siku mume wangu atakuwa huru, naomba ieleweke kwamba sina mpango na mwanaume yeyote na sasa namgonjea atoke tuendelee na maisha yetu,” alisema Kajala.
Mume wa Kajala, Faraja Agustino anatumikia kifungo cha miaka 7 baada ya kushindwa kulipa faini ya shilingi milioni 200 kufuatia kesi ya kutakatisha fedha iliyokuwa ikimkabili.
Kwenye kesi hiyo, Kajala ambaye naye alihusishwa, alilipiwa faini ya shilingi milioni 13 na mwigizaji Wema Sepetu, kifungo cha miaka mitano kikamuepuka.

Soma Habari Kamili

DUDUBAYA ASAKWA NA JESHI LA POLISI

MKONGWE wa Bongo Fleva, Godfrey Tumaini ‘Dudubaya’ anasakwa na polisi kwa RB namba OB/RB/11650/2014 KUTISHIA KUUA mganga wa jadi Mery Kapalisya ambaye inadaiwa alikuwa akiishi naye kama mkewe.
Mkongwe wa Bongo Fleva, Godfrey Tumaini ‘Dudubaya'.
Akisimulia mkasa mzima, Mery alisema Dudubaya alitishia kumuua mara baada ya kumfukuza katika nyumba waliyokuwa wakiishi pamoja maeneo ya Tandale, jijini Dar.
“Mimi na Dudu (Dudubaya) tulikutana baada ya kukutanishwa na Mabovu (msanii) ndipo tukaanzisha uhusiano wa kimapenzi baada ya kuniomba niwe naye na kunieleza matatizo yake.
“Kwa sababu nilimpenda niliamua kumkubalia na kuanza naye maisha ambapo tulikuwa tukilala katika baa yangu  nyumbani kwa akina Mabovu.
“Tukiwa ndani ya uhusiano, Dudubaya  alianza kunibembeleza kwamba baa ile tuipe jina la Mamba ikiwa ni chata yake, kwa sababu nilimpenda niliamua kumkubalia lakini nilimwambia aongeze herufi nyingine mbili ambazo zitamaanisha na mimi nahusika, tukakubaliana,” alisema Mery na kuongeza:
Mganga wa jadi Mery Kapalisya ambaye amedaiwa kuishi na 'Dudubaya' kama mke wake.
“Baada ya baa kubadilishwa jina, matatizo yakaanza taratibu kwani walijaa wasanii wa kila aina, baa ikaanza kuwa na sifa mbaya mpaka wateja wote wakaondoka wale waliokuwa wanajiheshimu.”
Mery alisema alikuwa akimuonya Dudubaya juu ya tabia za kumsaliti na kulala na wanawake ndani ya nyumba pale anapokuwa amesafiri kwenda kwenye mambo ya kitabibu lakini alikuwa hasikii.
“Baada ya kunifukuza nyumbani, amenitumia maneno mazito sana ambayo siwezi kusimulia kiukweli lakini ninao ushahidi wa SMS,” alisema Mery alipokuwa katika Kituo cha Polisi Oysterbay.
Wakati Mery alipokuwa kituoni hapo, polisi walimpigia simu Dudubaya, akasikiliza maelezo ya polisi kisha akakata simu na alipopigiwa tena, hakupokea.

Soma Habari Kamili

LULU MICHAEL AANIKA PAJA NJE KUWATEGA WANAUME



GAUNI alilovaa msanii wa filamu Bongo, Elizabeth Michael hivi karibuni alipokuwa kwenye hafla ya utoaji wa Tuzo za Watu limeonesha kuwatega wanaume hasa wakware kufuatia kuuanika ‘upaja’ wake.
 
Akiwa ndani ya Ukumbi uliopo ndani ya Hoteli ya Serena, Posta jijini Dar, Lulu alionekana amevalia gauni refu lakini pembeni likiwa na mpasuo mkubwa ambapo kila alipokaa, mapaja yake yalionekana wazi hivyo kumfanya ahangaike kuyaficha huku wanaume nao wakitumia muda mwingi kumkodolea macho kisha kunong’ona.
 
“Duh!Haka kabinti kazuri na lile gauni alilovaa ndiyo anawaacha hoi sana wanaume,ile ni kututafuta ubaya na kama ni kututega kafanikiwa kwa silimia 100,” alisikika kijana mmoja akisema.
 
Mwandishi wetu alifanya jitihada za kutaka kuongea na Lulu juu ya mpasuo huo, lakini hakuwa tayari na hata baada ya zoezi la utoaji wa tuzo, aliondoka fasta akiwa na wapambe wake.

Soma Habari Kamili

JOKATE MWEGELO APANGUA TUHUMA ZA KUVUNJA NDOA YA DIDA



Mtangazaji wa Kipindi cha The One Show, Jokate Mwegelo ‘Jojo’ amefunguka kuwa hahusiki na kuvunjika kwa ndoa ya Khadija Shaibu ‘Dida’ kwani ni mshikaji wake na wanaheshimiana.
 
Akijibu tuhuma kuwa, yeye anahusika na kuparaganyika kwa ndoa hiyo kufuatia ‘ku-fall in love’ kwa mume wa Dida, Edzen Jumanne ambaye ni mtangazaji mwenzake, Jokate alisema:
 
“Yaani watu wanapenda kuungaunga maneno kweli, jamani mimi siwezi hata siku moja kuwa na Edzen, ni mfanyakazi mwenzangu halafu Dida ni mshikaji wangu siwezi kabisa, tena wasitake kunitibulia.”

Soma Habari Kamili

PICHA YA DIAMOND AKIWA NA MBWA YAZUA KASHESHE


Diamond Platinumz ambaye jina lake halisi la dini ya kiislamu ni Naseeb Abdul ameshambuliwa Instagram na baadhi ya mashabiki baada ya kupost picha akiwa beach huko ughaibuni huku ameshikilia kamba iliyomfunga mbwa.
 
Mashabiki wengi walimshambulia wakielekeza point yake kwenye suala la imani ya dini ya kiislamu huku wakiunganisha tukio hilo na mwezi mtukufu wa Ramadhani.
 
Rashyalhambeshy: ramadhan acha kupost pc zisizo eleweka ww umaaruf ww una umaaruf km mtume muhammad s.w.a na yote kakataza acha mambo yk ayo jua kuna kufa muangalie firauna laanatullah ila me lng jicho. na ktk dini tumeambiwa tukumbushaneni me nimekemea kwa mdomo ok.
 
Hata hivyo sio wote waliomshambulia, wapo wengi pia waliomtetea kwa points tofauti kama Leanlilie aliyetumia point hiyo hiyo ya imani.
 
leanlilie :I jus keep wondering who a u to judge another person?kumhukumu mwenzio tuu ni dhambi wew je ni mwema sana?huu ni wakati wa toba jisalie na uombee makosa yako,mwachie Allah ndio mtoa hukumu we Tanzanians tumezidi jaman khaaaaa!!can we atleast think abt our sins and pray acheni watu ma maisha yao.!
 
Nimejaribu kuwauliza watu wawili watatu ambao wamejikita katika masuala ya dini ya kiislamu kuhusu picha hiyo na imani ya dini hiyo, lakini wao wamenieleza kuwa sio kosa kumgusa mbwa bali ni haramu mbwa kumnusa muumini wa dini ya kiislamu.

Soma Habari Kamili

LOVENESS DIVA AACHIA PICHA ZA UCHI



Mtangazaji  maarufu  wa  Clouds  Fm  Loveness  Diva  ameposti  picha  katika  account  yake  ya  Instagram  akiwa  ameuanika  mwili  wake  wote  kwa  jamii....

Mtangazaji  huyo  ameamua  kujidhalilisha  tena  bila  kujali  nafasi  yake  ya  kazi  kwa  kile  kinachoelezwa  kuwa  ni  kutafuta  kick....

Mashibiki  wengi   hasa  Followers  wake  wamemuelezea  mtangazaji   huyo    kama  mtu  anayetaka  kurukwa  na  akili.....
 

Soma Habari Kamili

AINA TATU ZA MICHEPUKO HAPA BONGO

1. Mchepuko wa Lami: huu ni ule ambao hauombi pesa, upo njema unajua designer zote, katulia hana mapepe, uwe nae usiwe nae maisha yake yanaendelea.

2. Mchepuko wa Vumbi: huu ni ule ooh sina pesa, naomba vocha, sijui simu imekufa, charge iko low, ooh nipo saloon nadaiwa elfu thelathini nitumie kwa tigopesa, naomba nauli, nadaiwa kodi, mtoto wa shangazi kaja, nrushie  dompo, nk. Na hii ndio noma maana njia kuu lazima washtukie mchepuko vumbi unachafua na unasumbua fulltime!

3. Mchepuko kokoto: huu ni mkali zaidi ya njia kuu kila mara huuliza upo wapi? na nani?
Why hupokei simu yangu? Nomaaaa!

Baki njia Kuu!

Soma Habari Kamili

Ungana Nasi, Like Page Yetu Hapa Chini