Showing posts with label SKENDO. Show all posts
Showing posts with label SKENDO. Show all posts

LUNDENGA AKIRI KUWEPO WASICHANA WANAOTOA RUSHWA YA NGONO KUPATA TAJI LA MISS TANZANIA


Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino International Agency, ambao ni waandaji wa Miss Tanzania, Hashim Lundenga amedai kuwa wasichana wengi wanaoingia kwenye mashindano ya Miss Tanzania hufanya mbinu za kuwalaghai baadhi ya watu kwenye kamati kwa kuwapa rushwa ya ngono ili washinde taji la miss Tanzania.

Akizungumza na Global TV, Lundenga amedai kuwa kuna wasichana wanaoingia kwenye mashindano hayo wakiwa tayari kwa kila kitu.
 
“Kikumbwa ninachokwambia kuna wasichana ndani ya wasichana,kuna wasichana mule ambao katika mashindano yanayokuja they are ready for every thing,wapo wasichana hao na sisi tunajua hivyo,wasichana wanakuja pale wameshajua mimi nimegombana na boyfriend wangu nimemuacha boyfriend wangu kanikataza,mama yangu, baba yangu nimekuja kwajili hiyo, nilazima nishinde, sasa anashindaje? 

"Lazima apitepite kwa viongozi sisi,wanapitapita sana,wanajilegeza sana kwetu sisi,sasa sisi kama hatuna ethics ndiyo tunaingia kwenye mtego mbaya,kwasababu kuna mtu kwenye kamati yetu tumeshamsuspend mara mbili,tunamsuspend kwasababu ya upumbavu wake, mara mbili tumeshamsimamisha kwasababu ya upumbavu wake,” alisema.
 
Kuhusu tuhuma za kuwauza warembo watu wenye pesa, Lundenga alisema: 

"Unajua hapa mjini, mimi leo siwezi kusema Musofe simjui,siwezi sema mapedejee gani simjui, najuananao ndio watu wa mjini hao,tunakula nao tunalala nao, si ndio! Sasa huwezi sema completely ukaknock-out, haiwezekani,no it’s very difficult, akina nani wote wa Musoma yule,akina nani, huwezi, hao ndio mapedejee wa mjini.”

Soma Habari Kamili

MKE NA MUME WATEKWA KWA PAMOJA

Mariam Kimaya anayedaiwa kutekwa.
KIJANA aliyetambulika kwa jina la Dickson Mathias (35), na msichana aliyejulikana kwa jina la Mariam Kimaya wanadaiwa kutekwa kwa nyakati tofauti baada ya kufunga ndoa ya siri katika Kanisa la KKT, Tegeta jijini Dar, Mei Mosi, 2012, Risasi Mchanganyiko linakupa zaidi.
Akizungumza na gazeti hili kwa majonzi makubwa, dada wa Dickson, Aneth Mbaga alisema tukio hilo lilitokea baada ya Dickson kufunga ndoa hiyo na Mariam bila idhini ya wazazi wake kwenye kanisa hilo.
“Baada ya habari za kufunga ndoa ya siri kanisani kuwafikia baadhi ya ndugu wa Mariam, Dickson alianza kupokea simu za vitisho wakimuuliza ni kwa nini alifunga ndoa ya siri na binti yao wao wakiwa hawajui?
“Agosti 10, mwaka jana, nikapata taarifa kwamba Dickson alitekwa maeneo ya Mbezi ya Jogoo (Dar) na watu wasiojulikana.

Dickson Mathias anayedaiwa kutekwa pamoja na mkewe.
Walimweleza sababu za kumteka ambazo mimi sizijui,” alisema Aneth.
Aneth alizidi kuongeza kuwa miezi minne mbele, alipata taarifa kuwa,  mkewe Mariam naye alitekwa na watu wasiofahamika, hadi sasa hajulikani alipo kama vile mumewe.

“Yeyote mwenye taarifa sahihi naomba aripoti kituo chochote cha polisi kilicho jirani yake maana ndugu tuna wasiwasi mkubwa, hata kwa ndugu wa mwanamke nako hakuna anayejua waliko wawili hao,” alisema dada huyo huku akimwaga machozi.
Taarifa za kutekwa kwa Dickson ziliripotiwa katika Kituo cha Polisi Tabata na kuandikiwa jalada: TBT/RB/1988/2013 na polisi bado wanawasaka wanandoa hao.

Soma Habari Kamili

MWANAFUNZI AFIA KWA MPENZI WAKE

Mwili wa Atu ukiwa chumbani kwa mtu anayesadikika kuwa ni mpenzi wake, Hafidh Mohammed.
MSICHANA Atu Gabriel mwenye umri wa miaka 20,  mwanafunzi wa Chuo cha Eden Hill kilichopo Kwamfipa wilayani Kibaha mkoani Pwani, amekutwa amekufa chumbani kwa mtu anayetajwa kuwa ni hawara yake, Hafidh Mohammed.
Tukio hilo lilitokea April 26, mwaka huu na kukusanya umati huku mwanaume aliyelala na binti huyo akitokomea kusikojulikana.Marehemu anadaiwa kuwa mwenyeji wa Makambako mkoani Njombe.
Akizungumza na waandishi wetu juzi Kibaha, mama wa Hafidh ambaye pia ni mjumbe wa eneo hilo, Zainabu Saidi alisema mwanaye alimweleza kutokea kwa tukio hilo asubuhi kulipokucha na kabla ya hapo, hakuwa akifahamu kama alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na msichana huyo kwa vile aliyekuwa akimfahamu ni mwanamke mwingine ambaye alizaa naye.
“Mimi kwa kweli sikuwa na taarifa yoyote juu ya uhusiano wao na huyu  mwanafunzi, nimeletewa taarifa asubuhi na kijana wangu huku akionekana kuchanganyikiwa, nimejaribu kumsihi asikimbie lakini imeshindikana,” alisema mama huyo.
Mwili wa Atu ukiingizwa kwenye gari la polisi.
ALIVYOAGA CHUONI
Wanafunzi wa chuo hicho kinachofundisha masomo ya biashara na habari ambao walikataa kutaja majina yao waliliambia gazeti hili kuwa, marehemu Atu aliwaaga anakwenda jijini Dar es Salaam kumuuguza wifi yake aliyelazwa katika Hospitali ya Amana, Aprili 23, mwaka huu.

Hata hivyo, walisema uondokaji wake uliwapa maswali mengi kwani tofauti na walivyotegemea kuwa angebeba mfuko mkubwa wenye nguo za kubadili, yeye aliondoka akiwa na mkoba wake wa mkononi pekee hali iliyoonesha hakuwa akienda mbali.
Walisema siku tatu baadaye walipatwa na mshtuko mkubwa baada ya mlinzi wa hosteli yao kuwaletea taarifa za kifo cha mwenzao kilichotokea katika chumba cha mvulana huyo anayeishi jirani.

MAJIRANI NAO WANENA
Majirani waliozungumza na gazeti hili walisema kwao haikuwa mara ya kwanza kumuona msichana huyo, kwani mara kwa mara alikuwa akifika pale ingawa akishaingia ndani hakuwa akitoka nje.

Walisema mara zote hizo, mwanaume huyo mwenyeji ndiye alikuwa akitoka nje na kwenda kumnunulia chakula.
Wananchi na wanausalama wakiwa eneo la tukio.
POLISI WAUPELEKA MWILI HOSPITALI YA TUMBI
Jeshi la polisi liliwasili eneo la tukio na kuukuta mwili huo ukiwa umelala kitandani ukiwa hauna jeraha, lakini pembeni yake kulikutwa vidonge ambavyo havikufahamika ni vya aina gani ambavyo pia vilichukuliwa pamoja na mkoba wake hadi kituonis.

Minong’ono kutoka kwa majirani kuhusiana na vidonge hivyo ilitofautiana,  baadhi yao walisema huenda vilitumika katika jaribio la kutoa mimba, wengine walisema inawezekana msichana huyo alipata ugonjwa wa ghafla usiku na mwanaume huyo alikwenda kumchukulia vidonge hivyo ambavyo havikuweza kumsaidia marehemu kupata nafuu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani,  SACP Ulrrich Matei alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema juhudi za kumtafuta mwanaume huyo zinaendelea huku madaktari nao wakiendelea na uchunguzi wao ili kubaini chanzo cha kifo hicho.

Soma Habari Kamili

WABONGO WASUSIA KESI YA JACK CLIFF, .ATOKWA NA MACHOZI KORTINI NCHINI CHINA!


HATIMAYE modo maarufu Bongo, Jacqueline Fitzpatrick ‘Jack Patrick’ amepandishwa kortini kwa mara ya kwanza huko Macau nchini China, Aprili 10, mwaka huu kwa kukutwa na madawa ya kulevya tumboni aina ya heroin kete 57 au kilo 1.1 yakiwa na thamani ya zaidi ya shilingi milioni 223 huku ishu kubwa kwa muda wote aliokuwa mahakamani ikiwa ni kuangua kilio kila wakati. 

Jack alipandishwa kwenye korti hiyo ikiwa ni mara yake ya kwanza tangu alipokamatwa na madawa ya kulevya ‘unga’ Desemba mwaka jana akitokea Bongo kupitia Thailand na kuingia nchini humo.
ILIKUWAJE?
Kwa mujibu wa chanzo chetu makini kilichopo Macau, Jack alifikia hatua hiyo dakika 15 baada ya kupanda kizimbani na kukutana na nyuso za Wachina tu zikimwangilia

“Yeye alijua angekuta Wabongo au hata watu weusi wakimpa kampani, lakini matokeo yake alikutana na sura za Wachina tu,” kilisema  chanzo chetu.
Kikaendelea: “Unajua kwa kawaida mtu anapopanda kizimbani mara zote anafarijika sana endapo atawaona anaowafahamu, hasa ndugu zake ambao watafika kumtia moyo, sasa yeye hakulipata hilo.”
DAKIKA 10 ZATUMIKA KUMSOMEA MASHITAKA
Kuna madai kwamba, msoma mashitaka wa mahakama hiyo alitumia dakika 10 kutokana na taratibu za kisheria za huko huku akitakiwa kusema ndiyo au hapana tu kabla keshi hiyo kupigwa kalenda hadi Mei 23, mwaka huu

KUNA MADAI ALIZOMEWA
Chanzo hicho kiliendelea kudai kwamba, mbali na kukutana na upweke huo mahakamani, pia Jack alipata kisanga kingine pale baadhi ya raia wa nchi hiyo walipomzomea kwa sauti ya chini wakati akitoka kortini.
Inadaiwa kuwa, kwa Wachina kumzomea au kumsema vibaya mtu aliyedakwa na madawa ya kulevya ni kawaida kwani hakuna biashara, inapigwa vita nchini humo kama ya unga wakiamini unaangamiza nguvu kazi ya kizazi kijacho.
NDUGU WADAIWA KUMKATIA MAWASILIANO
Habari nyingine kutoka chanzo chetu zilidai kwamba, kwa sasa Jack amebaki yeye na Mungu wake baada ya nduguze waishio Bongo kumkatia mawasiliano kwa kile walichodai kuwa kitendo alichokifanya kimeiaibisha familia nzima.
“Unajua ndugu zake walikata mawasiliano kabisa? Nchi nzima au tuseme dunia nzima kilio ni jinsi vijana wanavyoharibika kwa madawa ya kulevya, sasa kule kubainika kwamba Jack alibeba unga tumboni kwenda kuuza kumeifanya familia kujisikia vibaya sana,” kiliongeza chanzo hicho kikiomba chondechonde kisitajwe gazetini.

KAMA ATARUDI BONGO SALAMA
Habari zaidi zinadai kwamba modo huyo ambaye pia ni Miss Ilala No 3, 2005, aliwahi kumwambia mshirika wake mmoja akiwa mahabusu kwamba, kama atabahatika kurejea Bongo salama,
atakwenda kupiga dua juu ya kaburi la mama yake ili amsimamie katika kumwondolea nuksi kama siyo mabalaa. Baba wa Jack anadaiwa kuishi nje ya nchi.
TUJIKUMBUSHE
Jack alikamatwa Desemba 19, mwaka jana kwenye Uwanja wa Ndege wa Macau nchini China akitokea jijini Bangkok nchini Thailand kuelekea Guangzhou, Mji Mkuu wa Jimbo la Guangdong Kusini mwa China ambako ilidaiwa ndiko alikokuwa anafikisha unga huo.
Ilidaiwa kuwa miongoni mwa mambo yaliyochangia kukamatwa kwake ni kuonesha uso wenye uchovu, kuanza kuwa na hali mbaya ya mwili, kushindwa kujibu maswali vizuri na hati yake ya kusafiria, yaani ‘passport’ kukutwa imegongwa mihuri ya kuingia nchini humo kila mara jambo ambalo wakaguzi waliliona si la kawaida kwa msichana kama yeye.
GPL

Soma Habari Kamili

MISS TANZANIA WALIOJITANGAZA HADHARANI KUWA WANA GONJWA HATARI



Miss Tanzania wawili, Happiness Millen Magese (2001) na Angela Damas (2002), wamejitokeza na kujitangaza wazi kuwa ni miongoni mwa mamilioni ya wanawake duniani wanaosumbuliwa na tatizo liitwalo ‘endometriosis’ ambalo huwafanya wapate maumivu makali wakati wa hedhi na pia kuwafanya wasiwe na uwezo wa kushika mimba. Tatizo hilo husababisha seli hai zinazounda mji wa mimba kukuwa/kuota nje ya mji wa mimba. “To all the ladies who have to live with the sufferings of endometriosis- May sharing our messages make us realize we are not alone, and may the sharing allow us to look for ways to help us live with less pain,” ameandika Angela Damas.
Ujumbe huo umemvutia, Happiness Magese ambaye naye aliamua kujitangaza wazi kuwa na tatizo hilo na kuanzisha kampeni ya ‘endometriosisafrica’.
“Praying for more women to speak out and share their stories .Wow this made my day ….thank you my darling Angela(Miss Tz 2002) for sharing your story .I feel better that we all finally speak out . Insta fam Angela Damas was actually the next queen after me in Wow this made my day ….thank you my darling Angela(Miss Tz 2002) for sharing your story .I feel better that we all finally speak out . Hi sisters Angela Damas was actually the next queen after me in Tanzania . How would Could one tell this amazing ,smart n beautiful person has this battle # endo power #we can do this together emojiemojiemoji @skinkissedbird we can save one’s happiness n pains. Let’s speak out cc @ladivamillen Tanzania.”



Millen anasema ameshafanyiwa upasuaji mara 12 hadi sasa Wakati wa kutangaza kuwa na tatizo hilo, March 16 mwaka huu, Millen aliandika kwenye Instagram:
It took me 17 years of struggle ,12 surgeries ,blocked Fallopian tubes ,1digestive system surgery,1ovary failure ,1miscarriage and still in pains I don’t know when it will stop.For the help of @ritadominic awareness and padma Lakshimi my friends @funminewyork @byanakusophy @adhiamboml n my family . I’m able to come out today and say this “I wear Yellow for me and all women from all over the world who struggling with Endometriosis . It’s ok to talk about our menstrual pains . You’re all warriors #speak about it #Dont ask for sympathy ,ask for help before it’s too late #March 2014 millions women walk for endometriosis #Dont loose hope. By rising this awareness we could help the cause to be able to give us free or reasonable price which can help all women to afford the treatment.#teamendometriosisafrica#Tanzania.

Soma Habari Kamili

KIGOGO AMHONGA KAJALA MILLIONI 10

Siri zimezidi kuvuja juu ya uhasama baina ya mastaa wawili wa kike bongo. Miss tanzania 2006. Wema sepetu na kajala masanja. Ambapo inaelezwa kuwa kiasi cha pesa sh.mil 13. Ambazo wema alimlipia kajala kumuokoa na hukumu ya kwenda jela katika mahakama ya hakimu mkazi kisutu dar hazikuwa zake.

kwa mujibu wa watu wa karibu na mastar hao Wema hakuwa na jeuri ya kutoa fedha hizo ndio maana familia ya mrembo huyo ilionyesha mshtuko mkubwa kwa binti yao kutoa pesa za bure kwa mtu baki kama kajala.
Habari zaidi zimesema kwamba kabla wema hajatoa pesa hizo alimpigia simu mfadhili huyo na kumueleza kilichokuwa kinaendelea mahakamani hapo ambapo aliruhusu pesa kutolewa.

kama pesa hiyo ingetoka mfukoni mwa wema basi familia yake akiwemo mamake asingeweza kumwacha bila kumuhoji bint yake.lakini mama wema alieleweshwa hali ilivyo na ndio maana akatulia.pesa ilitolewa na kigogo huyo ambaye sasa anatoka na kajala.
Aidha mtoa habari huyo alidai kwamba kabla ya wema kumsaidia Kajala mil.13 hakuwahi kutoa msaada wowote wa kifedha zaidi ya kula ubwabwa na watoto yatima.

Sani iliwahi kumpa taarifa wema kwamba kulikuwa na mama anayehitaji msaada wa laki moja kutokana na matatizo aliyokuwa nayo alijibu kwamba yeye sio serikali na kumsaidia Kajala kusiwafanye watu wamuone kama taasisi ya kutoa misaada.

Taarifa zaidi zimedai kwamba kutokana na tabia za mastaa zilivyo isingekuwa rahisi kwa Wema kutoa hata senti tano yake!
Naamini kwa hali ya mastaa ilivyo Wema kama wema asingeweza kutoa hata sh. Mia ili kumtoa kajala.Nyuma ya kesi ya kajala kulikuwa na huyo kigogo ambaye hivi sasa pesa zake zote anammwagia kajala.mambo yamegeuka ndivyo sivyo!” alisema.

Vyanzo vyetu hivyo vilitoa mfano wa msanii mwingine jack wolper ambaye alimpa msaada wa mil.10 aliyekuwa nyota wa filam Juma kilowoko au Sajuki kwa ajili ya matibabu na kudai hazikuwa zake , Wolper hakuwa na uwezo huo pesa zilikuwa za Dallas ambaye alimtumia Wolper kama kama bahsha kuufikisha mchango wake. Kiliongea chanzo hicho.
Mwandishi ni Christopher Lissa.

credit : swahilit1Q

Soma Habari Kamili

Ungana Nasi, Like Page Yetu Hapa Chini