Showing posts with label MAPENZI. Show all posts
Showing posts with label MAPENZI. Show all posts

WEMA SEPETU NA DIAMOND WANASWA WAKINYONYANA DENDA HADHARANI

Nasibu Abdul ‘Diamond’, na Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu wakiwa kwenye pozi la mahaba
MASUPASTAA ambao ni wachumba (wanasema wenyewe), Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu na Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, walijikuta wakionesha upendo wao mbele za watu kwa kudendeka  barabarani, Amani lilishuhudia.
Ishu hiyo ambayo wapendanao wengi huifanya kwa faragha, ilijiri hivi karibuni maeneo ya Bamaga- Mwenge jijini Dar es Salaam ambapo ni hatua chache kutoka kwenye Ofisi za Global Publishers ambao ni wachapishaji wa Magazeti Pendwa ya Amani, Risasi, Uwazi, Ijumaa, Championi na Ijumaa Wikienda.

ILIVYOKUWA
Kwa mujibu wa watu walioshuhudia tukio hilo, Wema alikuwa kwenye shughuli zake za kila siku maeneo hayo ambapo alikuwa ameegesha pembeni gari lake la rangi ya pinki aina ya Toyota Lexus Harrier bila kujulikana alikokuwa ameelekea.

Wakionyeshana upendo hadharani
DIAMOND AIBUKA PEKE YAKE
Ikadaiwa kuwa, mara Diamond naye alitokea bila kujulikana alikotokea akiwa anaendesha gari lake aina ya Toyota Prado na kuegesha gari lake jirani na alipoegesha Wema.


SIMU YAPIGWA CHUMBA CHA HABARI GLOBAL
Mapaparazi wa Global wakiwa katika kazi za kila siku ndani ya ofisi, simu ilipigwa kwa mmoja wao na kutonywa kuhusu wawili hao kuwepo eneo hilo kimahabamahaba.

“Jamani Global hapa jirani na ofisi zenu Diamond amekuja sasa hivi, lakini inaonekana amemfuata Wema maana Wema alishakuwepo muda mrefu uliopita, njooni mchukue picha si ndiyo zenu au bado mna bifu na Wema tangu siku ile alipokuja kuwafanyia fujo?”

PAPARAZI AWAFIKIA
Haraka sana paparazi mmoja alibeba kamera yenye uwezo wa kupiga picha kwa umbali wa mita hata 250 bila mhusika kushtukia na kutoka nayo.

Kweli, lilikuwa tukio lilionesha kushangaza kwani paparazi alikuta wapita njia wakiwa wanapunguza mwendo ili kuwashuhudia wawili hao walichokuwa wakikusudia kukifanya bila kuogopa watu.
WEMA NJE, DIAMOND NDANI
Kamera ya paparazi wetu iliweza kuwanasa wawili hao, Wema yeye alisimama nje ya gari la Diamond upande wa dirisha la dereva na kuongea na mwandani wake huyo jambo ambalo hakuna mpita njia aliyeonekana kushangaa.
Hata hivyo, mshangao ulianza pale Diamond alipotoa mkono nje na kumshika kiuno Wema huku wakiendelea kuongea ndipo baadhi ya wapita njia nao walipokoleza macho kodo, wengine wakihoji kama aliyesimama nje ya gari ni Wema, nani alikuwa ndani ya gari hilo!

Haikuwa rahisi kupata majibu kwani wengi walikuwa wanashindwa kumwona Diamond. Wengine waliamini kwamba, Wema alikuwa ameshikwa kiuno na mwanaume mwingine ambaye huena akampindua Diamond kama na yeye alivyompindua yule kigogo wa ikulu ‘CK’.
“Sasa mbona Wema anakubali kushikwa kiuno hivihivi tu, haoni watu?” alihoji mpita njia mmoja ambaye alijitambulisha kwa jina la Salome, mwanafunzi wa Chuo cha Ustawi wa Jamii, Kijitonyama jijini Dar.

DENDA NJE NJE
Katika hali isiyotarajiwa, baada ya kushikwa kiuno, Wema alikwenda mbali zaidi pale alipomwinamia ‘baby’ wake huyo na kula naye denda ambapo naye mwanaume hakufanya ajizi hata kidogo.

“He! Jamani! Naona wenzetu leo wameamua, hata barabarani? Huu ustaa nahisi unawafanya watu wawe vichaa mbele za watu. Mimi siwezi kabisa kudendeka mbele za watu,” alisema mrembo mmoja ambaye hakutaka kutaja jina lake lakini naye ni denti wa Chuo cha Ustawi wa Jamii ambacho kipo jirani kabisa na eneo la tukio.

DIAMOND ACHOMOKA KWA KASI
Baada ya denda hilo lililodumu kwa dakika moja, Diamond alimuaga Wema na kukanyaga mafuta kuondoka katika eneo hilo huku wananachi wakimfuatilia kwa macho yaliyojaa mshangao.

Soma Habari Kamili

HUSNA IDDI KISOMA, MKAZI WA MKOA WA PWANI ATIWA MBARONI NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA KUZINYOFOA SEHEMU ZA SIRI ZA MUMEWE KATIKA UGOMVI WA WIVU WA MAPENZI!


Jeshi la polisi mkoa wa Pwani linamshikilia Husna Iddi Kisoma (19) , mkazi wa Kisemvule Mkuranga mkoa wa Pwani kwa tuhuma za kumuua mumewe Jumane Mwalami (21) baada ya kumvuta sehemu za siri na kuzinyofoa kutokana na ugomvi uliosababishwa na wivu wa mapenzi.
 
 Akizungumza na kipindi cha Maskani cha 100.5 Times Fm, kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani, Ulrich Matei ameeleza kuwa tukio hilo lilitokea juzi usiku na kwamba kulikuwa na ugomvi kati ya wawili hao huku kijana huyo akimtuhumu mwanamke huyo kuwa na uhusiano wa kimapenzi na wanaume wengine.
 
 Ameeleza kuwa wakati ugomvi unaendelea, mwanamke huyo alizishika sehemu za siri za mumewe na kuzivuta hadi kuzinyofoa.
 
Mwanaume huyo alipata maumivu makali na alikimbizwa hospitali ya Mkulanga ambapo alifariki.
 
Jeshi la polisi limefanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo na tayari ameshafikishwa mahakamani akikabiliwa na kesi ya mauaji.

Soma Habari Kamili

DEREVA AFUMANIWA AKIFANYA MAPENZI NA CHANGUDOA NDANI YA GARI

Yelewiii!  Dereva ‘suka’ wa kampuni moja binafsi yenye makao yake makuu Kurasini jijini Dar (jina halikupatikana) Jumapili iliyopita alinaswa akifanya mapenzi na changudoa  ndani ya gari la kampuni hiyo, kikosi cha Oparesheni Fichua Maovu (OFM) kilishuhudia tukio hilo laivu.

‘suka’ baada ya kunaswa akiwa na changu (kulia).
Dereva huyo akiwa na mwenzake walifika maeneo ya Mbagala Zakhem saa 7 usiku wa Februari 16, mwaka huu bila kujua kama OFM ilikuwa katika maeneo hayo kwa ajili ya kufanya oparesheni tokomeza machangudoa.
OFM ilimshuhudia dereva huyo na mwenzake wakishuka ndani ya gari aina ya Toyota Hilux (isiyokuwa na ‘pleti’ namba upande wa  mbele) mali ya kampuni  hiyo, wakiingia kwa fujo katika moja ya madanguro maarufu na kupaki gari  kisha wakashuka kuelekea kwenye danguro la machangudoa.


Baada ya muda, mmoja wao alirejea akiwa na changudoa maarufu kwa jina la Waluwalu na kujifungia ndani ya gari hilo.
Kama kawaida yake OFM iliwataarifu askari wa Kituo cha Kizuiani waliokuwa doria katika eneo hilo ambao kwa pamoja walilivamia gari na kumuamuru dereva  ashuke.

Hata hivyo, suka huyo alikuwa mbishi akaamua kufunga milango na kupandisha vioo ili asiweze kubughudhiwa na kile alichokuwa akikifanya ndani ya gari.
Askari waliokuwa na silaha wakalizunguka gari hilo na dereva huyo alipoona mambo yamekuwa magumu alifungua mlango na kutimua mbio lakini hakufika mbali kabla ya kuwekwa chini ya ulinzi sambamba na changudoa aliyekuwa naye.

Akizungumza kwa hofu dereva huyo alisema, yeye na mwenzake ni madereva wa kampuni... (jina tunalo) na walikuwa maeneo hayo kwa bahati mbaya na si kama walifika kuwanunua machangu hao.
Dereva huyo alipotakiwa atoe sababu za kujifungia ndani ya gari hilo na changudoa kisha kutoa pleti namba ya mbele ya gari, alijitetea kwa kusema kuwa pleti namba ilidondoka barabarani tangu mchana, hivyo walikuwa wakimtafuta fundi ili awatengenezee.


na Changu wakiwa na watuhumiwa wengine walionaswa katika operesheni tokomeza uchangudoa.
Alipohojiwa changudoa waliyekuwa naye, hakuwa na lolote la kusema zaidi ya kuangua kilio na kuomba aachiwe huku akilaumu ukali wa maisha kama sababu ya kujiingiza katika biashara ya kujiuza.
Wahusika hao walifikishwa Kituo cha Polisi cha Kizuiani kabla ya kesho yake (Jumatatu) kupelekwa Mahakama ya Jiji kusomewa makosa yanayowakabili.

Soma Habari Kamili

MFANYABIASHARA KARIAKOO AFUMANIWA AKIFANYA MAPENZI NA SHEMEJI YAKE


MFANYABIASHARA maarufu wa simu za mikononi maeneo ya Kariakoo jijini Dar, aliyefahamika kwa jina moja la Devi, hivi karibuni alipatwa na soni ya aina yake baada ya kukutwa katika nyumba ya kulala wageni akiwa na mke wa rafiki yake wa karibu.
Mfanyabiashara maarufu wa simu za mikononi maeneo ya Kariakoo jijini Dar, anayefahamika kwa jina moja la Devi baada ya kufumaniwa na mke wa rafikiye.
Mtoa habari makini aliliambia gazeti hili kuwa kisa kizima kilianza baada ya mwenye mali (mume) kukuta ujumbe mfupi wa simu katika kilongalonga cha mkewe unaoashiria mambo ya mapenzi na mbaya zaidi, meseji hiyo ilitoka kwa rafiki yake huyo.
Licha ya kukuta ujumbe huo wa kimahaba, chanzo chetu kilidai kuwa pia mume huyo alikutana na sms kadhaa zilizokuwa zimetuma fedha kwa njia ya mtandao wa simu, zikielekezwa kwa dada huyo kwa ajili ya matumizi yake.
Wafumaniwa hao wakiwa chini ya ulinzi wa makamanda wa OFM.
Baada ya jamaa huyo kujiridhisha kuwa Davi alikuwa na nia mbaya na mkewe, mume huyo aliamua kuanzisha mkakati na kumtuma mdogo wake kufuatilia ishu nzima kwani yeye alibanwa na majukumu mengine ya kikazi.
Bila kujua kuwa nyendo zao zinafuatiliwa, Davi na shemeji yake walipanga kukutana katika hoteli moja (jina linahifadhiwa)iliyopo Sinza na baada ya kupata chumba na kuingia ndani, bila hofu, walianza kujiandaa kwa ajili usaliti.
Mke wa mtu baada ya fumanizi hilo.
Huku mwanaume akiwa ameshatoa nguo zake sambamba na mpenzi wake, mlango wa chumba chao uligongwa, lakini wakiwa hawana hofu,wakiamini ni mhudumu walifungua na wote kupatwa na bumbuazi baada ya kugundua aliyekuwa mbele yao ni mdogo wa mwenye mke ambaye wote wanamfahamu!
“Huwezi kuamini, baada ya sisi kuingia chumbani na kuwakuta kama walivyozaliwa, jamaa alikimbilia chooni na kwa jinsi alivyokuwa, alionyesha kabisa kuhitaji kujitumbukiza, lakini bahati nzuri vyoo vile ni vya kisasa,” kilidai chanzo hicho.
Mwandishi wetu alimtafuta kwa njia ya simu mwenye mke kutaka kujua kilichoendelea baada ya tukio hilo ambapo alipopatikana alisema:
“Ni kweli tukio hilo limetokea ila siwezi kuzungumzia zaidi, jamaa alikuwa akinizunguka kwa mke wangu lakini arobaini yake imefika, zaidi nenda Kituo cha Polisi Oysterbay utaelezwa kila kitu.”

Soma Habari Kamili

MREMBO ACHOMWA KISU BAADA YA KUFUMANIWA AKIWA NA MUME WA MTU


Amina Hussein akipata matibabu katika hospital ya taifa Muhimbili.
JESHIla polisi mkoani hapa linamshikilia mwanamke aliyejulikana kwa jina la Pima Mabubu kwa tuhuma za kumchoma kisu mpaka kumjeruhi vibaya mwanamke mwenzake, Amina Hussein akidai ana uhusiano wa kimapenzi na mumewe, Adam Ndekeja, Risasi Jumamosi lina mkasa wote.
Tukio hilo lililowaacha watu vinywa wazi, lilijiri Aprili 22, mwaka huu shambani katika Kijiji cha Kigwa, Kata ya Ukondamoyo wilayani Uyui, Mkoa wa Tabora.

KISU KILIVYOFANYA KAZI
Habari kutoka kwa baadhi ya mashuhuda zinasema kuwa, Amina alichomwa kisu mara mbili, kwenye paja mguu wa kushoto kisha kwenye mgongo ambapo kilizama na kutoka mpini tu!
Amina Hussein akikimbizwa hospital baada ya kupatwa na mkasa huo.
KISA KINASIMULIWA
Kwa mujibu wa taarifa za awali, siku ya tukio, Pima alitoka nyumbani kwake na kumfuatilia mumewe huyo kwenye shamba la tumbaku la kaka wa Amina (jina halikupatikana) ambako alisikia kuwa mwanamke huyo yupo na mumewe.
“Pima alisikia Amina ana uhusiano na mumewe. Siku hiyo akasikia wapo shambani. Akatoka nyumbani na kufuatilia akijua atawanasa laivu,” kilisema chanzo hicho.
Kisu kinachosadikika kilitumika kumjeruhi Amina Hussein.
MWANAMKE ALIYECHOMWA KISU
Akizungumza akiwa amelazwa akiuguza majeraha katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora, Kitete, Amina alisema:
“Mimi sina uhusiano na huyo mwanaume jamani. Kwanza huyo mwanamke simjui kabisa. Nimemwona kwa mara ya kwanza siku hiyo ya tukio.
“Siku hiyo mimi na mwanangu kichanga (wa miezi mitatu) tulikuwa shambani, mimi nilikuwa nikimsaidia kaka yangu kuvuna tumbaku, akaja Adam (mwenye mke) naye akawa anasaidia kuvuna. Kuna wakati nilikwenda kupumzika mahali ili nimnyonyeshe mwanangu.
“Ghafla aliibuka huyo mwanamke. Nilimwona akinifuata mimi moja kwa moja. Aliponifikia alinirukia na kuanza kunichoma kisu mgongoni na kwenye paja la kushoto.
“Ilikuwa ni hatua chache tu tokea mahali ambako mume wake alikuwa akivuna. Nilipiga kelele za kuomba msaada, mume wake akaja mbio kusaidia kwa kumdhibiti mke wake asiendelee kunichoma kisu zaidi,” alisema Amina.
Akaendelea: “Nilianguka chini na kuanza kugalagala huku damu nyingi zikinitoka. Ndipo wasamaria wema nao walifika na kumkamata Pima, wakamfunga kamba na kumpeleka ofisi ya kata ambako alipelekwa Kituo Kikuu cha Polisi Tabora.”

BODABODA YAMKIMBIZA HOSPITALI
Habari zaidi zinasema kuwa, Amina akiwa hoi na damu chapachapa, alipandishwa kwenye bodaboda na kukimbizwa kweynye hospitali ya rufaa ya mkoa kwa ajili ya matibabu huku hali yake ikionekana si ya kuridhisha.

KILA MTU NA WAKE
Taarifa zaidi zinasema kuwa, wakati ndugu wa Amina wakihaha kumshughulikia majeruhi huyo kupata matibabu kwa lengo la kuokoa uhai wake, baadhi ya ndugu wa Pima walipiga kambi nje ya kituo cha polisi wakipigania kumdhamini ndugu yao huyo.
“Ukitaka kujua msemo kwamba kila mchuma janga hula na wa kwao fuatilia mkasa huu. Wakati ndugu wa Amina wakihaha kuokoa maisha yake hospitalini, ndugu wa Pima nao walikuwa wakihangaika kuhakikisha mtuhumiwa huyo anapata dhamana ili arejee uraiani. Hakuna aliyekwenda kumjulia hali Amina,” kilisema chanzo.

KUHUSU MUME WA MTUHUMIWA
Katika hali isiyotarajiwa, mume wa mtuhumiwa huyo alikimbia kusikojulikana muda mfupi baada ya mkasa huo kutokea jambo ambalo limezua maswali yasiyo na majibu.
Wengi wamekuwa wakiuliza ni nini kimemkimbiza mwanaume huyo kama kweli yeye hana uhusiano wowote na mwanamke huyo?!
“Au kuna ukweli unafichwa? Kama hakuna ni kwa nini Adam alikimbia? Hapa kuna haja ya jeshi la polisi kumsaka mwanaume huyo mpaka kumkamata ili ukweli ujulikane,” alisema mkazi mmoja wa eneo hilo.

Soma Habari Kamili

CHUCHU: PIGA, UA LAZIMA RAY ATANIOA!


Vincent Kigosi ‘Ray’ akiwa kwenye pozi la kimahaba na Chuchu hans
LICHA ya hivi karibuni gazeti dada la hili, Risasi kumnukuu mcheza filamu mahiri Vincent Kigosi ‘Ray’ akikana kuwepo kwa mpango wa kumuoa mpenzi wake Chuchu Hans, dada huyo ambaye pia ni msanii wa fani hiyo, ameibuka na kusema piga ua lazima wataoana.
Akizungumza na gazeti hili juzikati, Chuchu alisema hana uhakika kama mpenzi wake huyo alimaanisha kile kilichoandikwa gazetini kwa vile ana mapenzi ya dhati kwake.
Vincent Kigosi ‘Ray’
“Kiukweli mimi moyo wangu unakataa kama alisema maneno hayo kwa vile ni mtu ambaye namjua ana mapenzi ya dhati kwangu,” alisema.
Chuchu Hans
Mwanadada huyo aliongeza kuwa, anahisi kuna kidudu mtu mwenye nia ya kuleta mtafaruku ndani ya uhusiano wao kwa kuchochea fitina ili mapenzi yao yavurugike.
“Unajua kuwa kuna uwezekano kabisa kuna kidudu mtu ambaye anataka kuleta mtafaruku ili tugombane bila sababu na hilo mimi sikubaliani nalo,” alisema.

Soma Habari Kamili

UKICHEPUKA MARA MOJA, INAWEZA KUYAGHARIMU MAISHA YAKO YOTE KUREJESHA UPENDO!

Jumanne iliyopita (Aprili 22), niliandika ujumbe katika akaunti zangu za mitandao ya kijamii, Facebook (Luqman Maloto), Twitter (@luqmanmaloto) na instagram (@LuqmanMaloto) wenye lengo la kushauri marafiki zangu kuheshimu mapenzi wanayopata kutoka kwa wenzi wao.
Niliandika: “Kabla hujamfanyia vitimbi mwenzi wako. Kabla hujachepuka, ukamsaliti na kumsababishia maumivu makali ya moyo pamoja na usumbufu usiomithilika katika katika maisha yake, tambua kuwa huyo mwenzi wako hukumuokota jalalani, kwamba alikuwa katupwa, katelekezwa na hakuna mwingine wa kumpenda.

“Kwamba baada ya kutupwa, eti wewe ndiye ukamuokota na kumhifadhi. Tambua kuwa yeye ni mtu kamili, anamezewa mate pia. Ukipuuza utu wake, thamani yake, uzuri wake na mapenzi yake, siku akiondoka utajuta na kuumia kwa kuwaza mazuri yake.
“Akishaondoka, hao uliowaona ni bora hawatakuthamini, watakuchezea kama nyasi za Uwanja wa Taifa. Kwa nini ujute baadaye? Wakati ni huu wa kutimiza wajibu. Mpende akupendaye, usimuumize. Ukithubutu kumuumiza, wewe utajuta zaidi zamu yako ikifika.”
Niliandika ujumbe huo baada ya kuguswa na stori ya msomaji wangu ambaye ni mwanamke. Nilikutana naye Jumanne hiyo saa 5 asubuhi, alinisimulia mkasa wake wa mapenzi, nikamshauri kwa jinsi ambavyo Mungu aliniongoza lakini nikaona si vibaya kuwaandikia marafiki zangu, kama mwenye kasumba ya kumsaliti mwenzi wake au kumfanyia vitimbi, aache.
Siku zote uwe na angalizo kuwa unapomsaliti mara moja lakini akikugundua, inaweza kukugharimu maisha yako yote kubembeleza na kujisafisha ili akupende kama ilivyokuwa mwanzo bila mafanikio.
Kitakachomfanya asirejeshe upendo wa mwanzo ni kumbukumbu za usaliti uliomfanyia na maumivu aliyoyapata.
Wengi hufanya kama utani, wakijua watachepuka mara mbili tatu bila kugundulika. Wakati wa kuanza huo uchepukaji, huwa hawawazi siku ya kunaswa na aibu ambayo wataipata. Utokaji wa njia kuu, imekuwa kama fasheni kwa wanaume na hata wanawake.
Mume ana nyumba ndogo, mke anamiliki kidumu.
Kisaikolojia, ni afadhali kwa asilimia 70 kuachana baada baada ya kufumaniana kuliko kuendelea kwa sababu upendo hauwezi kuwa kama awali.
Imani itashuka kwa kiwango kikubwa. Hata lugha ya mawasiliano hugeuka ya kukoseana adabu baada ya fumanizi.
Tahadhari kuu ndani ya kichwa chako ni kuwa kama unampenda mwenzi wako, usithubutu kufanya jaribio la usaliti hata kwa bahati mbaya. Endapo atakugundua, kuna matokeo mabaya ya aina mbili ambayo utayapata; mosi anaweza kukupiga chini jumla.
Pili ni kuwa endapo atakusamehe, ni vigumu sana kufurahia mapenzi yake kwa sababu imani yake kwako itashuka, kwa hiyo na upendo pia hautakuwa ule wa awali.
Utajisikiaje mtu ambaye alikuwa anakupa mapenzi mazito, baadaye awe anakupimia kwa kukusikilizia kwa sababu hakuamini? Akili ‘kumkichwa’.

HESHIMUPENZILAKE, LINDAPENZILAKO
Unapoingia kwenye uhusiano wa kimapenzi, lengo la juu kabisa la kwako wewe, linatakiwa liwe kumfanya mwenzi wako afurahi kuwa na wewe, vilevile na yeye awe na msukumo unaofanana na huo wa kuhakikisha unafurahia mapenzi yenu siku zote.
Kama kila mmoja ataweka nia hiyo na kuitekeleza kwa vitendo, hapo ndipo unapoweza kuona kitu kinachoitwa ‘malavidavi’ au kwa swaga za mapenzi tunaita mahabati. Ikiwa ni kielelezo kuwa wahusika wa uhusiano wanakuwa kwenye kiwango kizuri sana cha kufurahia ‘kapo’ yao.
Tatizo kubwa hutokea pale ambapo wahusika kwenye uhusiano wanakuwa wanapishana mitazamo au uamuzi. Unajua kabisa hilo unalolifanya litamuudhi mwenzi wako lakini unakosa hofu, unatenda tu. Siku akisema “nakwenda” ndipo unashtuka na kudondosha machozi.
Ni kama unavyoelewa kuwa hakuna mtu ambaye anaweza kufurahia mwenzi wake kusaliti. Unavaa ujasiri na kuanzisha uhusiano wa pembeni. Anapobaini hilo na kuondoka zake, unapiga magoti kumzuia asichukue uamuzi huo. Akiondoka unabaki kujutia ulichomfanyia.

Itaendelea wiki ijayo.

Soma Habari Kamili

ISABELA NA KALAMA WAMWAGANA

Ule uchumba wa muda mrefu wa wasanii wawili wa muziki wa kizazi kipya, Isabela Mpanda an Kalama Bakari ‘Luteni’ umevunjika kwa kinachoelezwa kuwa ni kukosekana kwa uaminifu baina yao.

Chanzo makini kilicho karibu na nyota hao wawili, kilisema kuachana kwao kunatokana na Luteni Kalama kukosa uaminifu kwa mwenzake kwani mara kadhaa, Isabela alizifuma meseji za wanawake wengine kwenye simu yake.

Kana kwamba haitoshi, Kalama ambaye ni memba wa Kundi la Gangwe Mobb, pia hivi karibuni, licha ya kutotokea kwenye sherehe za kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Isabela, lakini alishindwa hata kumtumia ujumbe wa kumtakia heri.
 “Ni kweli nimeamua kujiweka pembeni kwa sababu Kalama siyo mwaminifu, nilikuta meseji mbalimbali za mapenzi za wanawake wengine, naogopa Ukimwi, bora nikae pembeni nimuache aendelee kufanya umalaya wake maana huyu ni sikio la kufa,” alisema Isabela baada ya kutakiwa kutoa ufafanuzi wa habari hizo.
 “Kilichoniumiza zaidi, hivi karibuni ilikuwa bethidei yangu hata hajani-wish kunijulia hali wakati nilikuwa ninaumwa, bora niendelee na maisha yangu, ndiyo maana mmeona hata kwenye uzinduzi wa Global Tv kila mtu alikuja kivyake.”
 Kalama alipoulizwa kuhusiana na suala hilo alisema: “Mimi sijui kama tumeachana, lakini kama Isabela ameamua hivyo ni sawa tu, ninachojua kila mtu yupo kwake, mimi niko Tabata yeye Kijitonyama.”

Soma Habari Kamili

JINSI YA KUKARABATI PENZI LILILOCHAKAA

Inawezekana hili lisiwe geni, lakini si vibaya kukumbushana.Fanya yafuatayo kurudisha upendo uliopotea kwa mkeo:
1.Jaribu kuwahi kurudi nyumbani kama ulikuwa una kawaida ya kuchelewa
2.Jitahidi kuja na zawadi mara kwa mara unapotoka kwenye mihangaiko yako hata kama zawadi hiyo si ya gharama
3.Mbusu mkeo kila unapotaka kutoka au unaporudi nyumbani
4.Jifunze kusema ASANTE kwa kila anachokufanyia hata kama ni wajibu wake kufanya hivyo.
5.Jifunze kuijuwa hobby ya mkeo, tenga muda japo wa saa moja kwa wiki kushiriki na mkeo katika hobby yake hata kama wewe si hobby yako
6.Jifunze kumpa credit(kumsifia) kwa kile afanyacho mf. Sifia chakula alichopika, namna livyotandika kitanda, malezi yake kwa watoto,mavazi n.k
7.Kaa pamoja na familia yako angalau mara 1kwa wiki na mfanye kitu kwa pamoja as a family mf.Fanyeni general cleaness kwa pamoja as a family and take part in it fully. Hii itampendeza sana mkeo na kuona namna unavyojali familia
8.Toka pamoja na familia yako hata mara moja kwa wiki/mwezi kwa matembezi ya jioni. Si lazima muwe na gari,mnaweza kutembea kwa mguu as a family kumtembelea jirani yenu au rafiki au ndugu aliekaribu na unapoishi
9. Shiriki michezo,homeworks na watoto wako. Mf usiku kaa mezani na familia yako ukiwasaidia watoto wako home works zao au hata kuwepo tu mezani wakati wao wanafanya home works, uwepo wako si tu ni muhimu kwa watoto lakini utamuonesha mkeo namna unavyoijali familia yako.
10. Do not demand too much, pia acha kulalamika. Ikiwa unapendelea mkeo akufanyie kitu fulani na hafanyi, usimlalamikie hovyo, show her how to do it, try to be example as a leader siku zote lead by example
11.Ongeza frequencies za kumpa mkeo haki ya ndoa, kama ulikuwa unampa mara moja kwa wiki basi ongeza iwe mara mbili au tatu and do it effectively and efficiently. Kumbuka hakuna MOYO MZEE, nae pia ana ihitaji huduma hiyo mara kwa mara
12...........Ongezea
Wanaume tusiishi na wake zetu kwa mazoea! Tukarabati makovu ya ndoa zetu na turejeshe furaha na amani ndani ya ndoa
NB:Japokuwa nimezungumzia wanaume tu, ila baadhi ya nukta zinaweza kuwahusu pia WANAWAKE,so Vice Verser is true!
Poleni kwa thread ndefu ila naamini urefu si hoja,ila content matters.
Usiku mwema!

Soma Habari Kamili

SNURA AGANDWA NA MAHABA NIUE


STAA wa wimbo wa Majanga, Snura Mushi anaonekana kugandwa na mahaba niue baada ya hivi karibuni kuanika hisia zake na kuonesha dhahiri kuwa amezama vilivyo kwenye penzi motomoto la jamaa yake aitwaye Hunter Sleiyum. 
Staa wa wimbo wa Majanga, Snura Mushi akiwa kwenye mahaba mazito na boyfriend wake aitwaye Hunter Sleiyum.
Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni, Snura aliwataka wanaume wakware waache kumsumbua kwa sababu amempata mwanaume sahihi maishani mwake, anafurahia mapenzi na uzuri zaidi mpenzi wake anampenda yeye pamoja na mwanaye.
Snura Mushi akiwa na Hunter Sleiyum.
“Hata kuamua kufanya kazi hii ya kunengua majukwaani ni kwa sababu nilikwepa mambo ya kujiuza kwa wanaume, kazi hiyo siiwezi kabisa, niko tofauti na wengine wanaokubali kujiuza na kutothamini miili yao,” alisema Snura.
Mbali na kumzungumzia mpenzi wake huyo ambaye ni DJ wa Maisha Club, Snura alikanusha kuhusu taarifa za kutajwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mchezaji wa Yanga, Mrisho Ngasa.
“Huwezi kuamini, Ngasa hajawahi kutoka na mimi, alikuwa ni mshkaji tu,” alisema Snura.

Soma Habari Kamili

CHUCHU NA RAY KAMA KIM NA KANYE


KUKOPI na kupesti bila kuboresha! Mastaa wenye mapenzi kama ya njiwa kutoka kiwanda cha filamu za Kibongo, Chuchu Hans na Vincent Kigosi ‘Ray The Greatest’ wamekuwa wakitupia swaga za picha kama zile za Kim Kardashian na mwandani wake, Kanye West.
Wasanii wa filamu za Kibongo, Chuchu Hans na Vincent Kigosi ‘Ray The Greatest’ wakijiachia.
Kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii, Chuchu na Ray ambao majina yao yameunganishwa na kuwa Chura wamekuwa wakichukua sampo za picha za akina Kim nao kujifotoa kisha kuzisambaza.
“He! Mmewaona Chuchu na Ray? Eti wanakopi na kupesti swaga kama zile za Kim na Kanye kisa mapenzi yamekolea,” alisema mdau mmoja baada ya kuziona picha hizo mtandaoni.

Soma Habari Kamili

ISABELA NA KALAMA WAACHANA KIMAPENZI

Wasanii wawili wa muziki wa kizazi kipya, Isabela Mpanda 'Bella' na Kalama Bakari ‘Luteni’ wakiwa katika picha ya pamoja ndani ya Global TV Online hivi karibuni  kabla ya kumwagana.
MWISHO umewadia! Ule uchumba wa muda mrefu wa wasanii wawili wa muziki wa kizazi kipya, Isabela Mpanda an Kalama Bakari ‘Luteni’ umevunjika kwa kinachoelezwa kuwa ni kukosekana kwa uaminifu baina yao.
Chanzo makini kilicho karibu na nyota hao wawili, kilisema kuachana kwao kunatokana na Luteni Kalama kukosa uaminifu kwa mwenzake kwani mara kadhaa, Isabela alizifuma meseji za wanawake wengine kwenye simu yake.
Kalama Bakari ‘Luteni Kalama’ memba wa Kundi la Gangwe Mobb katika pozi.
Kana kwamba haitoshi, Kalama ambaye ni memba wa Kundi la Gangwe Mobb, pia hivi karibuni, licha ya kutotokea kwenye sherehe za kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Isabela, lakini alishindwa hata kumtumia ujumbe wa kumtakia heri.
“Ni kweli nimeamua kujiweka pembeni kwa sababu Kalama siyo mwaminifu, nilikuta meseji mbalimbali za mapenzi za wanawake wengine, naogopa Ukimwi, bora nikae pembeni nimuache aendelee kufanya umalaya wake maana huyu ni sikio la kufa,” alisema Isabela baada ya kutakiwa kutoa ufafanuzi wa habari hizo.
“Kilichoniumiza zaidi, hivi karibuni ilikuwa bethidei yangu hata hajani-wish kunijulia hali wakati nilikuwa ninaumwa, bora niendelee na maisha yangu, ndiyo maana mmeona hata kwenye uzinduzi wa Global Tv kila mtu alikuja kivyake.”
Kalama alipoulizwa kuhusiana na suala hilo alisema: “Mimi sijui kama tumeachana, lakini kama Isabela ameamua hivyo ni sawa tu, ninachojua kila mtu yupo kwake, mimi niko Tabata yeye Kijitonyama.”

Soma Habari Kamili

KAMA MPENZI WAKO BADO ANAWASILIANA NA ‘EX’ WAKE, FANYA HAYA!

Unapoingia katika penzi jipya, ni kipindi ambacho moyo wako unakuwa na furaha ya hali ya juu. Unaweza kuhisi unaibeba dunia nzima kwa raha ya penzi jipya, utajitahidi kumuonesha huyo uliyempata kila aina ya mahaba ilimradi aendelee kuwa na wewe na akupende zaidi
Lakini kadiri unavyozidi kukaa na mwenzako na mnavyozidi kuzoeana, ndipo unapopata nafasi ya kuyajua maisha yake kwa undani.
Taratibu utaanza kufahamu yeye ni mtu wa aina gani, kabla yako alikuwa na nani (ex wake), anatokea kwenye familia ya namna gani au anaishi katika mazingira gani.
Hapo ndipo matatizo yanapoanzia. Yawezekana kuna mambo mengi alikuficha wakati mnakutana lakini sasa unaanza kuyabaini wewe mwenyewe. Hiki ni kipindi kigumu ambacho wengi hushindwa kukivuka na matokeo yake, kukaa kwenye uhusiano wa kimapenzi kwa wiki kadhaa au miezi kadhaa ndiyo inaonekana fasheni.
Utafiti mwepesi unaonesha kuwa wanawake au wanaume wengi wanaingia kwenye uhusiano mpya baada ya ule wa awali kuvunjika au kulegalega. Ni wachache sana wanaoingia katika uhusiano ambao mwenzi wako hajawahi kuwa na mpenzi au amekaa kipindi kirefu bila kutoka na mtu yeyote.
Kwa mantiki hiyo, unapoingia katika penzi jipya, unatambua kwamba wewe siyo wa kwanza. Kuna wenzako walishatangulia kabla yako ambao mwenzi wako ndiye anayewajua kwa majina na sura.
Pia utafiti mwingine unaonesha kwamba hakuna jambo gumu kama kutengana katika uhusiano wa kimapenzi.

Kwamba hata kama mwenzako ameshakwambia hakutaki, itakuchukua muda mrefu sana kuamini kwamba kweli anamaanisha kile alichokisema.
Katika kipindi cha mwishomwisho wakati uhusiano wa kimepenzi ukielekea mwisho, lazima yule anayeachwa atakuwa anaendelea kubembeleza apewe nafasi nyingine au asamehewe kama kuna jambo alikosea.
Kwa bahati mbaya, wengi wetu huwa hatujipi muda wa kutosha unapotoka kwenye penzi la awali kuingia kwenye penzi jipya. Matokeo yake, wengi wanajikuta wameanzisha uhusiano na mtu mwingine katika muda ambao mpenzi wa awali bado hajaliafiki suala la kutengana.
Bado anabembeleza na kuamini anaweza kupata nafasi nyingine ya kurekebisha pale alipokosea ili maisha ya kimapenzi yaendelee.
Kinachotokea sasa, unakuta umekaa na mpenzi wako mpya lakini bado yule wa zamani anakupigia simu au anakufuatilia mitaani akitaka kupata muda wa kuzungumza na wewe ili myamalize na kuendelea na uhusiano.
Ni hapo ndipo unapopata nafasi ya kujua kuwa kumbe mpenzi wako alikuwa anatoka na mtu mwingine na bado anampenda ndiyo maana anampigia simu ukiwa naye, anamfuata kila anakokwenda na wakati mwingine anakuja hata ukiwa na mpenzi wako mpya.
NINI CHA KUFANYA KUKABILIANA NA HALI HIYO?
Ni ukweli usiopingika kuwa hakuna mtu anayeweza kufurahia kugundua mpenzi wake bado ana mawasiliano na mtu wake wa zamani. Ni katika kipindi hiki, wengine uzalendo unawashinda na kuamua kukubali kukaa pembeni kuepusha msongamano.

Hata hivyo, hutakiwi kuwa mwoga, kupandwa na jazba, kupigana, kutukanana au kuvunjiana heshima na x wa mpenzi wako. Itaendelea wiki ijayo.

Soma Habari Kamili

P FUNK AFUNGA NDOA YA SIRI

Mtayarishaji nguli wa muziki Bongo, Paul Mathyasse ‘P Funk’ wakati wa harusi yake.
BAADA ya kuishi maisha ya kisela kwa muda mrefu, hatimaye mtayarishaji nguli wa muziki Bongo, Paul Mathyasse ‘P Funk’ ameoa kwa siri.
Taarifa kutoka kwa chanzo makini kilichoshuhudia tukio hilo, lilichukua nafasi jijini Arusha mwishoni mwa wiki iliyopita kwa usiri mkubwa.
Imeelezwa kuwa, P Funk aliamua kumuoa rasmi mzazi mwenzake, Samira baada ya kuishi naye kwa miaka kadhaa kama mke na mume lakini haikujulikana mara moja sababu za kuweka usiri katika tukio hilo la kheri.
Maharusi wakipongezwa na ndugu na jamaa zao baada ya ndoa.
“Jamaa (P Funk) amevuta jiko rasmi kwa siri kubwa lakini ameamua kufanya siri hata sijui ni kwa nini, tukio limechukua nafasi huku Arusha na watu kadhaa walialikwa lakini mastaa siyo wengi.
“Sherehe imefana, watu wamekula, wamekunywa kwelikweli maana misosi ilikuwepo ya kumwaga,” kilisema chanzo hicho.
Chanzo hicho kilizidi kumwaga data kuwa, katika harusi hiyo, kulikuwepo na ulinzi mkali wa watu kuzuiwa kupiga picha hivyo matukio mengi kushindwa kusambaa mtandaoni.
“Daah! Ilikuwa ngumu sana, watu hawakuruhusiwa kupiga picha, hata simu zilizotumika zilikuwa zaidi ni za bwana na bibi harusi na ndugu wa karibu,” kilisema chanzo.


Mke wa P Funky.
Paparazi wetu aliposhibishwa habari hizo na baadhi ya picha kuvuja katika Mtandao wa Instagram, alimvuti waya P Funk lakini simu yake ya kiganjani iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa.
Pamoja na paparazi wetu kumtumia ujumbe mfupi na kujitambulisha, hadi tunakwenda mitamboni prodyuza huyo hakupokea huku geti la nyumbani kwake, Bamaga-Mwenge likiwa limefungwa pasipo kujulikana kama yumo au la!

Soma Habari Kamili

MIPAKA YA HAUSIGELI NDANI YA NYUMBA


TUKO ndani ya kumalizia Sikukuu ya Pasaka,  lakini moyo wangu utakuwa safi kama sikukuu hii itapita huku nikiwa nimetoa la moyoni kuhusu maisha ya wanandoa wa siku hizi.
Ninaposema wanandoa namaanisha watu wawili wa jinsi tofauti wanaoishi kama mume na mke ndani ya nyumba moja.
Katika miaka ya hivi karibuni, kimjinimjini familia nyingi zinazojiweza zimekuwa zikiajiri wasichana wa kazi (mahausigeli) kwa ajili ya kuwasaidia kazi za ndani, hilo si baya, inakubalika. Lakini hausigeli ndani ya nyumba ana mipaka yake.
HAUSIGELI, BAADAYE MAPENZI
Lakini baadhi ya familia hizohizo, wasichana hao wa kazi wamekuwa ndiyo chanzo cha ndoa kuvunjika kama siyo kuparaganyika kwa madai kwamba, akina baba wengi hujikuta wakinasa kimapenzi kwa mahausigeli hao.
Nilipata bahati ya kuzungumza na baadhi ya akina baba waliowahi kuangukia kwenye penzi la siri na wasichana wa kazi mpaka ndoa zao kuyumba, walisema tatizo ni kishawishi cha ukaribu!
HAUSIGELI KUWA MTU WA MWISHO, WA KWANZA
Kikubwa ambacho nilikibaini kuhusu madai ya kuwepo kwa ushawishi wa ukaribu ni kitendo cha baadhi ya wanafamilia, hasa mke ndani ya nyumba kumpa hausigeli kazi ya kumfungulia mlango baba mwenye nyumba endapo atakuwa amechelewa kurudi.

HAUSIGELI NA CHAKULA   CHA BABA
Si kufungua mlango tu, akina mama wengi, ukifika muda wa kulala, kazi ya kuandaa chakula cha ‘baba’ huwa ni ya msichana wa kazi. Yeye ndiye ajue maji ya kunywa yapo, sabuni ya kunawia ipo, matunda yapo, nyongeza ya chumvi inafanyika vizuri endapo baba mwenye nyumba atahitaji wakati wa kula.

HAUSIGELI NA MILANGO YA NYUMBA
Kama msichana wa kazi atamfungulia mlango baba, haina ubishi ndiye atakayefunga na kuanza kumwandalia chakula.
Kwa hesabu za harakaharaka mpaka hapo, hausigeli anakuwa mtu wa mwisho kwa siku kukutana na baba mwenye nyumba na anakuwa mtu wa kwanza kukutana naye asubuhi.
MADHARA YAKE
Madhara ya utaratibu huu ni kuibuka kwa mazoea yasiyokuwa na sababu yoyote, kama vile baba mwenye nyumba kutaniana na msichana wa kazi.
Msichana wa kazi kujenga mazoea ya kumwomba baba mwenye nyumba fedha za mahitaji yake madogomadogo kama mwanamke (yanajulikana) ambayo anapomweleza mama mwenye nyumba humwambia asubiri mshahara wake mwisho wa mwezi.  
HAUSIGELI HUTUNZA SIRI KULIKO MKE
Utafiti unaonesha kwamba, msichana wa kazi anapozoeana na baba mwenye nyumba na kupewa vijisenti vya kujikimu, hana haja ya kuambiwa asiseme kwa mama mwenye nyumba bali mwenyewe anajua wajibu wake ni kutokusema ili ‘kutuzwa’ huko kuendelee kila wakati wa uhitaji unapaofika.
Wengi wanasema wake zao si watunza siri kama mahausigeli.
Akina baba wengi waliozungumza na safu hii, walikiri kwamba mara mazoea ya msichana wa kazi na baba yanaponoga na kufikia hatua ya kumpa pesa za matumizi,
basi msichana wa kazi hawezi kununua kitu kikubwa mpaka anapopata mshahara wake wa mwisho wa mwezi na kama atanunua, mfano nguo, kuzivaa ni mpaka pale anapopokea mshahara unaotambulika.
Lengo ni kwamba, atakapoonekana na nguo mpya iwe rahisi kuaminika na mama mwenye nyumba kwamba mshahara wake ndiyo umefanya kazi hiyo.
Kama utapitia kwa umakini tangu mwanzo wa makala haya utabaini kwamba, yote niliyoyaandika yanatokana na akina mama wengi kuwapa majukumu makubwa wasaizidi wao wa ndani na hivyo kuwa ndiyo wenye nyumba na wao kuwa wasaidizi. Inachekesha sana! Huu ni ubishoo wenye kulea madhara.
MIPAKA YA HAUSIGELI NDANI YA NYUMBA
Hii ndiyo hoja ya msingi kabisa ndani ya makala haya, kwamba, kumbe kuna mipaka ya msichana wa kazi ndani ya nyumba anayoitumikia.
Itaendelea wiki ijayo.

Soma Habari Kamili

RECHO NA TID WADAIWA NI WAPENZI

Mtoto mzuri kutoka Jumba la Vipaji Tanzania (THT), Winfrida Josephat ‘Recho THT’
MALOVEE? Bosi wa Top Band, Khaleed Mohamed ‘TID’ au ‘Mzee Mnyama’ na mtoto mzuri kutoka Jumba la Vipaji Tanzania (THT), Winfrida Josephat ‘Recho THT’, wanadaiwa kuwa na uhusiano uliotafsiriwa ni wa kimapenzi, Ijumaa Wikienda limeinusa.
Kwa mujibu wa chanzo makini, wawili hao wamekuwa wakionekana pamoja sehemu mbalimbali huku wakidaiwa kupiga ‘mitungi’ kiasi cha kushindwa kuzificha hisia zao.
Bosi wa Top Band, Khaleed Mohamed ‘TID’ au ‘Mzee Mnyama’.
“Mbona ipo wazi, TID na Recho siku hizi hawafichi kitu, tena wanapopiga mitungi ndiyo kabisa, mfano mzuri ni juzikati walikuwa pamoja mjini Dodoma, waliponda raha kinomanoma,” kilitiririka chanzo hicho.
Kama ilivyo ada, wanahabari wetu waliingia mzigoni kwa kuanzia nyumbani kwa Recho, Kinondoni, Dar, wakamkosa lakini badala yake, walipatikana mashosti zake wa karibu.

“Recho kwa sasa anatoka na Mnyama na hapa tunavyoongea yupo Njombe ambapo ametimka baada ya taarifa za yeye kutoka na TID kuzagaa mtaani, halafu pia Recho siku hizi anapombeka sana na tunahisi hata ‘mambo meupe’ anatumia,” alisema shosti huyo.
Baada ya kushibishwa data hizo, waandishi wetu walitinga ofisini kwake THT, Kinondoni ambapo wanamuziki wenzake walisema staa huyo ana muda mrefu hajafika kazini hapo pasipo kutoa sababu za msingi.
Ijumaa Wikienda lilimpigia simu Recho, akafunguka:
“Kweli nakunywa pombe lakini si kiivyo watu wanavyonisema. TID ni mtu wangu kikazi wala siyo kimapenzi. Watu wamekuwa wakinishutumu kila ninapokuwa na mwanaume wanasema ni bwana’ngu kitu ambacho si cha kweli kama wanavyonizushia kuvuta bangi.

“THT siendi kwa sababu nimesafiri, hapa ninapoongea nipo Njombe. Nimekuja kutulia huku kutokana na maneno kuzidi na watu kunipakazia uongo,” alisema Recho.
Kwa upande wake TID, alipopigiwa simu, alijitetea kwa kusema kuwa yupo na Recho kikazi na wala si vinginevyo.
“Dah...! Ebwana naomba uachane na hizo habari za mapenzi, mimi ni mtu mzima nina mengi ya maendeleo ambayo natakiwa nifanye,” alisema TID.

Soma Habari Kamili

PICHA ZA HARUSI YA P-FUNK MAJANI

‘Finally I made the big move’ ni moja ya caption za picha alizoweka Producer huyu ambae mikono na akili yake vimetumika sana kuuinua muziki wa bongofleva toka inaanza enzi hizo na kina Juma Nature na wengine.
 
 
Mashallah Mr & Mrs Majani.
Mrs Majani aka Hidaya akiwa na kichuna chao.
 Maharusi mara baada ya kufunga ndoa yao.
Mabrouk to P Funk & Hidya tunawatakia kila la kheri

Soma Habari Kamili

SNURA NDANI YA PENZI ZITO NA DVJHUNTER

Snura Mushi na Dvj Hunter wa Club Maisha Ya Mjini Mbeya wakiwa katika Pozi.

Kwa mujibu wa mtu wa karibu aliozinasa picha hizo zilizopigwa huko mkoni Mbeya alisisitiza kwamba jina lake lisitajwe humu mtandaoni, Pia alizidi kufunguka kwamba kabla hajakwanyua picha hizo alibahatika kusikia maneno ya Snura kama ifuatavyo: Mimi kwa huyu jamaa sina ujanja na kamwe sitosikia la mtu ng'o! Mmmh.. Penda sana Hunter...!
Jamaa aliishia hapo akasema alikuwa anapita tu!

DVJ Hunter katika moja na mbili.

Soma Habari Kamili

JOKATE: SIJAPIGA PICHA ZA UCHI

Sexy lady Jokate Mwegelo akiwa kwenye pozi tofauti.
Sexy lady Jokate Mwegelo amekanusha vikali kuhusiana na picha za utupu zilizozagaa mitandaoni hivi karibuni kuwa si zake.
Akizungumzia ishu hiyo, Jokate ambaye pia ni mwigizaji alisema kuna mitandao imeanzisha uvumi huo kwa kuweka picha ya mtumwingine na kudai ni yeye.
“Mitandao ya kijamii inakera sana. Kila mtu anaandika habari itakayowafanya watu wafungue ‘blogi’ yake, siwezi kupiga picha ya utupu,” alisema Jokate.

Soma Habari Kamili

NAHISI SIWEZI KUENDELEA KUWA MPWEKE, NAHITAJI MUME WA KUISHI NAYE!

 
Toka niachane na boyfiend wangu ni mwaka sasa nimejitajidi kuwa mwenyewe kwa muda lakini naona sina sababu na mimi nahitaji kupendwa, nahitaji mtu wa kuwa karibu nae na kumwambia yaliyo moyoni mwangu. Nimechoka na upweke jamani.!! tatizo ni kwamba Kila atakaye nitongoza naona kama ndio wale wale tu hakuna jipya...Ila sasa nimeamua Acha number au e-mail mwenye Bahati Ntampigia tuongeee..

Soma Habari Kamili

Ungana Nasi, Like Page Yetu Hapa Chini