
STAA wa wimbo wa Majanga, Snura Mushi anaonekana kugandwa na mahaba niue baada ya hivi karibuni kuanika hisia zake na kuonesha dhahiri kuwa amezama vilivyo kwenye penzi motomoto la jamaa yake aitwaye Hunter Sleiyum.
Staa wa wimbo wa Majanga, Snura Mushi akiwa kwenye mahaba mazito na boyfriend wake aitwaye Hunter Sleiyum.Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni, Snura aliwataka wanaume wakware waache kumsumbua kwa sababu amempata mwanaume sahihi maishani mwake, anafurahia mapenzi na uzuri zaidi mpenzi wake anampenda yeye pamoja na mwanaye.
Snura Mushi akiwa na Hunter Sleiyum.
Mbali
na kumzungumzia mpenzi wake huyo ambaye ni DJ wa Maisha Club, Snura
alikanusha kuhusu taarifa za kutajwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na
mchezaji wa Yanga, Mrisho Ngasa.“Huwezi kuamini, Ngasa hajawahi kutoka na mimi, alikuwa ni mshkaji tu,” alisema Snura.
0 comments:
Post a Comment