Lionel Messi akishangilia na wachezaji wenzake wa Barcelona baada ya kufunga bao la kwanza dakika ya 67.
Pablo Zabaleta wa Man City akitolewa kwa kadi nyekundu baada ya kupewa kadi ya pili ya njano.
Wachezaji wa PSG wakifurahia kutinga Robo Fainali.
Patashika wakati wa mtanange huo.
TIMU ya Barcelona imeibuka na ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Manchester
City kwenye mpambano wa Hatua ya 16 Bora ya Michuano ya Ligi ya Mabingwa
Ulaya uliopigwa Uwanja wa Nou Camp nchini Hispania na kufanikiwa
kutinga Robo Fainali ya michuano hiyo.
Kwa matokeo hayo, Man City wameondolewa kwenye michuano hiyo kwa
kufungwa jumla ya mabao 4-1. Nayo timu ya PSG ya Ufaransa ilifanikiwa
kutinga robo fainali ya michuano hiyo baada ya ushindi wa bao 2-1 dhidi
ya Bayer Leverkusen. Leverkusen wameondolewa baada ya kufungwa jumla ya
mabao 6-1.
0 comments:
Post a Comment