
Samuel Sitta ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa kudumu wa Bunge la katiba kwa kupata jumla ya kura 487 kati ya kura zote 563 zilizopigwa na wawakilishi wa bunge hilo....
Miongoni
mwa changamoto alizoziahidi kuzishughulikia ni pamoja kulifanya bunge
hili kuwa bunge la viwango na kuahidi kutumia muda mfupi zaidi kwenye
bunge hili la Katiba sambamba na kuwashughulikia wanaotaka muungano
uvunjike.
Samuel John Sitta amewahi kuwa Spika wa Bunge la tisa na sasa ndiye
Mwenyekiti wa Kudumu wa Bunge Maalum la Katiba baada ya kushinda kwa
kura 487 dhidi ya 69 alizopata mpinzani wake ambae ni Hashim Rungwe.
Tarehe March 13 ( kesho ) zitapigwa kura kumtafuta Makamo Mwenyekiti wa Bunge
hili ambapo kulingana na sababu za kimuungano atatokea upande wa
Tanzania visiwani(Zanzibar) na kuweka usawa wa jinsia kwa hivyo
atakaechaguliwa kutoka huko atakuwa ni Mwanamke.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wakimpongeza Mhe. Sitta kwa ushindi wake wa kishindo

Wajumbe wakipiga kura.

Upigaji kura ukiendelea.




Mikono ya pongezi yazidi kumiminika

0 comments:
Post a Comment