
Dereva bajaj akijaza kuponi ya Promosheni ya Shinda Mahela na Championi.
Zawadi ambazo zitatolewa siku hiyo ni runinga bapa ‘flat screen’
itakayoambatana na dekoda yake, dinner set pamoja na jezi za michezo.Akizungumza na Championi Jumatano, Meneja wa Global Publishers ambao ni wachapishaji wa gazeti hili, Abdallah Mrisho ‘Abby Cool’, alisema wameona ni vyema wakatoa zawadi hizo siku chache kabla ya kusherehekea sikukuu ya Krismasi ili washindi wajiachie na zawadi hizo majumbani kwao huku wakiburudika na sherehe hiyo.
“Wasomaji hatutakiwi kuwaacha hivihivi kwenye sikukuu ya Krismasi kwani tumeamua kutoa zawadi mapema sana ili ikifika siku hiyo waburudike na familia zao wakiwa na ukumbusho kutoka Championi.
“Wasomaji waendelee tu kuleta kuponi zao, bado tunazipokea, cha muhimu wawahi mapema kabla ya tarehe hiyo ya kuchezeshwa droo,” alisema Mrisho.