MARTIN KADINDA ‘AMMISS’ JACK PATRICK

Modo Jack Patrick.

MWANAMITINDO maarufu Bongo, Martin Kadinda ameonesha hisia zake hadharani baada ya kutupia picha ya rafiki yake kipenzi, modo Jack Patrick mtandaoni na kuonesha kuwa amemkumbuka.
Jack alikamatwa nchini China akidaiwa alikuwa amebeba madawa ya kulevya ambapo kabla hajaondoka, walikuwa wakishirikiana kikazi na mwanamitindo huyo ambaye amemwambia mwandishi wetu kuwa waliishi kama ndugu.
Mwanamitindo maarufu Bongo, Martin Kadinda.
“Jack Patrick alikuwa zaidi ya rafiki, tuliishi vizuri, tumekula good time pamoja na mambo mengine mengi, sitaki kuongelea ishu yake iliyompata lakini kimsingi namkumbuka sana,” alisema Kadinda.

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

Post a Comment

Ungana Nasi, Like Page Yetu Hapa Chini