BATULI: MUDA WA KUVAA UCHI UMEPITA

Mwigizaji mwenye mvuto Bongo, Yobnesh Yusuph ‘Batuli’
MWIGIZAJI mwenye mvuto Bongo, Yobnesh Yusuph ‘Batuli’ amewataka wasanii wenzake wabadilike na kuvaa kama yeye kwani muda wa kuvaa nusu utupu umepitwa na wakati.
Akizungumza na paparazi wetu baada ya kutupia picha yake aliyovaa gauni refu mtandaoni, Batuli alisema: “Muda wa kuvaa utupu umepita, wasanii tunapaswa tubadilike kwani kila siku tumekuwa tukisemwa vibaya na jamii.”
Yobnesh Yusuph ‘Batuli’ akiwa kwenye pozi.
Batuli aliongeza kuwa, kama kila msanii wa kike atavaa kiheshima, wataheshimiwa na kuwa mfano wa kuigwa.

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

Post a Comment

Ungana Nasi, Like Page Yetu Hapa Chini