Marafiki katika yote hayo, inategemewa zaidi na namna wahusika
wanavyoendesha uhusiano wao; kwa maana kwamba, yote yanahitaji
ushirikiano wa wote. Hapo ndipo mwanzo wa matatizo. Wenzi wawili huwa na
tofauti za hulka.
Kwa wanawake, wengi hupenda sana kufuatilia na kuhakikisha uhusiano
unakuwa imara. Likitokea tatizo, mwanamke huwa mstari wa mbele
kulishughulikia ili mambo yaishe. Wanawake wengi hawapendi kuwa
wamewaudhi wenzi wao.

Ni wepesi wa kusahau mambo au kuyachukulia kwa wepesi. Mfano,
mwanamke wake akikasirishwa na jambo fulani, ni rahisi tu kuishia
kusema: samahani. Wakati mwingine anaweza asiseme kabisa, akijua mambo
yameshaisha. Wanawake ni tofauti. Wanafanya mambo yao kwa taratibu sana.
Hasira zao zinachelewa kuisha, lakini ni rahisi zaidi kuzimaliza kwa
kumwambia tu: nakupenda mpenzi, najua nimekosea, samahani mama.
Ni sentesi fupi sana lakini kwao ina maana na thamani kubwa sana.
Mapenzi ni sawa na bustani, wakati mwingine inahitaji kumwagiliwa na
kuwekewa mbolea. Kama ni kweli unampenda, tuliza akili na muda wako
kuhakikisha furaha yake inaendelea kuwepo.
Inamaanisha kuwa, upendo wake kwako ukitamalaki muda wote – mafanikio
ya kazi ya mikono yako yapo jirani tu. Mfanye mwanamke wako atabasamu.
Pamoja na ubize wako, tenga nafasi kidogo kwa ajili yake.
MSAMAHA SI KUJISHUSHA!
Wanaume wengi wanaamini kumwambia mwanamke samahani ni kujishusha na kuwa chini yake, si hisia sahihi. Msamaha ni uungwana. Kama kweli unampenda kwa dhati, una shaka gani kumwambia akusamehe ili uhusiano uendelee kuwa wenye nguvu?

Hutapungua mahali popote kukubali kosa, ikiwa umekosea au
kumrekebisha mwenzako badala ya kubaki bubu huku ukiwa umenuna na
kusitisha baadhi ya huduma. Kama ilivyo kwako, tambua kuwa mwanamke naye
ni binadamu, anaweza kufanya makosa lakini asijue!
Kumwambia kwa upole ni jambo zuri. Atakusikiliza, atakuelewa na atajirekebisha alipokosea. Kukaa nalo moyoni hakuna maana.
UBABE SIYO MPANGO
Wapo baadhi ya marafiki wanaamini kuwa ubabe ni sehemu ya ukamilifu wa uanaume. Siyo kweli. Huna sababu ya kuwa mkali sana au mwenye amri muda wote. Mwanamke anahitaji kubembelezwa, upendo na kuonyeshwa namna anavyothaminiwa.

Wengine wana tabia ya kuwapiga wenzi wao, kitu kidogo tu, tayari
kipigo. Vipi akikutana na mkarimu, asiyepiga na anayebembeleza?
Akiachana na wewe utamlaumu nani? Ni kweli kuna wakati mwanamke
anahitajika kukaripiwa akikosea, lakini si sawa kuwa mkali kupitiliza
wakati wote.
Wiki ijayo tutamalizia mada yetu, USIKOSE!
Wiki ijayo tutamalizia mada yetu, USIKOSE!
Joseph Shaluwa ni Mshauri wa Saikolojia ya Uhusiano anayeandikia
Magazeti ya Global Publishers. Kwa sasa anaandaa kitabu chake kipya cha
Maisha ya Ndoa.
0 comments:
Post a Comment