Watanzania watatu ni miongoni mwa washtakiwa sita wanaodaiwa kumvamia Mkuu wa Majeshi wa Rwanda aliye mafichoni , Jenerali Faustin Kayumba Nyamwasa.
Washtakiwa hao pamoja na Wanyarwanda watatu wamefikishwa katika mahakama za Afrika Kusini kujibu mashtaka hayo.
Jenerali Nyamwasa alishambuliwa wiki hii, ikiwa ni muda mfupi
baada ya mauaji ya Mkuu wa Usalama wa Taifa wa Rwanda na mpinzani wa
Rais Paul Kagame , Patrick Karegeya.
Ofisa usalama huyo aliuawa kwenye hoteli ya kifahari mwanzoni mwa mwaka huu nchini Afrika ya Kusini.
Watanzania hao wanatuhumiwa kuhusika na mkasa wa Jumatatu wiki hii
uliohusisha watu wenye silaha kuingia nyumbani kwa Mkuu wa Majeshi
wa zamani wa Rwanda, Jenerali Faustin Kayumba Nyamwasa, jijini
Johannesburg, Afrika Kusini.
Hata hivyo, Nyamwasa ambaye pia alinusurika kifo mwaka 2010, hakuwapo nyumbani siku hiyo na hivyo kupona tena.
Mwanzoni mwa mwaka huu, Karegeya aliyekimbilia Afrika Kusini mwaka
2007 baada ya kudaiwa kuwa alipanga mapinduzi ya kumng’oa Kagame
madarakani akishirikiana na Jenerali Nyamwasa, aliuawa hotelini alipokuwa
anaishi.
Wakosoaji wa Rais Kagame wamemtuhumu kuhusika na mauaji ya
Karegeya na mashambulizi ya hivi karibuni yaliyofanyika nyumbani kwa
Jenerali Nyamwasa.
Majina ya Watanzania hao hayakutajwa na haikufahamika walishirikije katika mashambulizi hayo.
Taarifa hii ni kwa mujibu wa kituo cha televisheni cha Al Jazeera iliyorushwa jana.
Credit:
Nipashe
0 comments:
Post a Comment