Chama Cha Wananchi(CUF) kimepinga wazo na rai ya kupunguza masharti ya Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 ili kulegeza nguvu zake kisheria na kuwapa fursa Watanzania Bara kumiliki ardhi Visiwani Zanzibar.
Msimamo huo umetolewa na Mkurugenzi wa Habari na
Mwasiliano ya Umma wa CUF Salum Bimani katika taarifa yake kwa vyombo
vya habari iliyotolewa jana visiwani humo, siku chache baada ya Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais(Muungano) Samia Suluhu Hassan, kushauri Katiba ya
Zanzibar kuangaliwa upya na kuwapa nafasi Watanzania Bara kumiliki ardhi
Zanzibar.
Bimani alisema kuwa suala la ardhi siyo la
Muungano tangu mkataba wa awali wenye orodha ya mambo ya Muungano na
siyo sahihi kufanyika marekebisho ili kuwapa nafasi Watanzania Bara
kumiliki ardhi Zanzibar kwani ni ndogo na ndiyo sababu hata waasisi wa
Muumgano waliamua ardhi hiyo imilikiwe na wazanzibari pekee.
0 comments:
Post a Comment