RUSHWA YA NGONO YAMTAFUNA AFISA ELIMU


AFISA Elimu Sekondari wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Julius Kakyama, anaandamwa na tuhuma nzito. Tuhuma hizi zinatoka wilayani Muleba, mkoa wa Kagera alikofanya kazi kabla ya kuhamishwa. 
 
Anadaiwa kutumia madaraka yake kuomba rushwa ya ngono; kuomba rushwa ya fedha taslimu kutoka kwa walimu, wanafunzi na watumishi wengine katika halmashauri ya Muleba.
 
Ni mazingira hayo ya kutuhumiwa huku na kule, baadhi ya walimu walisusia tafrija ya kumuaga ambayo iliandaliwa na wakuu wa shule wilayani Muleba.

>>Tanzania  daima

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

Post a Comment

Ungana Nasi, Like Page Yetu Hapa Chini