Staa wa sinema za Kibongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’
STAA
wa sinema za Kibongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’ amepata ajali ya gari wakati
akielekea Loliondo, Arusha kupata dawa ya kikombe inayotolewa na
mchungaji mstaafu, Ambilikile Mwaisapila.
Dude ameiambia Bongowood kuwa, hivi karibuni walikuwa na gari aina ya
Toyota Prado wakimpeleka mama yake kupata tiba ya ganzi mwilini ndipo
tairi lilipopasuka na gari kuangukia gema.
“Ilipoteza muelekeo, likayumba lakini nashukuru Mungu hatukuumia,
tukasaidiwa kunyanyua, tukaenda kupata tiba ya babu,” alisema Dude.
0 comments:
Post a Comment