Aisee!
Pati ya ‘bethidei’ ya klabu ya mastaa wa filamu za Kibongo ya Bongo
Movie Unity ya kutimiza miaka mitatu tangu ilipoanzishwa, ilikuwa noma
sana kwani watu walijiachia balaa.
Mwenyekiti wa Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Nyerere’ akizungumza machache mbele ya watu waliohudhuria.
Mpango mzima ambao ulishuhudiwa na Ijumaa Wikienda lililokuwa
likirandaranda ndani ya nyumba, ulichukua nafasi kwenye Ukumbi wa
Arcade uliopo Mikocheni, Dar.
Pamoja na kufana lakini shughuli hiyo ilijaa vimbwanga vya mastaa
ambao walidhihirisha kuwa yale wanayoigiza kwenye sinema ndiyo maisha
yao halisi wanapokuwa mitaani.
Steve Nyerere akikata keki.
Baadhi ya mastaa wa kike walitia fora kwa kuvaa ‘vinguo’ vya
kihasarahasara vilivyoacha nje sehemu kubwa za maumbile nyeti ya miili
yao.
“Duh! Unajua baadhi ya mastaa hawa utadhani hawana wazazi, sijui wanaona kukaa utupu ndiyo ustaa?
“Hebu waangalie wanavyotudhalilisha sisi wanawake wenzao utadhani
hawajazaliwa Tanzania, kwa nini wasibadilike?” alihoji mmoja wa mastaa
wanaojua thamani yao.
Wasanii na mashabiki wao wakicheza muziki.
Katika mambo ya ulabu, wapo baadhi ya mastaa wa kike waliolewa hadi
wakaanguka chini kama mizigo wakiwa wamevaa kihasara hivyo mambo ya
chumbani kuonekana hadharani.
Kwa upande wa mastaa wa kiume, wapo waliolewa kupita maelezo lakini kituko kilikuwa kwa chipukizi ambaye alianguka chini mithili ya papai lililodondoka lenyewe mtini kutokana na kulewa tilalila.
Kwa upande wa mastaa wa kiume, wapo waliolewa kupita maelezo lakini kituko kilikuwa kwa chipukizi ambaye alianguka chini mithili ya papai lililodondoka lenyewe mtini kutokana na kulewa tilalila.
Kwa upande wake, staa wa kike wa sinema, Salma Jabu ‘Nisha’ kwa mara
ya kwanza alionekana akiwa amevaa kihasara kwani aliacha ‘nido’ zake
nje, jambo ambalo lilizua mjadala midomoni mwa watu wakidai kwamba siyo
kawaida yake kwani ni binti wa Kiislamu.
Wapo
baadhi waliopendeza ambapo upande wa mastaa wa kike, Jacqueline Wolper
aling’aa zaidi huku Jacob Steven ‘JB’ akikimbiza upande wa wanaume kwani
alitupia bonge la suti na tai ya kipepeo cheusi.
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, ‘kaka mkubwa’ katika tasnia hiyo na mmoja wa wanahisa wa Bongo Movie Unity, Vincent Kigosi ‘Ray’ na mpenzi wake, Chuchu Hans waliingia mitini kwa kutotokea katika pati hiyo kiasi cha kuzua maswali kibao.

“Mhh! Hapa kutakuwa na namna, haiwezekani Ray na Chuchu wote waingie
mitini,” alisema mmoja wa waigizaji ambaye aliomba hifadhi ya jina.
Mastaa wengine ambao licha ya kupewa mialiko hawakuhudhuria, ni Blandina Chagula ‘Johari’ na Wema Sepetu.
0 comments:
Post a Comment