JIDE: MIMI NA GARDNER TUNAISHI KAMA KAKA NA DADA

 
Kumbe! Super woman katika Afro-Pop, Judith Wambura a.k.a Lady Jaydeee au Jide amefunguka kuwa yeye na mumewe, Gardner Habash ‘Kapteini’ kwa sasa wanaishi kama kaka na dada hivyo kuibua swali kivipi?
Akizungumza na Ijumaa Wikienda katika mahojiano maalum yaliyofanyika kwenye mgahawa wa staa huyo wa Nyumbani Lounge uliopo Ada Estate, Kinondoni jijini Dar mwishoni mwa wiki iliyopita, Jide alisema kuwa yeye na Gardner wamefikia hatua ya kuishi katika staili hiyo kutokana na mapenzi yao yaliyopitiliza.
“Gardner ananipenda sana na mimi pia vilevile nampenda sana mume wangu. Mapenzi yetu yamepitiliza hadi tunajiona kama vile tumezaliwa tumbo moja na ndiyo maana nawaambia kuwa mimi na yeye tunaishi kama kaka na dada,” alifunguka Jide.
 
Super woman katika Afro-Pop, Judith Wambura a.k.a Lady Jaydeee au Jide katika pozi na mume wake Gardner Habash ‘Kapteini’ .
Akiendelea kuzungumza kwa kujiamini, Jide alisema kuwa hadi simu ya mkononi wanatumia moja kwa ajili ya mawasiliano.
“Mimi hapa sina simu, anayo mume wangu lakini wakati mwingine nakuwa nayo mimi ila muda mwingi anakuwa nayo Gardner,” alimalizia Jide.
Kwa makala zaidi kuhusu usichokijua juu ya maisha ya Jide, nenda kurasa za nane na tisa za gazeti hili.

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

Post a Comment

Ungana Nasi, Like Page Yetu Hapa Chini