Mwanadada anayeuza nyago kwenye filamu za Kibongo, Tamrina Poshi ‘Amanda’ amejikuta katika wakati mgumu baada ya kumwagiwa matusi na mdada wa mjini aliyejulikana kwa jina la Jesca kisa kikidaiwa ni baada ya kutangaza kuwa, yeye na mume wake wa zamani, Hamis Bwela bado ni damudamu.
Akizungumza hivi karibuni na Ijumaa, Amanda alisema kuwa, Jesca
alianza kumtukana kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook akihisi huenda
yeye na Bwela bado wanaendeela wakati hakuna chochote zaidi ya ukaribu
wa kawaida tu.
“Namshangaa
sana huyu mdada kunitukana wakati hana hata hadhi ya kutukanana na
mimi, Bwela alikuwa mume wangu lakini tukaachana kwa makubaliano hivyo
hatuwezi kuwekeana kinyongo, mimi naongea naye vizuri, sasa nashangaa
kuona eti ananitukana na sijui yeye na Bwela wakoje, watu wengine
bwana!” alisema Amanda.
Credit: Gazeti la Ijumaa/ GPL
Credit: Gazeti la Ijumaa/ GPL
0 comments:
Post a Comment