Ule ugomvi uliokuwepo kwa takribani miaka miwili kati ya mastaa wakubwa na warembo Jackline Wolper na Irene Uwoya hatimaye umefikia tamati baada ya kupatanishwa juzi.
Wawili hao walidaiwa kuingia katika beef zito baada ya Uwoya kumsema Wolper vibaya kwenye media ambapo pia aliwahi kukaririwa na gazeti moja akiwa jijini Arusha akisema kuwa Wolper amemroga ili amshushe kwenye sanaa na yeye(Wolper) kuwa juu kisanaa kitu ambacho kilidaiwa kumuudhi sana Wolper.
Chanzo kimoja kilicho karibu na mastaa hao kikizungumza na Swahiliworldplanet
kilisema kuwa aliyewapatanisha ni Steve Nyerere na wote wawili
wakakubali kuondoa tofauti zao.
"Wolper na Irene Uwoya wameitwa na kupatanishwa na Steve Nyerere sasa wako poa, unajua Wolper alikasirishwa na kitendo cha Uwoya kwenda kwenye media na kumchafua kwa mambo ambayo hakufanya kipindi cha nyuma" kilisema chanzo hicho huku kikikataa kuwekwa jina lake kweupe.

0 comments:
Post a Comment