Semina ya wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba leo imelazimika kuahairishwa baada ya kuibuka vurugu ndani ya ukumbi wa Bunge.
Zogo
hilo liliumuka baada ya kuibuka kwa mvutano baina ya wajumbe
uliosababishwa na kutuhumiana kwamba zipo dalili za upendeleo
wanazofanyiwa baadhi ya wajumbe kutokana na sababu za kiitikadi za
vyama.
Hali
hiyo ya hewa ilichafuka baada ya kuibuka kwa mvutano baina ya Mjumbe
Mhe. Christopher Ole Sendeka ambaye aliingia katika mvutano na Mjumbe
wa Kamati ya Kanuni Mhe Abubakar Hamis Bakari kuhusiana na uwasilishwaji
wa majedwali ya marekebisho ya kanuni.
Awali
Mjumbe Sendeka alipewa ruksa na Mwenyekiti wa muda wa Bunge hilo Mhe
Pandu Ameir Kificho, awasilishe mapendekezo ya mabadiriko katika
kifungu cha 58 cha kanuni hizo kilichokuwa kikijadiliwa muda huo.
Lakini
baada ya Mhe Sendeka kuwasilisha mabadiriko yake, alisimama Mjumbe
Bakari ambaye kiutaratibu alipaswa kujibu hoja hiyo hasa kwa kuwa ni
mjumbe wa kamati ya kanuni.
Mhe.
Bakari alikataa kupokea hoja ya mabadiriko ya Mhe. Sendeka kwa kusema
kuwa hayakuwa yamewasilishwa kwa kufuata taratibu za uwasilishwaji wa
mabadiriko ya majedwali, na kwamba Kamati haina mapendekezo hayo hivyo
haiwezi kujibu jambo lisilo jadiliwa.
Katika
kukataa huko Bakari alikitupia lawama kiti cha Mwenyekiti huyo kwa
madai kuwa kimekuwa kikitaja majina ya wajumbe na kuwapa nafasi ya
kuongea wakati hawapo kwenye utaratibu wala hawakuwa wameomba toka
awali.
Aliongeza
kuwa si kwa Mhe. Ole Sendeka pekee, bali pia Mwenyekiti huyo amekuwa
akiataja wajumbe wengine wakiwamo Peter Serukamba pamoja na Umy Mwaimu
ambao wote hawakuwa wamewasilisha majedwali ya mapendekezo ya
marekebisho toka awali.
"Mheshimiwa
Mwenyekiti, Ole Sendeka hayupo katika orodha ya walioleta mapendekezo,
lakini nashangaa wewe unampa nafasi ya kuzungumza wakati hakuwapo kwenye
orodha yetu, kamati hatuwezi kumpa nafasi ya kujibu hoja yake
hatuitambui.
"Hata
hao wakina Ummy Mwalimu hawapo katika orodha. Mwenyekiti ukiendeleza huu
mtindo wa kuruhusu kila anayetaka kuzungumza hapa azungumze
hatutofika. tutatumia miezi 6 hapa kutengeza kanuni tu. Lazima uwe na
maamuzi kuwa wanaoleta mapendekezo hivi sasa hatupokei"alisema Mhe
Bakari
Baada
ya Mhe Bakari kumaliza kuzungumza, Mhe Kificho aliingilia kati na
kusema kuwa jambo hio linaweza kuwa limechanganywa na sekretarieti
inayoandaa na kwamba yeye binafsi amepewa majina ya waliopeleka
marekebisho hivyo anashangaa kuona kama hayapo kwa wajumbe hao.
Mhe
Kificho alitoa ruksa kwa Ole Sendeka kuongea tena, ambapo katika
mazungumzo yake alitoa kaulia akisema kuwa mapendekezo yake
aliyawasilisha mapema na kwamba kama Mhe Bakari ana itikadi zake za
vyama asimuhusishe humo.
Mhe.
Ole Sendeka alisema kuwa yeye ana uzoefu wa kanuni na kwamba alifuata
taratibu akiwa na wenzakeMhe Serukamba pamoja na Mhe Mwalimu na kwama
kama mapigo yao yanawaumiza wajumbe wengine wavumilie tu.
"Mheshimiwa
mwenyekiti tuliopo hapa ni wajumbe. Nilijua na mimi sio dhaifu kwenye
kanuni. Nnajua haki yangu kwa kuwasilisha kwa wakati, nilitimiza wajibu
wangu, kama mapigo yetu yanawaumiza.
"Kazi
yetu si kupeleka majina yetu kwa Abubakari, kama yeye ana chama chake
na hoja zetu zinamuuma, asimame na kutuweka wazi kuwa yupo katika
msimamo gani. Lakini mimi nimewasiisha kama taratibu
zinavyonitaka"alisema Ole Sendeka
Kauli
ya Mhe Sendeka ilianzisha sintofahamu ndani ya Bunge hilo baada ya
baadhi ya wajumbe kuanza kuzomea na wengine wakisiama na kutaka kupewa
ruksa ya kuzungumza huku wakiwasha vipaza sauti.
Hali
hiyo ilimuinua Mhe Kificho ambaye aliwasihi wajumbe kuacha kuingiza
masuala ya vyama hasa kwakuwa wajumbe walioingia hapo ndani
wamewakilisha makundi.
"Niwaombe
wajumbe tujitahidi sana, tusionyeshe misimamo ya vyama, tumepata
heshima kubwa ya kuwapo humu ndani hivyo si vyema kuanza kuonesha vidole
kwasababu huyu katika CCM, sijui CUF ama Chadema au kokote itaibua
hisia ambazo si vyema.
"Mheshimiwa
Ole Sendeka naona ulimi umekwenda mbali kidogo ukamgusa mheshimiwa
Bakari. Mimi naona hili jambo limekwenda nje. Kwa hiyo naomba tuwe
makini"alisema Kificho
Baada ya kauli ya Kificho, wajumbe walianza kupiga kelele wakitaka Mhe
Ole Sendeka kumwomba radhi Mjumbe Bakari huku wengine wakimtaka asifanye
hivyo.
Mhe
Kificho alitoa nafasi nyingine kwa Mhe Bakari kuzungumza, ambapo katika
mazungumzo yake ndipo fujo hizo zilipoibuka.
Katika Mazungumo yake, Mhe Bakari alisema kuwa alichosema yeye ni kwa
faida ya Bunge na nchi, na kwamba taratibu ni kuwasilisha mapema
mapendekezo na kwamba majina ya kina Sendeka hayakuwapo.
"Mimi
nilizungumza vizuri hili kuweka utaratibu mzuri wa kupokea majedwali
haya. Mheshimiwa mwenyeiti kwa bahati mbaya mdogo wangu Ole Sendeka
anadai kanuni anazijua vizuri, lakini ninachosema sifikirii..sifikirii
kama ana uzoefu wa kujua kanuni kunishinda mimi.
"Mheshimiwa
mwenyekiti toka mwaka 1980 nipo katika mabunge haya, kwa hivyo
sifikirii kama mtu katoka Simanjiro miaka kumi iliyopita anaweza akaja
hapa na kusema anajua kanuni kunizidi.
"Mimi sitaki aniombe radhi, ila ninachotaka kumfahamisha ni kwamba kuna
watu wana ujuzi zaidi kuliko yeye hivyo awe makini katika mazungumzo
yake"alisema Bakari
Kauli hiyo ilizidisha mgawanyiko katika Bunge hilo, ambapo wajumbe walisimama na kuanza kupiga meza wengine wakizomea.
Baadhi ya wajumbe walionekana wakirushiana maneno na hata kupeleka kutaka kurushiana makonde.
Hali
hiyo ilipeleka askari ambao ni wapambe wa Bunge kusogea karibu ikiwa ni
njia ya kutuliza vurugu hizo, huku wajumbe hao wakiendelea kurushiana
maneno.
Vurugu
hizo zilionekana kusambaa katika ukumbi mzima ambapo wajumbe wengine
walionekana kurushiana maneno, hali iliyopelekea Mhe Kificho kuahirisha
Semina hiyo.
Sehemu
ya Wajumbe wa Bunge maalum la Katiba wakitawanyika mara baada ya
mwenyekiti kuahirisha kikao kutokana na baadhi ya wajumbe kutoelewana
katika hoja.Semina imeahirishwa hadi saa 10.00 jioni.
Mjumbe
wa Bunge Maalum la Katiba,Mhe. Ole Sendeka akizungumza na waandishi wa
habari kuhusu tuhuma za baadhi ya wajumbe kuwa Mwenyekiti anampendelea
kwa kumpa nafasi nyingi za kuchangia hoja katika semina ya kanuni za
bunge maalum.
Mjumbe
wa Bunge la Katiba na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo,Mhe. Freeman Mbowe akiongea na waandishi wa habari nje ya
Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma leo,mara baada ya kuahirishwa kwa kikao.
Mjumbe
wa Bunge la Katiba,Mhe. Kajubi Mkajanga kutoka taasisi ya vyombo vya
Habari akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya mwemyekiti
kulazimika kiuahirisha semina ya kujadili kanuni hadi saa kumi (10:00) jioni.
Bofya hapo chini usikilize:
Bofya hapo chini usikilize:
Bofya hapo juu usikilize
0 comments:
Post a Comment