HUYU DADA ANAHITAJI MSAADA WAKO WA USHAURI KUTOKANA NA UNYAMA ALIOTENDEWA NA RAFIKI YAKE

Mwaka jana mwezi wa tisa nikiwa na rafiki zangu mara baada ya kumaliza mitihani tuliamua kwenda kujirusha.

Tulikubaliana twende tukakae pahali patulivu tukiwa sisi kama sisi yaaani mimi, evelyne, Trice na shakira.

Baada ya kufika bar mwenzetu Trice akadai rafiki yake wa kiume angependa kuja pale, tukabishana sana kuwa mbona huu ulikuwa mtoko wa sie peke yetu? Lakini baadae tukaamua tumkubalie amwite tuu hasa ukizingatia ni shemeji yetu.

Dakika chache baadae akaja shem akiwa na jamaa zake watatu na kufanya kuwa idadi ya mabinti wanne na vijana wanne wa kiume. Haiukuninigia akilini lakini nikajua kama kuna kitu nafichwa vile.

Baada ya utambulisho tuluendelea kufurahi na mazungumzo yakiendelea.Pamoja na mazungumzo bia ziliendelea kushuka mezani ingawa mimi nilikuwa nikinywa kinywaji aina ya Bavaria hata kama walinisakama nijaribu pombe kidogo.

Walizidi kunishawishi na baadae nikanyanyuka kwenda maliwatoni nilipo rudi nikaendelea kunywa bavaria yangu ingawa nikawa nahisi kama inakuwa tofauti na kichwa chazidi kuwa kizito.

Badae nikamuuliza Trice kuhusu hali ile akaniambia labda kwa kuwa nimekunywa nyingi ila akanishawishi ninywe bia moja itatulia lakini mpaka muda huo unafika nilishaanza kuona maluweluwe so ikawa vigumu kukataa.

Baada ya saa moja baadae hali yangu ikawa imebadilika nikawa sijiwezi, kitu cha mwisho nilicho kukumbuka nikuwa tuliondoka kwenda kutafuta chakula.

Asubuhi nilihamaki kujikuta naamka nikiwa katika mazingira ya kutatanisha na maanisha katika sehemu nisiyoifahamu, nikiwa katika hali hiyo mara akatokea James niliyetambulishwa jana na Trice kuwa ni kaka yake.

Katika kipindi hicho nikawa nahisi maumivu sehemu zangu za siri kama nimeingiliwa vile. Na wakati huo James akawa nae kama anaona aibu vile.

Niliamka na kuondoka haraka kurudi hostel na kumkuta Evelyne ingawa nae alionekana kuchoka.

Nikakaa nikiwaza kwa muda mrefu nikiumia sana juu ya lile tukio na baadae nikaamua kumshirikisha rafiki yangu mmoja akaniambia kuwa Trice amekua na tabia ya kuwaunganishia watu wanaume na kuwa yawezekana waliniwekea madawa.

Niliumia sana na baada kuona hali yangu.yazidi kuwa ya kinyonge mwezi wa kumi na mbili nikaenda kupima katika hospitali ya taifa ya Muhimbili ambako baada ya vipimo daktari aliniambia ya kuwa nina mimba ya miezi mitatu na nimeathirika na ugonjwa wa ukimwi.

Ni zaidi ya mwezi sasa nimekuwa nikiwaza nijiue ama nitoe mimba bila kujua la kufanya.

Rafiki kama umeguswa na hili naomba ushauri wako maana naona kama kila kitu kimekuwa jehanamu kwangu.

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

Post a Comment

Ungana Nasi, Like Page Yetu Hapa Chini