Mwenzenu
karibia yananikuta makubwa sijui itakuwaje natamani siku zigande….mimi
ni msichana wa miaka 23 nilikutana na Mkaka mmoja mwaka umepita sasa
tukawa wachumba akanitambulisha kwao na mie nikamtambulisha kwetu na
kuanza uchumba rasmi lakini katika kipindi hicho chote wakati tunaanza
nilimdanganya mimi bikira kaka wawatu akafurahi sana na kuahidi
kutonigusa mpaka siku ya harusi yetu na kweli kaka wa watu hakunigusa
mpaka leo zimebaki week mbili tufunge Harusi..na amewaambia wazazi wake
waandae zawadi watakayo nipa baada ya kunitoa bikira siku ya Harusi
tutakapofanya kwa mara ya kwanza , Eti atawapelekea shuka lenye damu
alafu nipewe zawadi ya kujitunza, ki ukweli mimi sina bikira kabisaaa,
ilitoka toka na miaka 15 ,
Naombeni ushauri hili litanitokea puani na kunipa aibu.
Naombeni ushauri hili litanitokea puani na kunipa aibu.
0 comments:
Post a Comment