Star wa filamu Swahiliwood mwenye jina kubwa kuliko umri wake
Elizabeth Michael "Lulu" amemdatisha tajiri wa mafuta mwenye asili ya
kiarabu ambaye ana makazi yake Dubai. Kwa mujibu wa Visa mwarabu huyo
ameoza kwenye penzi la Lulu hivyo anataka kumuoa kabisa huku akimuahidi
kumnunulia gari na jumba la kifahari. Habari zaidi zinasema kuwa muaribu
huyo kwasasa ameweka kambi jijini Dar es salaam huku akimtumia Dr.Cheni
ili amshawishi Lulu akubali ombi lake la kumuoa, imefikia hata Dr.Cheni
ametishwa na kasi ya tajiri huyo wa mafuta kutaka kumuoa Lulu. Hata
hivyo inadaiwa kikwazo ni dini kwani Lulu hataki kubadili dini na kuwa
muislamu huku tajiri huyo akitaka kufunga ndoa ya kiislam na Lulu.
Kikizungumza na gazeti hilo chanzo kilisema "Anamtumia Dr.Cheni ili
aweze kumshawishi Lulu lakini kinachofanya zoezi hilo kuwa gumu ni imani
ya kikristu ya Lulu kwasababu Lulu hataki kubadili kabisa dini yake
wakati jamaa anataka kumuoa kiislamu"
Lulu
0 comments:
Post a Comment