Mgombea kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo jimbo la Kalenga, Iringa Vijijini, Godfrey Mgimwa (wapili kushoto), Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu na Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Bara Mwigulu Nchemba, wakiserebuka na wananchi baada ya kuwasili katika Kijiji ya Kibebe Kata ya Ulanda kwa ajili ya mkutano wa kampeni, jana.

Mgombea
kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo jimbo la Kalenga, Iringa
Vijijini, Godfrey Mgimwa (kushoto) akiwasalimia wananchi kwa kuwapungia
mkono, baada ya kuwasili katika Kijiji ya Kibebe Kata ya Ulanda kwa
ajili ya mkutano wa kampeni. pamoja naye ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wsa
Iringa, Jesca Msambatavangu na Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Mwigulu
Nchemba.

Wananchi
wa Kijiji ya Kibebe Kata ya Ulanda, wakiwa wamembeba kumpeleka kitini
mgombea wa CCM jimbo la Kalenga Godfrey Mgimwa, alipowasili kwenye
kijiji hicho kufanya mkutano wa hadhara.

Mwenyekiti
wa CCM Iringa, Jesca Msambatavangu akihutubia mkutano wa kampeni za
uchaguzi mdogo jimbo la kalenga, katika Kijiji ya Kibebe Kata ya
Ulanda.

Ni shangwe na nderemo kwa wananchi wa kijiji ya Kibebe ya Ulanda katika mapokezi ya mgombea wa CCM alipowasili eneo lao.

Mwana-CCM
Maria Geofrey, akiwa ameketi kivulini na mtoto wake, wakati wa mkutano
wa kampeni ulipokuwa kifanyika katika Kijiji ya Kibebe Kata ya Ulanda.

Mama
akichota maji safi na salama, Kijiji ya Kibebe Kata ya Ulanda, jimbo la
Kalenga, Iringa Vijijini, wakati CCM wakiendelea na mkutano wa kampeni
katika eneo hili. Kwa mujibu wa wenyeji kisima hicho cha maji
kilichimbwa na Mbunge wa zamani wa jimbo la Kalenga, Marehemu Dk.
William Mgimwa, ambaye alifariji Januari Mosi, mwaka huu, na kusababisha
jimbo kuingia katika uchaguzi mdogo. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO.
0 comments:
Post a Comment