
Leo March 07 Kamati ya maudhui ilikua na kikao cha kusoma uamuzi dhidi ya vituo vilivyokiuka kanuni za utangazaji. Akisoma uamuzi huo mbele ya waandishi wa Habari, Mwenyekiti wa Kamati maudhui ya Tcra mama Magreth Mnyagi amevigusia vituo vitatu vilivyokiuka kanuni hizo.
Vituo vilivyopewa onyo hilo ni vituo vinavyomilikiwa na Ipp pamoja na
Sahara Media ambayo kwa Ipp onyo limepewa kituo chake cha ITV,upande wa
Sahara Media onyo limepewa kupitia vituo vyake vya Star Tv na Radio Free
Africa kwa kutangaza maudhui yanayokiuka kanuni za utangazaji za mwaka
2005.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui Injinia Margaret Mnyagi amesema kuwa
adhabu ya onyo kali imetolewa kwa ITV na Star Television kwa kurusha
tangazo la Policy Forum 3/01/2014 ITV na 06/10/2014 lenye mwelekeo wa
kichochezi, lililokusudia kuwashawishi wananchi kutolipa kodi na
kuchukia serikali nakuvunja kanuni za utangazaji za mwaka 2005,5 (a) na
6 (3).
Upande wa Radio Free Africa mnamo tarehe 27/6/2013 ilirusha wimbo wa
msanii Nash MC unaoitwa “sindano za moto” ambao ulikuwa na mwelekeo wa
kichochezi wenye ilikuwa na lengo la kuashiria uvunjifu wa amani,utulivu
na kukiuka kanuni za utangazaji za 2005 na 5(a) 15(c) na 5(m). Radio
Free Africa wamepewa onyokali na Kamati.
Ma’ Munyagi amesema kamati imeridhika kuwa vituo hivyo vinastahili
adhabu hizo na kuwa endapo vituo hivyo vitarudia tena makosa ya namna
hiyo adhabu kali itachukuliwa dhidi ya vituo hivyo.
0 comments:
Post a Comment