Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari
katika ofisi za CCM Mkoa wa Mwanza.Nape alisema kitendo cha wana CCM
kushambuliwa ni kitendo cha kinyama na kinatakiwa kikemewe na kila
mtu,pia alisisitiza Vijana wa CCM kuwalinda wapigaji kura wao siku ya
kupiga kura.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisisitiza jambo wakati wa
mkutano wake na waandishi wa Habari kwenye ofisi za CCM Mkoa wa Mwanza.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akitazama picha ya X-Ray ya
Sebastian Masonga Katibu wa UVCCM kata ya Majengo Wilaya ya
Kahama,Masonga amevunjika mkono wa kushoto baada ya kupigwa na wafuasi
wa Chadema wakati walipokua wanarejea kwenye mikutano ya kampeni za
Udiwani.
Katibu
wa NEC Itikadi na uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akimpa pole Afisa
Mtendaji wa Kata ya Ubagwe wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga ambaye
alipigwa na kutobolewa macho na wafuasi wa Chadema .
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akitoka nje ya jengo la hospitali
ya Bugando akiongozana na baadhi ya viongozi wa CCM Mkoa wa Mwanza
ambapo waliwatembelea na kuwajulia hali majeruhi walioumizwa na wafuasi
wa Chadema mjini Kahama.
0 comments:
Post a Comment