Hamisa Hassani Mobeto amezaliwa mwaka 1994 mkoani Mwanza na kabila lake ni Mnyamwezi, wengi wetu tulimfahamu baada ya kushinda taji la Miss XXL BACK TO SCHOOL BASH 2010 iliyoandaliwa na kipindi cha XXL kutoka Clouds Fm..Sasa hivi ni video Queen,ameshaonekana katika video ya Quick
Racka ft Ngwair-MY BABY.
Nyota yake ilianza kung'ara mwaka 2011 baada ya kuibuka mshindi wa pili Miss Dar Indian Ocean, mshindi wa pili Miss Kinondoni na kuingia nusu fainali ya Miss Tanzania mwaka huo wa 2011.
Hamisa amejipatia mafanikio makubwa kupitia fani ya uanamitindo na uigizaji ambapo ameshiriki kwenye maonesho mengi sana ya mavazi na filamu tofauti nchini.
Amekuwa kivutio kikubwa kwa wasichana wengi wa kitanzania na kumfanya role model wao wengi wakipenda siku moja kuwa kama yeye.
Pamoja na hayo yote Hamisa ana ndoto za kuja kuwa mmoja kati ya wafanyabiashara wenye mafanikio makubwa hapa Tanzania.Mwaka jana mwishoni hamisa ameingia mkataba na kampuni ya Buoart ambayo ni maarufu kwa umahiri wa kupiga picha zenye hadhi ya kimataifa
0 comments:
Post a Comment