Mkuu wa jeshi la polisi nchini
Akisimulia kukamatwa kwa jambazi huyo
Kamanda wa mkoa wa kipolisi Tarime/Rorya Justus Kamugisha amesema kuwa
mtuhumiwa huyo alikamatwa jioni ya Tarehe 06.02.2014 majira ya saa 1.30
na katika mahojiano ya awali ya jeshi la polisi
mtuhumiwa huyo alikiri kuhusika na matukio ya mauaji ya kuanzia tarehe
26 hadi 28 na unyang'anyi wa kutumia silaha pamoja na mengine.
Kamugisha alimtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni Bw. Chaerles Range
Kichune, 38 maafuru kama Josephat Chacha ama Joseph Charles Chacha
Msong'o mkazi wa Kenyamanyori kata ya Turwa Wilayani Tarime.
Aidha
Kamugisha amesema kuwa mtuhumiwa alimtaja Marwa Keryoba Alex 30 - 38
mkazi wa Kijiji cha Kebeyo Sirari Wilayani kuwa wanashirikiana kufanya
ujambazi na silaha ametunzia nyumbani kwake huko Musoma.
'“Polisi
baada ya kupata taarifa hizo walifuatilia hadi nyumbani kwa mtuhumiwa
ambapo walimkuta na alipo waona maasikari polisi alijaribu kukimbia huku
akiwa amebeba silaha aina ya (bunduki) SMG .Askari walipiga risasi
hewani wakimtaka kujisalimisha lakini alikaidi na kuanza kuwarushia
risasi na ndipo asikari waliendelea kurushiana risasi na hatimaye
kumpiga risasi, marehemu alifia njiani akiwa anapelekwa hospitalini kwa
matibabu,” alisema Kamugisha.
Kamugisha ameendelea kusimulia kuwa
marehemu alikutwa akiwa na Bunduki anina ya SMG moja na iliyo futwa
namba na kukatwa kitako na mtutu,magazine moja na risasi kumi katika
upekuzi nyumbani kwake polisi wamefanikiwa kupata vitu kadhaa vikiwemo
simu mbili za mkononi , CD 21 za picha mbalimbali deki moja,viatu pea
mbili na tochi mbili na mpira wa baiskeli moja na bidha mbalimbali za
dukani.
Pia Kamanda alisema tukio hilo lilitokea majira ya saa
1.45 Februari 7, 2014 katika Kijiji cha Nyabisare kata ya Bweri Mjini
Musoma mkoani Mara ambapo marehemu ameuawa kutokana na taarifa zilizo
tolewa na Bw Charles Chacha Kichune maafuru (kenonke) ambaye amemtaja marehemu
kuwa ni mshirika wake.
Kamugisha ameshukuru jeshi la polisi Mkoa
wa Tanga kwa kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi Tarime/Rorya
kuhakikisha jambazi huyo anakamatwa.Pia amewataka wananchi kuwa watulivu
na kuendelea kufanya shuguli zao kama kawaida wakati hatua zingine
zinachukuliwa .
Aidha amewataka wananchi kutoa ushirikiano na yeyote
atakaye toa taarifa ya jambazi kukamatwa atapewa zawadi ya Tsh milioni
moja papo hapo.
0 comments:
Post a Comment