Chama cha mapinduzi (CCM) kimesema kuwa kinashangazwa na kitendo cha chama cha demokrasia na maendeleo (Chadema)kutumia Helikpota kwenye chaguzi zake huku kikidai kuwa ni mkombozi wa wananchi jambo ambalo ni kujitafutia sifa na umaarufu pekee kwa wananchi.
Hayo yameelezwa na Naibu Katibu mkuu wa CCM ambaye pia ni Naibu waziri
wa fedha Mwigulu Nchemba wakati akifungua rasmi kampeni za udiwani
katika kata ya Sombetini . Mwigulu alisema kuwa CCM inashangaa sana
Chadema kutumia Helikpota kwenye chaguzi nyingi hapa nchini jambo ambalo
wanaonesha wazi kuwa wanatumia gharama kubwa kwa ajili ya kuongeza sifa
kwani gharama ambazo zinatumika hadi kumalizika kwa kampeni ni zaidi ya
Milioni 200.
Alisema kuwa Gharama ambayo inatumika kwenye uendeshaji wa Helkopta ni gharama ambayo ingeweza kuwasaidia wanachama wao. “Wananchi wa kata ya Sombetini napenda kuwaambia kuwa hata sisi wenyewe huwa tunashangaa sana ujio wa hii Helikopta na ninapenda kusema wazi helikopta hiyo inakuja ili iweze kuwazubaisha ninyi, sasa msikubali kudanganywa na helikopta bali angalieni sera za mgombea “aliongeza Mwigulu
Pia aliwataka wananchi kuhakikisha kuwa kamwe hawatumiki kwenye siasa za sifa na ushahbiki kwani siasa hizo wakati mwingine zinasababisha hata vifo vya watu ambao hawana hatia ya kufa ovyo: “wananchi mnapswa kujua na kutambua kuwa siasa za sasa zimebadilika sana msikubali kuwa mashabiki wa siasa bali mnatakiwa kuangalia zaidi sera za vyama na mahitaji yenu msije mkachagua kiongozi kwa ushabiki itawagharimu sana kwenye utendaji”aliongeza Mwigulu
Awali Mgombea Udiwani katika kata hiyo ya Sombetini kwa tiketi ya CCM Bw David Mollel alisema kuwa ana mikakati mingi sana ya
kuhakikisha kuwa anasaidia kata hiyo endapo atapata ridhaa ya
kuongoza rasmi kama diwani .David alisema kuwa changamoto ambazo
atahakikisha kuwa anazitatua ni pamoja na urekebishaji wa
barabara, uboreshaji wa masoko,kna uimarishaji wa vikundi vya wanawake
na jamii kwa ujumla
0 comments:
Post a Comment