HELIKOPTA ya Chadema maarufu kama Chopa, juzi ilipotea angani na kusababisha viongozi wa chama hicho kushindwa kufanya mkutano katika Kijiji cha Mpwayungu wilayani Chamwino, kama ilivyokuwa imepangwa kwenye ratiba.
Kwa mujibu wa ratiba iliyokuwa imepangwa, viongozi wa kitaifa ambao
ni Mwanasheria Mkuu wa chama hicho, Tundu Lissu na Mwenyekiti wa Umoja
wa Vijana (BAVICHA), walikuwa wafanye mkutano katika kijiji hicho saa 4
asubuhi.
Akizungumza na MTANZANIA, Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa
Dodoma, Steven Massawe alikiri kupotea kwa helikopta hiyo na kukanusha
kwamba hakuna njama zozote zilizofanywa na CCM kutokana na kupotea kwa
helikopta hiyo.
Kijiji cha Mpwayungu kipo katika Kata ya
Mpwayungu, ambayo nafasi ya udiwani ipo wazi na vyama vya Chadema na CCM
vyote vimesimamisha wagombea.
“Sababu kubwa ya kupotea kwa
helikopta ni tatizo la mawasiliano kama mnavyojua Kijiji cha Mpwayungu
hakina mawasiliano. Helikopta ilikuwa ifike katika Kijiji cha Mpwayungu
saa nne asubuhi, lakini Kapteni alipotea na kusababisha kukaa angani kwa
saa moja na dakika arobaini na akatua Kijiji cha Chipogolo.
“Alipofika
Chipogolo akaambiwa sio kijiji hicho chenye mkutano na akatakiwa kurudi
nyuma kwa upande wa magharibi kwa kilometa 40, hata hivyo hakufanikiwa
ikabidi arudi mjini kujaza mafuta,” alisema Massawe.
Alisema
baada ya kujaza mafuta, viongozi hao hawakwenda tena kufanya mkutano
Mpwayungu badala yake wakaenda Mpwapwa ambapo kulikuwa na mkutano
mwingine saa 7 mchana kwa mujibu wa ratiba.
“Leo (jana) hii
viongozi hao kwa kutumia helikopta wamekwenda tena Mpwayungu na
kufanikiwa kufanya mkutano majira ya saa nne asubuni na baada ya hapo
waliekea Kijiji cha Segala Wilaya ya Chamwino, baadaye wataenda Kiteto
na Moshi,” alisema.
Alisema sio kweli kwamba CCM walifanya njama
helikopta ya Chadema ipotee ili isifanye mkutano katika kijiji hicho na
kwamba Chadema na CCM vyote vilishafanya uzinduzi wa kapteni katika kata
hiyo.
“Chadema ilifanya uzinduzi wake wa kampeni katika Kata ya
Mwayungu, Januari 26 mwaka huu na CCM walifanya uzinduzi wao Januari
20,” alisema Massawe.
Naye Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa, amesema iwapo Serikali ya CCM
haitaweka mazingira ya haki kwa makundi mbalimbali ndani ya jamii kwa
ajili ya amani ya kudumu, migogoro ya ardhi italitumbukiza taifa katika
sintofahamu na hatari kubwa nchini.
Dk. Slaa aliyasema hayo
kwenye mikutano ya M4C Pamoja Daima, jana alipokuwa akiwahutubia
wananchi wa maeneo ya Iselamagazi, Kishapu, Mhunze, Itilima, Lugulu na
Bariadi.
Alisema ni haki kwa wananchi kuwa na matumaini, kwani ndiyo misingi wa amani ya kweli ambayo haihitaji kuhubiriwa jukwaani.
>>Mtanzania
>>Mtanzania
0 comments:
Post a Comment