KAULI YA KAIMU KAMANDA POLISI TEMEKE KUHUSU MOTO ULIOTEKETEZA MALI KADHAA NDANI YA GHOROFA YA NNE KATIKA JENGO LA GMC HEIGHTS HAPO JANA



Moto ulizuka jana katika ghorofa ya nne katika Jengo la GMC Heights lililopo Barabara ya Nyerere umeteketeza vitu vyote vilivyokuwamo katika chumba ambacho kinatumika kama stoo ya kuhifadhi santuri (CD) za muziki na stika zake. 
 
Moto huo ambao chanzo chake hakijafahamika ulizuka saa 7:45 mchana katika jengo hilo ambalo lina ghorofa saba na kuzua mtafaruku mkubwa kwa majirani na watu wengine wanaotumia jengo hilo.
 
Kaimu Kamanda Polisi Temeke, Ibrahim Kihongo ambaye alikuwapo eneo la tukio alisema ni mapema mno kuweza kuzungumzia moto huo ila ni kweli umetokea.
 
Kaimu Kamanda wa Kikosi cha Zimamoto na Ukoaji Wilaya ya Temeke, Uli Mbuluko alisema moto huo wamefanikiwa kuudhibiti baada ya kulazimika kufanya kazi ya ziada kuweza kuufikia baada ya kukuta mizigo ya santuri na karatasi za lebo zake.
 
“Tulifika mapema muda mfupi baada ya moto kuanza kuwaka lakini hata hivyo haikuwa rahisi kufika eneo ambako moto ulikuwa unawake kutokana na kukuta mizigo mingi katika ngazi,” alisema.
 
Kaimu kamanda huyo alibainisha kuwa chanzo cha moto huo hakijajulikana na haukujeruhi.

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

Post a Comment

Ungana Nasi, Like Page Yetu Hapa Chini