***
BENKI
Kuu ya Tanzania (BoT) imetoa sarafu maalumu ya kumbukumbu ya miaka 50
ya Mapinduzi ya Zanzibar yenye thamani ya sh 50,000. Gavana wa BoT,
Profesa Benno Ndulu, amesema kuwa sarafu hiyo iliyotengenezwa kwa madini
ya fedha kwa asilimia 92.50, imetolewa kwa ajili ya kumbukumbu tu na
haitaingizwa katika mzunguko wala kutumika kwa kulipia malipo ya aina
yoyote.
Sarafu hii imetolewa maalumu kama maadhimisho ya miaka 50 ya mapinduzi
ya Zanzibar, haitatumika kwa manunuzi.
Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki ya BoT ilimnukuu Profesa Ndulu akisema sarafu hiyo imetolewa kwa idadi ya vipande 3,000 kwa ajili ya tukio hilo na kuwahimiza wananchi kuinunua kwa ajili ya kumbukumbu hiyo.
Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki ya BoT ilimnukuu Profesa Ndulu akisema sarafu hiyo imetolewa kwa idadi ya vipande 3,000 kwa ajili ya tukio hilo na kuwahimiza wananchi kuinunua kwa ajili ya kumbukumbu hiyo.
Kwa
mujibu wa Gavana Ndulu, kutolewa kwa sarafu hiyo kunakwenda sambamba na
utaratibu wa Benki Kuu kutoa sarafu maalumu za aina hiyo kama sehemu ya
maadhimisho ya kumbukumbu ya matukio mbalimbali muhimu ya kitaifa na
kimataifa.
“Kwa
kawaida, baada ya muda, thamani ya sarafu kama hizi huongezeka na kuwa
na faida zaidi kwa wanaozimiliki,” alisema Profesa Ndulu.
Gavana
Ndulu alieleza sarafu hizo zitapatikana Januari 5 kwa bei ya sh 50,000
katika matawi ya benki za biashara zitakazokuwa zimepata sarafu hizo
kutoka Makao Makuu ya Benki Kuu, Dar es Salaam na matawi ya Benki Kuu
yaliyoko Zanzibar, Arusha, Mbeya na Mwanza.
“Benki
za biashara zinaweza pia zikasambaza sarafu hizi kupitia matawi
yake,” alisema gavana na kuongeza taarifa za usambazaji zitatolewa na
benki hizo.
Katika
sarafu hiyo, upande wa mbele unaonyesha sura ya hayati Sheikh Abeid
Aman Karume na maandishi yanayosomeka: ‘Rais wa Kwanza wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi’.
Upande
mwingine wa sarafu unaonyesha nembo ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,
maandishi yanayosomeka: “Miaka Hamsini ya Mapinduzi”, thamani ya sarafu
na miaka 1964-2014.
0 comments:
Post a Comment