Damu ya Mfanyabiashara huyo ikiwa imetapakaa katika gari lake baada ya kupigwa risasi na majambazi waliompora kiasi kikubwa cha fedha na kutoweka. |
Mfanyabiashara mmoja (Jina
Halikufahamika) Mwenye asili ya Asia ameshambuliwa na majabazi (majira
ya saa 12 Kasoro jioni )kwa kupigwa risasi katika paji la uso wake na
kisha majambazi hao kutoweka na mabegi mawili yaliyoojaa fedha.
Hata hivyo haikujulikana kwa haraka ni kiasi gani cha fedha ambacho kilikuwemo katika mabegi hayo. Wakiongea na mwandishi wetu baadhi ya mashuhuda wa tukio walidai kuwa majambazi hao walikuwa watatu na mmoja alikuwa na bunduki aina ya SMG

Wakielezea tukio hilo baadhi ya
wafanyabiashara wengine katika maeneo hayo ya mtaa wa Lindi na Kongo
(Kariakoo) walidai kwamba Mfanyabiashara huyo alitoka na kufunga duka
lake huku akiwa na mabegi mawili na Mashine ya kutolea Risiti ya EFD na
kuelekea katika gari lake dogo aina ya Suzuki Carry na Ghafla walitokea
watu wawili waliokuwa katika pikipiki na mmoja wa tatu alikuwa amesimama
pembeni kidogo na gari hiyo na kisha kuelekea moja kwa moja katika gari
hiyo na kumpiga risasi mfanya biashara huyo aliyekuwa akijiandaa
kuondosha gari lake.
Hata hivyo baadhi ya watu wamelaumu utaratibu wa wafanya biashara wengi wa kariakoo kuhifadhi fedha nyingi katika maduka na badala yake wamewataka wafanya biashara hao kutafuta mbinu mbadala itakayowaezesha kuweka fedha na mali zao salama kabisa ikiwa ni pamoja na kutumia huduma za kuhamisha fedha kwa kutumia mitandao, cheque, na hata credit card kuliko Cash kwani imekuwa kawaida kwa mtukio haya kujirudia eleo hili la Kariakoo.

0 comments:
Post a Comment