Jeshi la Polisi mkoani Morogoro limefanikiwa kukamata gari dogo aina ya Toyota Spacio likiwa limebeba mwili wa mtu aliefariki ambaye alitambulikwa kwa Jila la Khalid Kitala (47) na kukutwa na kete kadhaa za Madawa ya Kulevywa tumboni.
Polisi wa mkoa wa Morogoro waliweka
mtego wao kwenye kituo cha Mikumi na hatimaye kufanikiwa kukamata gari hilo
likiwa na watu watatu ndani (majina yao yamehifadhiwa),pipi saba za vitu vinavyosadikiwa kuwa ni dawa za
kulevya.
Mwili
huo ulipelekwa hospitali na kufanyiwa uchunguzi na kukutwa na pipi
nyingine kumi na saba tumboni mwa Marehmu huyo na inasemekana mtu huyo
alifariki akiwa Mbeya.
Watu
wote watatu ambapo wawili wanahusika na gari hilo na mmoja ni
mfanyabiashara wa Kariakoo wanashikiliwa na polisi huko Morogoro.
Kamanda wa Polisi Mkoani Morogoro,Faustine Shilogile akizungumza na wanahabari (hawapo pichani).
Hizi ndio baadhi ya Pipi zilitolewa tumboni mwa Marehemu Khalid Kitala.
Baadhi ya Makachero wa Polisi wakijadiliana jambo baada ya kuona Mwili huo.
0 comments:
Post a Comment