WANAWAKE WENGI SIKU HIZI WAMEKUWA MALIMBUKENI WA SOCIAL NETWORKS

Kuna mdada mmoja nilisoma naye chuo miaka fulani hapo nyuma, sasa jana katika pilikapilika zangu mjini, tukakutana ghafla maeneo fulani, kwa hiyo tukaanza kusalimiana na tukaona ni vizuri tusogee pembeni kwenye mgahawa fulani tukakaa. Basi tukawa tunapiga story za kawaida na kila mmoja akimwuuliza mwenzio yuko wapi na anafanya nini sasa. Katika kukaa naye kwa muda mfupi usiozidi nusu saa, kila baada ya sekunde kama 3 hadi tano nasikia simu yake (Sumsung galaxy S5) ikilia ndii, njee, ngaa, etc., huku akiishikilia na kucheza nayo muda wote! Sasa ikabidi nimwuulize mbona simu yako haiishi milio? Akajibu ni msgs - watu wananitumia msgs kutoka social networks mbalimbali.

Nikamwambia mmmhh, social networks gani hizo mpaka simu iwe busy muda wote? Akaniambia mie nipo (tena kwa madaha) karibu social networks zote halafu nina marafiki wengi sana, akaanza kunionyesha (sio kwamba sizijui, ila yeye alihisi mie ni mngoroko na sijui chochote kuhusu social networks), nami nikawa curious kufuatilia, maweeeeeeeeee! Mdada karibu kila social network unayoijua yupo na ni very active, halafu amejiunga na magroup kibao, singles, lovers without limit, love addicts, sijui magroup gani yaani basi:

- WhatsApp
-Viber
-Instagram
-Telegram
-Tango
-skype
-facebook
-Google+ (Google Talk)
-Twitter
-twoo
-flickr
etc.,

Kilichoniacha hoi ana contacts mpaka basi, yaani nimeona facebook ana marafiki wengi zaidi ya elfu, WhatsApp kama 3800 hivi, kwingine sikuendelea kuangalia.

Nikamwuuliza sasa hizi contacts zote unazitoa wapi? Akasema wengine tunakutana kwenye mishemishe lakini wengi ni kwenye mitandao.

Nikamwambia wewe hobby yako inaonekana kuchat! Akadakia "sana na kuangalia movie". Wakati naachana naye akawa anasisitiza nimpe namba ya simu tuwe tunawasiliana kupitia WhatsApp na social networks zingine, nikamwambia wewe nipe tu namba yako nikifika home nikatulia nitakuadd.

Natumaini wadada wengine wengi wa namna hii wapo!

Swali langu ni kwamba mwanaume ukikutana na mdada wa hivi ukaingia naye kwenye mahusiano, utakuwa na guts za kujipiga kifua kwamba utaweza kuclear strings na attachments zote alizozifanya? Watu wangapi amekutana nao, kutongozana nao na labda hata kusex nao?

Kwenye hizi social networks wanaume na wanawake mara nyingi hawaishii kuchat tu, bali hufikia hatua ya kutongozana na nimeona mahuasiano kadhaa ya ndoa au kiuchumba yaliyovunjika kwa wahusika kukutwa na msgs za kutongozana au kupeana miada ya kuchepuka!

Ukitaka mahusiano yako yabaki kuwa ndoto au yaingie matatani wewe mruhusu mwenzi (au jiruhusu mwenyewe) wako awe anachat, mara kushare photos na videos na watu wa jinsia tofauti - hata kama akidai ni ndugu zake, sijui kaka/dada wa hiari, sijui nilisoma naye chuo/sekondari, sijui mfanyakazi mwenzangu bila sababu ya msingi, utakuja kuniambia!

Leo ni siku ya muungano, epuka/piga marufuku mawasiliano yasiyokuwa na maana wala msingi wowote ili kudumisha muungano wa uhusiano wenu.

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

Post a Comment

Ungana Nasi, Like Page Yetu Hapa Chini