Rachel Daudi Mwegola akiwa ndani ya Global TV Online.
MSANII wa filamu Bongo, Rachel Mwegoha amefunguka ya moyoni kuwa anajuta kutamani kuolewa.
Akifanya mahojiano kupitia kipindi cha Mtu Kati kinachorushwa na Global TV Online, Rachel alisema kuwa anajuta jinsi alivyoutumia vibaya ujana wake kwa kuelekeza nguvu nyingi katika kutamani ndoa na mwisho kujikuta akiambulia maumivu.

“Nilikuwa nikitamani sana kuolewa lakini ndoto yangu iliishia kidato
cha pili baada ya kupewa ujauzito na kunifanya kukaa sana mpaka mtoto
alipofikisha umri wa miaka kumi ambapo nilipata mchumba na kuzalishwa
tena, hali ambayo ilinitesa kwani nikiwa mjamzito, mwanaume alikuwa
mlevi kupindukia,” alisema.
Rachel alizungumza mengi yahusuyo maisha yake hali iliyosababisha
kutoa Filamu ya Ahadi ya Maumivu. Ili kusikiliza mahojiano haya na
habari nyingine kibao zinazohusu mastaa na maisha ya kijamii, bofya
bango la Global TV Online kwenye www.globalpublishers.info.
0 comments:
Post a Comment