Meneja
Masoko wa Airtel akionyesha kipeperushi wakati wa uzinduzi wa huduma
mpya itakayowawezesha wateja wa Airtel kupata whatsapp, Facebook na
Twitter bure kupitia Vifurushi vya yatosha
kampuni ya simu za mkononi ya Airtel inayoongoza kwa kutoa huduma
bora imezindua huduma ya kibunifu itakayowawezesha wateja wake kupata na
kuunganishwa kwenye mitandao ya kijamii ya Facebook, Whatsapp na
twitter BURE kupitia huduma ya Airtel yatosha.
Akiongelea kuhusu huduma hiyo Mkuu wa kitengo cha mawasiliano wa
Airtel Bi Beatrice Singano Mallya alisema” sasa ni bure kabisa kwa
wateja wetu wote wa Airtel kuunganishwa na mitandao ya kijamii ya
Whatsapp, Facebook na Twitter. Airtel tunayofuraha kutoa nafasi kwa
wateja wetu kuwasiliana na marafiki na familia kupitia mitandao hii ya
kijamii bure bila makato yoyote, huku tukiendelea kuthibitisha kuwa
Airtel Yatosha ni BABA LAO!”.
Aliongeza kwa kusema mteja yoyote atakayenunua kifurushi cha data cha
yatosha kuanzia sasa iwe ni cha siku, Wiki au Mwezi vifurushi vyao vya
internet vya MB au GB hazitakatwa katika matumizi ya Facebook, Whatsapp
na Twitter na badala yake wataweza kutumia vifurushi vyao vya data
kwenye kuperuzi katika mitandao mingine kama vile YouTube na mingine
mingi kadri ya mahitaji yao”.
Akiongea kuhusu namna ya kujiunga Meneja Masoko wa Airtel Bi Upendo
Nkini alisema” ili kupata Whatsapp, Facebook na Twitter BURE wateja
watatakiwa kupiga *149*99# kisha kuchagua kifurushi kinachowafaa na
kuanza kufurahia BURE Whatsapp, Facebook na Twitter”
“Sambamba na hilo katika kuendeleza ubunifu na kurahisiaha upatikanaji wa vifurushi vya Yatosha, tumewawezesha wateja wetu kutumia simu za kununua vifurushi vya yatosha kwa ajili ya marafiki zao familia na kubaki wakiwa wameunganishwa na kufurahia mitandao hii ya kijamii ya Whatsapp, Facebook na Twitter BURE, furahia kuunganishwa katika mawasiliano kupitia mtandao wa Airtel” aliongeza Nkini

0 comments:
Post a Comment