Nyota wa Bongo Fleva, Herry Samir maarufu kama Mr. Blue akiwa kwenye pozi.
NYOTA wa Bongo Fleva, Herry Samir maarufu kama Mr. Blue amesema
wasichana warembo, Wema Sepetu na Najma ambao aliwahi kutoka nao
kimapenzi kwa nyakati tofauti miaka ya nyuma, walimfilisi kutokana na
matumizi makubwa ya fedha alipotoka nao viwanja.
Akizungumza na paparazi wetu hivi karibuni, Mr. Blue, msanii
aliyeanza kupata umaarufu akiwa bado kijana mdogo, alisema alilazimika
kutumia fedha nyingi akiwa nao, kwani vinginevyo wangemuona hana pesa,
kitu ambacho hakuwa tayari kuona kinatokea.
“Mademu wengi walikuwa wanapenda sana starehe, kila day (siku)
wanataka twende kiwanja, ndiyo maana kama unakumbuka niliyumba kimuziki.
Wema Sepetu a.k.a 'Beautiful Onyinye'.
“Wanawake wengi niliotoka nao hawajulikani, ila kuna Wema na Najma,
ilikuwa ukizama nao dukani lazima ufanye shopping (manunuzi) ya nguvu,
kuanzia laki saba, nane na kuendelea ili wakuone unazo na mademu wengi
wakisikia tu umepiga shoo, sms hazikauki kuomba uwatumie mawe (pesa),”
alisema.
Kuhusu maisha yake ya sasa, Mr. Blue alisema yamebadilika sana, kwani
hivi sasa ameoa mwanamke mwenye asili ya Kiarabu na amejaliwa kupata
mtoto mmoja, hivyo ni baba wa familia ambaye pia anakaribia kumaliza
mjengo wake siku si nyingi.
Mrembo Najma.
Hata hivyo alisema mkewe siyo maarufu, ana malengo na upendo kwani
amekuwa akimuaga kila safari anayofanya na kwamba hata yeye anaporejea
nyumbani, hupokelewa vizuri.
Mr. Blue ni mmoja kati ya wasanii wa muda mrefu ambao bado wanafanya muziki na wenye mashabiki wengi ndani na nje ya Bongo.
0 comments:
Post a Comment