MPENZI WANGU ANANITISHIA KUNILOGA

Huyu alikuwa mchumba wangu ambaye nilimpenda sana na tulikubaliana kuoana. Nilipatwa na matatizo njiani mwenzangu akanambia anaolewa na mtu mwingine (tulikuwa tunaishi mikoa tofauti). Niliumia sana na kutokana na hasira nikamwambia `Tutaona kama utaishi na huyo mwanaume.' Toka hapo sijawahi kuwasiliana naye tena!

Siku za karibuni alinitumia message kwamba anaomba kuongea na mimi, nikamtajia muda ambao ntakuwa free.
Muda huo akanipigia simu na kuanza kunilaumu `@nyalotsi kwanini umenifanyia hivi?'
Nikamuuliza, nimfenyaje?(huku nikiwa na mshangao)
`Umeniroga kila nikipata mimba inatoka, tafadhali sana nisamehe kama nilikukosea! Familia yangu itavurugika.'

Nilikata simu na kuanza kutafakari mambo mengi sana. Ina maana huyu dada kaniona mi mchawi? Mbona hata mizizi ya dawa za kawaida tu siifahamu? Hii laana gani tena? Baadaye nikakumbuka niliwahi kumtishia kwamba hataishi kwa amani na mumewe. Nikampigia simu na kumhakikishia kwamba siwezi kufanya kitu hiyo na wala sio muumini wa mambo hayo.
Nikamshauri pia waende na mumewe hospitali kufanyiwa uchunguzi wa kiafya na wataalamu.!

Kweli duniani kuna mambo!!

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

Post a Comment

Ungana Nasi, Like Page Yetu Hapa Chini