Nyota wa filamu za Kibongo, Yusuph Mlela
NYOTA
wa filamu za Kibongo, Yusuph Mlela amedaiwa kugeuka teja (mbwia madawa
ya kulevya) hali inayomsababishia ashindwe kujichanganya na wasanii
wenzake katika shughuli mbalimbali.
Kikizungumza na Amani juzikati, chanzo kilisema msanii huyo kwa sasa
anavuta unga kiasi cha uteja kujionesha waziwazi na kupoteza mwonekano
wake wa zamani.
Juzi, paparazi wetu alimtafuta Mlela na kufanikiwa kumpata nyumbani
kwao Kinondoni jijini Dar es Salaam ambapo alikuwa na haya ya kusema:
“Katika
maisha yangu sijawahi kutumia madawa ya kulevya na huwa nayapinga sana.
Wanaosema navuta ni waongo, mimi sasa hivi naitwa baba, hivyo majukumu
yameongezeka ndiyo maana sijichanganyi kivile.”
0 comments:
Post a Comment