JOHARI AZUNGUMZIA PENGO LA KANUMBA

Msanii wa Filamu Bongo, Johari.
Wikiiliyopita tulianza makala haya yamhusuyo maisha ya msanii wa Filamu Bongo, Johari, sasa endelea kufuatilia mahojiano yake mwandishi wetu Sifael Paul.
Sifael: Wewe ni miongoni mwa waigizaji wachache wakongwe, je, hadi sasa umecheza filamu ngapi?
Johari: Ni nyingi sana lakini nilizocheza kama main character (mhusika mkuu) ni zaidi ya filamu thelathini.
Sifael: Hapo katikati kulipita ukimya f’lani ukawa husikiki kabisa. Nini kilitokea?
Mrehemu Steven Kanumba.
Johari: Niliwapisha wasanii wachanga ili wapate nafasi lakini walishindwa kwa sababu wameibuka watu ambao hawakuwa serious na uigizaji badala yake walikuwa na lengo lingine (kutafuta wanaume) so tasnia iliwashinda. Ndiyo maana nikaamua kurudi kufanya kweli na tayari filamu zipo sokoni.
Sifael: Ukimya wako ulihusisha hadi kutohudhuria matukio muhimu na hasa kwenye kumbukumbu ya miaka miwili ya aliyekuwa mtu muhimu kwa tasnia, kama marehemu Kanumba. Kwa nini?
Johari: Nilikuwa nimesafiri kikazi kwenda mkoani Morogoro. Nilikuwa nashoot movie mpya. Siwezi kuitaja kwa sasa. Pia hapo katikati nilikuwa na project ya movie nilikuwa nafanya.
Kuhusu kumbukumbu ya Kanumba Aprili 7, mwaka huu, nilirudi Dar ghafla kwa ajili ya hiyo ishu lakini bahati mbaya nilichelewa kufika Dar Live (ukumbini).
Unajua inapofika siku kama hiyo nakumbuka vitu vingi sana. Bado namkumbuka sana. Huwa nikimuwaza nalia sana (akilengwalengwa na machozi). Mimi huwa simkumbuki Aprili 7 tu, hapana, huwa namuenzi Aprili 7 hadi Aprili 11 (siku aliyozikwa kwenye Makaburi ya Kinondoni, Dar).
Sifael: Kutokuwepo kwa Kanumba kuna madhara yoyote kwa tasnia ya filamu?
Johari: Katika sanaa kila mtu ana nafasi yake kwa namna alivyojitengenezea mashabiki wake. Watu wanaweza kummisi Kanumba zaidi lakini sisi RJ Productions (kampuni yake na Ray) tunammisi zaidi.
Unataka kujua kwa nini? Tumekosa ushindani. Kama utakumbuka kulikuwa na ushindani mkubwa sana kati ya RJ na Kanumba The Great. Sasa hivi hakuna kampuni ya kushindana na RJ. Angali kampuni nyingi za filamu. Sioni ambayo inaleta changamoto.
Sifael: Ni changamoto gani unakutana nazo kwenye tasnia ya filamu?
Johari: Changamoto kubwa ni kukosa mshindani halafu ndiyo linakuja suala la serikali kutambua Bongo Movies kuwa inatoa ajira kwa watu wengi hivyo kuwe na sapoti ya kutosha.
Sifael: Kuna watu wanaamini kuwa kifo cha Kanumba kimeua tasnia ya filamu. Je, ni kweli?
Johari: Kwa mtazamo wangu hiyo ni kauli ya watu wenye akili finyu.

Endelea kufuatilia makala haya wiki ijayo.

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

Post a Comment

Ungana Nasi, Like Page Yetu Hapa Chini