KhAA! Mshiriki wa Shindano la Miss
Kiswahili mwaka 2009 ambaye kwa sasa yuko nchini China akijitafutia
maisha, Rehema Fabian amenaswa laivu akiwa kimahaba na kibabu cha
kizungu.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda kwa njia
ya simu, mnyetishaji wetu ambaye naye yuko nchini humo alisema kuwa kwa
sasa mrembo huyo anajiachia na babu huyo ambaye kwa kumwangalia
harakaharaka anaweza kuwa sawa na mjukuu wake.
“Unajua mapenzi ya wazee ni mazuri sana,
kwanza wanajua kubembeleza, isitoshe hawakupi msongo wa mawazo mara kwa
mara kama yalivyo mapenzi ya vijana na ndiyo maana Rehema akaona bora
ajiachie na kibabu,” alisema mtonyaji huyo.
Baada ya kupata ‘infomesheni’ hizo, Ijumaa Wikienda lilimtafuta Rehema ili kujiridhisha kuhusiana na stori hiyo ambapo kwa upande wake alianza kucheka kisha kudai aachwe ale ujana. “Ahaha! Mshaanza mambo yenu, niacheni jamani nile ujana,” alisema Rehema.

Credits:GPL
0 comments:
Post a Comment