
Wiki iliyopita muigizaji wa filamu
nchini Kajala Masanja alikiri kuwekewa sumu wakati alipokuwa kwenye show
ya mwanamuziki Izzo Buzness. Star huyo aliwahi hospitalini na hali yake
kuwa nzuri. Hata hivyo star mmoja wa filamu akizungumza na
Swahiliworldplanet kwa sharti la kutoandikwa jina lake alisema kuwa
Kajala alifanyiwa kitendo hicho cha kifedhuli kutokana na madai ya
kutembea na mume wa mtu ambaye anadaiwa kumpangishia nyumba ya kifahari
"kachukua mume wa mtu huyo Kajala, yes kuna libaba limempangia nyumba
nzima so nahisi ndiyo sababu ya kuwekewa sumu" kilisema chanzo hicho.
Hata hivyo Kajala alijaribu kutafutwa ili kutolea ufafanuzi madai hayo lakini kwa siku mbili hakuweza kupatikana.
Hata hivyo Kajala alijaribu kutafutwa ili kutolea ufafanuzi madai hayo lakini kwa siku mbili hakuweza kupatikana.
CREDIT : SWAHILI WORLD PLANET
0 comments:
Post a Comment