
Nuru Nassoro ‘Nora’.
MWIGIZAJI mkongwe Bongo, Nuru Nassoro ‘Nora’ amefunguka kuwa anakerwa na matapeli walioibuka ambao wanawatapeli wasanii wa kike wakiwadanganya kwamba wanawachezesha filamu kumbe ‘changa la macho’.
Akistorisha na paparazi wetu, Nora alisema hivi karibuni alikutwa na
mkasa huo baada ya kupigiwa simu na wanaume wawili waliodai kwamba wana
filamu yao hivyo wanataka wamchezeshe kama mhusika mkuu (main character)
lakini baada ya kukutana nao, mazungumzo yao yalikuwa tofauti.
“Walinikera sana, waliniambia kwamba wanataka kunichezesha filamu
lakini nilipoenda kuonana nao walibadili mazungumzo na kuanza kunitaka
kimapenzi, ujinga mtupu, niliwakatalia,” alisema Nora.
0 comments:
Post a Comment