OMBA usifumaniwe! Jamaa aliyejitambulisha kwa jina la Salum Athuman
(22), amejikuta akivishwa kanga na kutembezwa mitaani baada ya kwenda
nyumbani kwa mwanaume mwenzake, Dastun Mkereti (26) kwa lengo la
kujivinjari na mke wa mtu, Stela Ramadhan (20), akafumaniwa.
Tukio hilo lililofunga mitaa lilijiri maeneo ya Temeke, Dar, hivi karibuni na kugeuka sinema ya bure.
Kama ilivyo ada, kikosi kazi cha Oparesheni Fichua Maovu (OFM) cha Global Publishers kilichopania kutokomeza maovu nchini, wiki hii kilitinga maeneo hayo baada ya kutonywa na Mkereti kwamba kuna njemba anamsumbua mkewe.
Kama ilivyo ada, kikosi kazi cha Oparesheni Fichua Maovu (OFM) cha Global Publishers kilichopania kutokomeza maovu nchini, wiki hii kilitinga maeneo hayo baada ya kutonywa na Mkereti kwamba kuna njemba anamsumbua mkewe.
Alidai kuwa jamaa huyo amekuwa akimsumbua mkewe kwenye simu kwa
kutaka waonane ili wavunje amri ya sita huku akijua fika kuwa Stela ni
mke wa mtu na alishapewa onyo mara nyingi na mwenye mke.
Alifunguka kuwa cha kushangaza, pamoja na mwanamke huyo kubadili
namba ya simu, wiki iliyopita jamaa alimpigia Stela kisha akamsisitiza
waonane, ikibidi alale naye siku nzima kwa kuwa alikuwa anataka
kukumbushia enzi zao kwa sababu aliwahi kutoka naye kimapenzi, kipindi
cha nyuma kabla hajaingia kwenye ndoa.
Mkereti alisema kwamba baada ya kuona ndoa yake iko shakani kutokana
na pepo la usaliti kumnyemelea mkewe, alimwambia mama watoto wake
amruhusu kidume huyo waonane, ikibidi wakutane nyumbani kwake kwa
kumdanganya kuwa haishi naye kwa sasa japo ndoa yao bado changa.
Alitiririka kwamba bila woga, njemba huyo alimpigia simu Stela na
kumtaka amuelekeze kwake ili afike na kujiachia ‘kimalavu’ siku nzima.
Mkereti ambaye ni mfanyabiashara, alisema siku hiyo hakwenda kusaka
‘bingo’ ili kumwekea mtego ‘mwizi’ wake aliyemsumbua kwa muda mrefu.
Wanandoa hao, wakiwa ndani wakimsubiri mgeni wao, mishale ya saa 8:00
mchana ndipo jamaa akatinga akiwa amepigilia pamba kali kwa lengo la
kumshawishi bishosti huyo aisaliti ndoa yake bila kujua mumewe
alikuwepo.
Alifunguka kwamba Salum alipofika, Stela alimkaribisha na kuketi huku yeye (Mkereti) akiwa amejibanza chobingo.
Alisema alimshuhudia mgoni huyo akijinafasi na kutawala nyumba kama
kwake huku akidai chakula na kukumbushia ombi lake la kulala na Stela
siku nzima.
Baada ya mambo kukaa sawa, ndipo Mkereti akawashtua OFM waliokuwa wanaujua mchezo.
Wakati jamaa akiwa tayari amesaula tayari kwa mchezo ndipo Mkereti na OFM wakamfuma laivu.
Wakati jamaa akiwa tayari amesaula tayari kwa mchezo ndipo Mkereti na OFM wakamfuma laivu.
Kwa kushirikiana na Mjumbe wa Serikali ya Mtaa, Gido Herman pamoja na
majirani wa wanandoa hao, walimhoji jamaa huyo kwa nini amekuwa
akimsumbua Stela, akatoa ufafanuzi wake.
“Jamani naomba mnisamehe, sina sababu yoyote lakini mimi na Stela
tulipendana sana kipindi hicho, sikujua kama nimewekewa mtego.”
Hata hivyo, Mkereti aligoma kumwachia au kumpeleka Salum kituo cha
polisi tangu mchana hadi saa 3:00 usiku alipomtoa kisha akafungwa kanga
na kuanza kumtembeza mitaani hadi polisi.
Wakiwa mitaani, watu waliojitokeza kushuhudia kituko hicho walikuwa wakimwimbia jamaa huyo nyimbo za kuudhi.”
Wakiwa mitaani, watu waliojitokeza kushuhudia kituko hicho walikuwa wakimwimbia jamaa huyo nyimbo za kuudhi.”
Alipofikishwa Kituo Kidogo cha Polisi, Temeke-Super Mini alifunguliwa
jalada la kesi namba WPP/RB/235/2014 TAARIFA kisha akachukuliwa maelezo
na kuwekwa lupango kusubiri hatua za kisheria.
0 comments:
Post a Comment