MJUMBE AMTAKA JK AVUNJE BUNGE LA KATIBA


 
Rais Jakaya Kikwete.
KUFUATIA sintofahamu inayozuka kila kukicha ndani ya Bunge Maalum la Katiba mjini Dodoma, mbunge mmoja wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (jina tunalo) ameibuka na kumtaka Rais Kikwete ‘JK’ kulivunja bunge hilo.

Akizugumza na Ijumaa Wikienda Jumamosi iliyopita kwa sharti la kutoandikwa jina lake gazetini, mbunge huyo kutoka Chama cha Mapinduzi ‘CCM’ ambaye kwa sasa ni mjumbe, alisema kuwa hali ilivyo sasa bungeni kuna uwezekano mkubwa wa kutokuwepo kwa faida ya kikao hicho.

“Kila siku hili, mara lile. Watu wazima lakini mambo yao ni kama watoto wadogo, mimi namshauri JK aamue kulivunja hili bunge halafu mchakato wa rasimu ya katiba upelekwe kwa wananchi wakaupigie kura,” alisema mbunge huyo akionesha jazba.

Aliendelea kuweka wazi kwamba kinachomshangaza wenye vurugu ndani ya bunge hilo ni pamoja na wabunge wa zamani ambao hawatokani na wale 201 aliowachagua rais.
“Mimi nashangaa sana, tena wabunge wengine wenye vurugu ni wale wazoefu si wale wajumbe  wa JK, sasa tunakwenda wapi? Siamini kama kweli hili bunge litakwenda hadi kumalizika,” alisema mheshimiwa huyo. 

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

Post a Comment

Ungana Nasi, Like Page Yetu Hapa Chini