STAA wa filamu za Kibongo, Ruth Suka ‘Mainda’ amejikuta akikumbuka pete aliyovishwa na aliyekuwa mchumba wake, marehemu Saidi Banda ‘Max’ na kusema ataendelea kumuombea kwani alikuwa ni mwanaume aliyekuwa na malengo makubwa kwake.
Mainda alifunguka hayo kupitia mtandao mmoja wa kijamii na kusema kuwa
kila akiziona picha za siku alipovishwa pete ya uchumba, anajikuta
akitokwa na machozi.
“Miaka inakimbia sana miss u so much…! Kama ndoto vile, siku ile sitaki kuikumbuka ila kwa yote namshukuru Mungu.
“Asante Saidi kwa sababu ulionyesha kuwa una malengo makubwa na mimi
mpaka sasa ningekuwa naitwa Mrs, upendo wako kwangu bado upo sanaa ila
hilo ulilolianzisha kwenye kidole changu japo ndoto haikukamilika
kupitia wewe litatendeka, asanteni wote mlioshiriki siku ya hili tukio
akiwemo Nina na Dotnata,” aliandika Mainda.
@ GPL
0 comments:
Post a Comment