Staa Elizabeth Michael ‘Lulu’ katika pozi.
E
LIZABETH Michael ‘Lulu’ anayetesa katika filamu za Kibongo, yupo kwenye
bifu zito na mshiriki wa Miss Tanzania mwaka 2012, Husna Maulid ambaye
anadai amempora bwana’ke.
Habari zinaeleza bifu lao limefikia hatua ya kuanikana waziwazi hadi
kumwagiana matusi kwenye mitandao ya kijamii, hasa Instagram lakini
huondoa majibizano yao machafu kila baada ya muda mfupi.
Chanzo cha habari hizi kinapasha kuwa ugomvi wa Lulu na Husna ni juu
ya mwanaume huyo ambaye anaishi jijini Arusha aliyetajwa kwa jina moja
la Seki anayeelezwa kuwa na pesa za kutosha kusumbua mjini. “Hao
wanamgombea jamaa fulani wa Arusha, anaitwa Seki, ana mawe (pesa) mbaya.
Mshiriki wa Miss Tanzania mwaka 2012, Husna Maulid.
Lakini wa kwanza kuwa na Seki ni Husna na Lulu alijua, sema Husna na
huyo jamaa walikuwa wanagombana na kumwagana mara kwa mara. Sijui sasa
nini kilimfanya Lulu kwenda kutembea tena na huyo jamaa wakati anajua ni
wa shoga yake, labda ni baada ya kujua wamemwagana,” kilipasha chanzo
hicho.
Elizabeth Michael ‘Lulu’.
Baada ya kupata habari hizi, mwandishi wetu aliwatafuta Lulu na Husna
kwa ajili ya kuthibitisha madai hayo. Lulu alikuwa wa kwanza kupatikana
ambapo alisema: “Jamani mimi simjui kabisa Husna Maulid wala hata
katika fikra zangu hayupo... yaani kifupi simjui.”
Husna alipopatikana na kuelezwa mkanda mzima, kwanza alishangaa Lulu
kutomjua, akasema: “Hakuna mtu asiyejua kuwa Lulu kanipora mwanaume
wangu. Lakini anajifanya mjanja, tutaoneshana tu. Anajidai sana,
anajifanya wa mjini hanijui mimi, lakini mimi ni wa mjini zaidi yake.”
0 comments:
Post a Comment