Nyota wa muvi za Kibongo, Kajala Masanja.
NI madai mazito! Kwamba, nyota wa muvi za Kibongo, Kajala Masanja
amehongwa gari na mtu anayedaiwa kuwa ni kigogo wa Ikulu. Hii ndiyo
habari ya mjini kwa sasa na Risasi Jumamosi limeifukunyua.
Kwa mujibu wa habari hizo ambazo zipo hadi kwenye mitandao ya
kijamii, hasa Instagram, Kajala alinunuliwa gari hilo aina ya Toyota
Brevis lenye rangi ya bluu iliyoiva wiki mbili zilizopita mara baada ya
kutua Bongo akitokea nchini China ambako alikwenda kwa mambo yake
binafsi.
Brevis aina ya gari aliyonunuliwa Kajala.
TAARIFA ZINAVYODAI
Wasambaza taarifa hao walidai kuwa, kigogo huyo wa Ikulu ni yule Clement ambaye amewahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi wa Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu.
Wasambaza taarifa hao walidai kuwa, kigogo huyo wa Ikulu ni yule Clement ambaye amewahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi wa Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu.
“Mmeisikia hii? Kajala amenunuliwa gari na Kile (Clement), lina
thamani ya shilingi milioni kumi na moja, Wema alie tu nakwambia. We
ukisema cha nini wenzako wanajiuliza watakipata lini?
Muonekano wa ndani wa gari aina ya Brevis.
“Kwanza mnajua kama bifu la Wema na Kajala lilitokana na Clement?
Alipoachana na Wema akatua kwa msichana anaitwa Naima, lakini akaona
bado akaenda hadi kwa Kajala. Wema alipogundua ndiyo akamnunia na kuanza
ushoga na Aunt Ezekiel,” msambaza habari za mjini mmoja aliliambia
Risasi Jumamosi juzi.
Akaendelea: “Unajua nini? Naamini Wema alimwacha yule bwana na
akurudi kwa Diamond baada ya kuona mambo yake siyo mazuri, lakini sasa
jamaa (kigogo wa Ikulu) mambo ni safi kwa hiyo anataka kumwoneshea Wema
ndiyo maana ameamua kumnunulia gari Kajala baada ya kuwa naye.” RISASI LALISAKA MITAANI
Baada ya kuzinyaka habari hizo za kimjini, timu ya waandishi wa Risasi Jumamosi, Jumatano iliyopita iliingia mitaani kulisaka gari hilo hasa baada ya Kajala kutopokea simu.
Baada ya kuzinyaka habari hizo za kimjini, timu ya waandishi wa Risasi Jumamosi, Jumatano iliyopita iliingia mitaani kulisaka gari hilo hasa baada ya Kajala kutopokea simu.
Awali, mtoa habari mmoja alisema Kajala yupo na gari hilo Kinondoni kwa Manyanya, lakini alipofuatwa hapo hakuonekana.
Habari zikapatikana kwamba, alikuwa kwenye Mgahawa wa Steers uliopo jengo la Millennium Tower, lakini pia alipofuatwa eneo hilo hakuonekana. ALHAMISI SAA 9:06 ALASIRI
Juzi, saa 9:06 alasiri, Kajala alipigiwa simu ambapo alipokea na mahojiano yakawa hivi:
Risasi: Mambo Kajala?
Kajala: Poa tu, mambo?

Risasi: Mambo poa. Eti, namba za gari lako Toyota Brevis ni ngapi?
Kajala: Mh! Yaani hata mimi mwenyewe sizijui, sijazishika kabisa.
Risasi: Sasa, kuna habari kwamba hilo gari umenunuliwa na Clement, yule aliyekuwa na Wema zamani. Kuna ukweli wowote?
Kajala: Mh! Yaani hata mimi mwenyewe sizijui, sijazishika kabisa.
Risasi: Sasa, kuna habari kwamba hilo gari umenunuliwa na Clement, yule aliyekuwa na Wema zamani. Kuna ukweli wowote?
Kajala: Mh! Hizo habari si za kweli. Wapo watu wanajiita Team Wema
ndiyo wameamua kunipakazia hivyo, wameandika hadi kwenye Instagram,
lakini siyo kweli kabisa.
“Mimi nimelinunua hili gari kwa mtu. Aliniuzia kwa shilingi milioni
kumi na moja (11,000,000). Sijahongwa wala sijanunuliwa. Kuna watu
wanataka kunichafua tu.
KUHUSU USHOGA WAO KUFA
Kuhusu kufa kwa ushoga wao, awali Kajala hakutaka kulizungumzia suala hilo lakini alipobanwa alidai hana tatizo na Wema na kwamba kwa sasa yuko bize kutengeneza filamu zake.
WEMA AKWEPA SIMU
Kwa upande wake, Wema alipopigiwa simu hakupokea lakini siku za nyuma aliwahi kuanika kwamba haamini kama Kajala anaweza kutembea na Clement. Hapo ni wakati ule wakiwa mashoga.
TUJIKUMBUSHE
Katika gazeti la Ijumaa, Machi 21, mwaka huu ukurasa wa mbele kulikuwa na habari ndogo yenye kichwa;

WEMA, KAJALA KIMENUKA!
Katika habari hiyo, ilidaiwa kuwa, wawili hao si mashoga tena huku sababu mbalimbali zikianikwa.
Ilidaiwa kuwa, kisa kilianzia kwenye saluni moja Kinondoni, Dar ambapo Kajala alifika akiendesha baiskeli iliyosababisha kuloa jasho sehemu kubwa ya mwili.

Chanzo kilisema, Wema alipomuona Kajala alitaka kumkumbatia lakini
Kajala alimkwepa kwa sababu alikuwa na jasho jambo lililomfedhehesha
Wema na kununa.
“Alichokifanya Wema, alimrushia Kajala maneno makali akimhoji kwa nini alimfanyia hivyo wakati hawana tatizo lolote kati yao,” kilidai chanzo.
“Alichokifanya Wema, alimrushia Kajala maneno makali akimhoji kwa nini alimfanyia hivyo wakati hawana tatizo lolote kati yao,” kilidai chanzo.
Siku nyingine ilidaiwa kwamba Kajala alikwenda nyumbani kwa Wema,
Kijitonyama kwa lengo la kumchukua waende location (sehemu ya kurekodia
sinema), lakini alipofika aliambiwa ‘bimkubwa’ huyo alilala na Diamond
hawezi kuamshwa.
Chanzo hicho kilisema Kajala aliwasiliana na Wema kwa njia ya simu ya
mkononi akamwambia asubiri lakini alikaa kwa muda mrefu bila mafanikio
hivyo hawakwenda kushuti siku hiyo.
Chanzo hicho kilidai pia kwamba ushosti wa wawili hao ulianza
kupepesuka muda mrefu lakini uzi wa mwisho umekuja kukatwa na Diamond
mara baada ya kurudiana na Wema.
0 comments:
Post a Comment