DIAMOND ATAMANI USHOGA!

Diamond alinaswa akiwa amevaa wigi hilo kichwani kisha kupiga nalo picha.
ILIVYOKUWA
NYOTA wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amewashangaza watu kufuatia kuvaa wigi (nywele bandia) la mpenzi wake, Wema Isaac Sepetu, kitendo kilichotafsiriwa kuwa ni dalili ya kutamani mambo ya ushoga.
Hivi karibuni, Diamond alinaswa akiwa amevaa wigi hilo kichwani kisha kupiga nalo picha huku Wema akilitafuta ili alitinge bila mafanikio.
Habari zilieleza kuwa baada ya Wema kutoka nje akiendelea kulitafuta wigi hilo, alipigwa na butwaa kumkuta Diamond amelivaa, tena akionekana kuwa na amani.
Wema Isaac Sepetu na mpenzi wake Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
WEMA AMWANIKA
“Jamani nimetafuta wigi langu muda mrefu sijaliona, nashangaa namkuta baby wangu (Diamond) amelivaa, lakini limempendezaje?” aliandika Wema kwenye ukurasa wake wa Instagram uliotembelewa na watu kibao.

WANACHOAMINI WATU KUHUSU USHOGA
Kitendo cha Diamond kuvaa wigi hilo, wengi wamekichukulia kama ni dalili zake za kupenda kuwa kama demu ambapo kwa mwanaume huitwa shoga, kwa vile wenye tabia hizo wengi walianza kwa kujihusisha na mambo ya kikekike, yakiwemo mavazi.
Emmanuel Adebayor (kushoto) na Diamond Platnumz wakiwa Four Point Hotel, jijini Lagos nchini Nigeria.
“Unajua watu wengi wanaojiingiza katika mambo ya ushoga huanza kwa kutamani kuvaa vitu vya kike kama nguo, hereni, viatu, kujipodoa na vingine vingi,” alisema staa mmoja ambaye hakutaka kutajwa gazetini.

WANAOMFAHAMU DIAMOND
Watu ambao wanamfahamu vizuri mwanamuziki huyo, walisema huenda fedha ambazo ameanza kuzipata hivi karibuni zimekuwa zikimpeleka puta kwa kufanya vitu ambavyo si sahihi.

ALIANZA MUDA
Miezi kadhaa iliyopita, Diamond na Wema walipokutana nchini China, jamaa huyo alipiga picha zilizomuonesha akiwa amevaa cheni ya mpenzi wake huyo na kuziweka kwenye mtandao wake wa kijamii wa Instagram.
Jokate Mwegelo.
SURUALI KAMA YA WEMA, JOKATE
Mwaka jana akiwa nchini Nigeria, Diamond aliingizwa kwenye mitandao ya kijamii kufuatia kitendo chake cha kuvaa suruali yenye mistari ya pundamilia ambayo wachunguzi walibaini kuwa, Wema na Jokate Mwegelo pia wanazo.
Jokate (kushoto) na Wema.
TABIA ZA MASTAA WAKIKAMATA FEDHA
Mastaa wengi duniani wamekuwa na tabia ya kufanya vitu ambavyo ni kinyume na maadili mara baada ya kupata ustaa na kushika fedha nyingi.
Mfano mkubwa, aliyekuwa mfalme wa Pop duniani, marehemu Michael Jackson, yeye alianza kufanya vituko kwa kujibadilisha ngozi na pua  mwaka 1984 ili aonekane mweupe. Ni baada ya kuwika kwenya anga la muziki huku kiasi kikubwa cha fedha kikiingia mfukoni mwake.
Hali hiyo ilimsababishia kupata ugonjwa wa Vitiligo hadi akaaga dunia Juni 25, 2009.

ELTON JOHN
Mwanamuziki Elton John wa Uingereza, naye alijikuta akijibadili na kuwa shoga baada ya kuzikamata fedha nyingi.
Mwaka 1984, Elton John alifunga ndoa na mwanamke aliyeitwa Renate Blauel. Mwaka 1988 walitengana, Elton akajiingiza katika mapenzi ya jinsi moja hadi kufikia hatua ya kufunga ndoa na mwanaume mwenzake, David Furnish mwaka 2005.

WHITNEY HOUSTON
Mwanamuziki mwingine ambaye alijizolea umaarufu mkubwa kutokana  na sauti yake nzuri ni Whitney Elizabeth Houston ambaye baadaye alijiingiza kwenye masuala ya usagaji na matumizi ya madawa ya kulevya ambayo aliyatumia kwa muda mrefu na kumsababishia kifo.
Whitney alifariki dunia mwaka 2013 katika bafu la Hoteli ya Baverly Hills nchini Marekani. Vyombo vya habari vilimwelezea marehemu huyo kuwa, alitumbukia kwenye matumizi ya ‘unga’ kwa sababu ya kumiliki mkwanja mnono akiwa na mumewe, Bobby Brown.

UZOEFU
Uzoefu kwamba mashoga wengi huanza kwa kupenda vitu vya mademu upo kwa baadhi ya vijana Bongo ambao nao ni ‘chakra’. Wengi waliowahi kuzungumza na vyombo vya habari wamekuwa wakisema kuwa walikuwa wakipenda kuongozana, kukaa, kuvaa au kulala kwenye vyumba vya dada zao.

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

Post a Comment

Ungana Nasi, Like Page Yetu Hapa Chini